Ubinafsishaji wa Mashirika ya umma: Zitto, badala ya kumshauri Rais aunde Tume ya Uchunguzi, peleka hoja binafsi Bungeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
NIimesoma kupitia gazeti la Citizen na nimeona unamshauri Raisi aunde Tume kuchunguza ubinafsishaji wa mashirika yote ya umma badala ya kudili na swala la kampuni ya Airtel pekee.

Wapinzani,ifike mahali mbadilike na zaidi mjifunza kwa Nassari na Lema juu ya wito walioutoa kwa mheshimiwa wa kutaka awachukulie hatua wateule wake waliotuhimiwa kuhonga madiwani na alichokuja kufanya mheshimiwa kwa wateule hao.

Nilishawahi kusema na leo narudia,nyinyi kama wabunge wa upinzani pelekeni hoja zenu Bungeni bila kujali zitapokelewa au laa cha msingi wananchi waone juhudi zenu na kisha wapime dhamira ya wana-CCM katika hiki wanachokiita ni vita vya kupambana na rushwa.

Mkipeleke hoja zenu zikakatakiwa au kama Bunge litazipokea na baadae kuja na maazimio alafu serikali ikashindwa kuyatekeleza, basi wananchi watakuwa wamepata majibu na hata nyinyi mtakuwa na hoja za kuwaeleza wananchi kuwa Bunge au serikali imekata hoja zenu hivyo si kwelu hawa mabwana wana nia ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi kama wanavyojinadi.

Zitto unachopawa kufanya ni kupekeka hoja binafsi Bungenj kutaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza mchakato mzima wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma au kulitaka Bunge lipitishe azimio la kuitaka serikali iunde Tume huru kuchunguza huo mchakato.

Tumieni nafasi zenu kama wabunge na wananchi wataona juhudi zenu ndani na nje Bunge na pia watapata nafasi ya kupima dhamira ya wana-CCM.

Yako mambo mengi sana yanakuja na kupita ambayo Bunge lilipaswa kuingilia kati hivyo nyinyi kama wabunge wa upinzani timizeni wajibu wenu wa kupeleka hoja binafsi Bungeni bila kujali kama walio wengi ndani ya Bunge watakwamisha hoja zenu au watazikubali.

Badilikeni.
 
Salaam,

Nimesoma ushauri wako. Nashukuru Sana. Hata hivyo ni vema kujielimisha kwanza mifumo inavyofanya kazi kwanza kabla ya kuona kuwa ushauri wako ni lazima ufuatwe. Naona unatutaka tubadilike, ni jambo zuri lazima tubadilike. Nashauri kuwa na wewe jitazame ubadilike. Umetolea Mfano wa Nasari na Lema kuhusu madiwani kuhongwa. Nadhani mwenyewe umeona matokeo yake ni nini. Jambo hilo limefika wapi? Zaidi ya headlines limeshughulikiwa? Unadhani tuendelee kufanya hivyo hivyo tukijua matokeo ni nini?

Hoja binafsi Bungeni ni rahisi kuitamka kuliko uhalisia wake. Hili ni Bunge la 11, sio la 10 wala la 9. Mimi hapa nina miswada 2 binafsi bungeni toka nimewasilisha haijapiga hatua yeyote. Muswada wa sheria ya Maadili ili kuweka tamko la Mali na Madeni wazi una miaka 2 sasa na muswada wa kuondoa mafuta na gesi kwenye masuala ya Muungano umefika mwaka sasa.

Sisi wabunge tunajua Bunge la sasa lipoje na suala la Hoja Binafsi ni mazoea tu ya kutamka Lakini hakuna litakalotokea.

Kwa kuwa hivi sasa Rais ndio kila kitu na mihimili mingine haifanyi kazi inavyopazwa tuache afanye yeye. Presidential Commission of Inquiry ni njia nzuri sana kwani ni njia ya kisheria kwa mujibu wa sheria. Sio Kamati au Tume za kawaida hizi kama Makanikia nk. Commission of Inquiry ni kama ile ya Jaji Kipenka kuhusu kesi iliyokuja kumshika Zombe. Sio jambo dogo. Nadhani ungejisomea kidogo ungeelewa nini ninapendekeza.

Asante kwa ushauri. Hoja Binafsi Bungeni Kwa sasa haina maana yeyote kwani Bunge ni kibogoyo. Labda kama unataka tusikike tu na sio jambo lifanyike. Endelea kutushauri.
 
Mheshimiwa, kwanza nashukuru kwa kujitokeza na kujibu hoja hii na kwa ulivyojibu wacha niamini utakuwa ni Zitto kweli.

Narudia,kwa sasa nyie timiezeni wajibu wenu bila kujali hivyo vikwazo maana wananchi wataona juhudi zenu na kupima dhamira ya hawa ambao kutwa ni kujisifu tu wakati dhamira zao ni za kutia mashaka.

Pili,kwakuwa mnaambiwa nyinyi kazi yenu ni kupinga kila kitu,sasa onyesheni juhudi za kuwaunga mkono kwa style hiyo alafu muoone kama kweli wako tayari kupokea hoja zenu na wananchi wataendelea kuwapima.
 
Tumeshafanya hivyo sana ndani ya Bunge. Hiyo hoja Binafsi ndugu yangu hata kupangiwa haitapangiwa, nafasi ya kujadiliwa.

Acha tutimize wajibu wetu hivi pia.

Mwaka 2009 Bunge lilipitisha kufanyika kwa post privatization audit kufuatia hoja ya Kamati ya POAC wakati ule. CAG na POAC/PAC tulishatoa Taarifa kadhaa Bungeni kufuatia mashirika mbalimbali ikiwemo hili la Airtel. Wakati tunamaliza Bunge la 10 tulikuwa na Taarifa ya special audit ya privatization ya mashirika 10 ya Umma aliyofanya CAG. NBC ilikuwa kwenye Taarifa hiyo na SPM mgololo. Pia tulifanya extensive work kuhusu ukodishwaji wa Airbus kwa ATCL na Madeni makubwa famba tunayodaiwa. Nasikia Bombardier nyengine ile kubwa C300 imeshawekwa chini ya ungalizi kufuatia deni hili la hawa wa airbus. Tatizo Watanzania wana short memory span lakini ukweli ni kwamba haya mambo yanayosemwa sasa sio mapya maana tulishayaibua na yana maazimio ya Bunge
 
ANGALIA ALICHOANDIKA MHE ZITTO KABWE KWENYE GAZETI LA RAIA MWEMA
Edward michael 0 siasa

zittokabwebungeni.jpg

Mhe Zitto Kabwe

Kinyongo cha Mwalimu kwa NBC halali Zitto KabweToleo la 377 29 Oct 2014 MJADALA wa kuuzwa Benki ya NBC kwa bei ya kutupwa bado haujafa na haustahili kufa mpaka ukweli halisi ufahamike kwa umma. Ukweli kujulikana ni sehemu tu ya Taifa kukua na kujifunza makosa yaliyofanyika. Katika maandiko yangu kadhaa na hotuba zangu katika mikutano ya kisiasa, kitaaluma na hata bungeni nimekuwa nikisema kuwa Ubinafsishaji ni suala ambalo nchi yetu haijalifanyia kazi vya kutosha ili kutorejea makosa. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) tuliwahi kupendekeza mwaka 2009 kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye uchunguzi maalumu kuhusu zoezi hili. Taarifa niliyonayo ni kwamba CAG amefanya kazi hii kwa Mashirika 10 yaliyouzwa na Taarifa amewasilisha kwa Kamati ya PAC. Hata hivyo, ubinafsishaji wa Benki ya NBC haukuwa sehemu ya uchunguzi huu. Kamati ya PAC, ambayo mimi ndiyo Mwenyekiti wake, inayoendelea na vikao jijini Dar es Salaam wiki hii ilikutana na Watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina ambaye ndiye mmiliki wa mali zote za Serikali kwenye Mashirika ya Umma au Kampuni binafsi ambazo Serikali ina hisa. Moja ya suala lililoibua mjadala ni uwezekano wa Serikali kupoteza hisa zake 30% katika Benki ya NBC. Hii inatokana na agizo la Benki Kuu la kutaka mtaji wa benki hiyo kuongezwa kufidia hasara kubwa ambayo NBC ilipata na hivyo kuchota akiba yake (reserves). Kwa kuwa Serikali haikuwa na fedha, iliamua kukopa kwa mbia mwenzake, Benki ya ABSA ya Afrika Kusini, jumla ya shilingi 22.5 bilioni kwa riba ya asilimia 8 kwa mwaka ili kuchangia mtaji wake ndani ya benki hiyo. Iwapo Serikali haitakuwa imelipa mkopo huo mpaka ifikapo Mwezi Machi mwaka 2015, his azote za Serikali katika NBC zitayeyuka (diluted). Mwanzo Ni muhimu kukumbuka kuwa NBC iliuzwa kwa jumla ya shilingi bilioni 15 kwa mujibu wa mkataba wa mauzo. Miniti za kikao cha iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) za tarehe 20 Julai, 1999 zinaonyesha kuwa licha ya serikali kulipwa shilingi bilioni 15, kwa kuwa ABSA watakuwa wamelipa kwa fedha za kigeni (dola za marekani), basi pakiwa na faida yeyote ya mabadiliko (exchange gain) itakwenda ABSA. Faida hiyo ilitokea kwani shilingi iliporomoka mara baada ya mauzo hayo. Pia serikali ilitoa dhamana (bonds) za thamani ya shilingi bilioni 28 kama mtaji kwa benki hiyo. Zaidi pia, fedha ambazo ABSA waliilipa serikali zilitokana na fedha za iliyokuwa NBC katika mgawanyo wa hifadhi ya fedha kati yake na Benki ya Makabwela (NMB). Kimsingi, toka mwanzo kabisa, ABSA walipewa benki bure na wakapewa mtaji wa kuanzia kazi. Pia ABSA walipewa mkataba wa kuendesha benki na pia kusaini mkataba wa ufundi. Kila mwaka tangia mwaka 2000, jumla ya dola za kimarekani milioni saba zinakwenda Afrika Kusini kutoka NBC kama malipo ya gharama za uendeshaji na gharama za kiufundi. Akaunti zote za NBC zipo nchini Afrika Kusini. Suala hili, licha ya kusemwa sana, halijafanyiwa uchambuzi wa kutosha kwani ni suala ambalo linahitaji uchunguzi wa kijinai na hata adhabu kutolewa kwa wote waliohusika na uuzaji wa mali za umma kwa kiwango cha namna hii. Ifahamike kuwa kupinga uporaji sio kupinga mabadiliko ya kiuchumi. Kila nikipata fursa nasema, ‘privatization’ si sawa na ‘liberalisation’ isipokuwa la kwanza limo ndani ya la pili. Kwanini mtaji uliotolewa kwa ABSA kupitia ‘bonds’ za Serikali hawakupewa NBC? Kwa nini kama tatizo lilikuwa ni uwezo wa kuendesha, hatukukodisha menejiment tu? Sasa Kati ya mwaka 2005 na 2008, NBC walianza kutoa mikopo ya magari kwa sekta ya usafirishaji. Mikopo hii ilisababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 137 kwa benki hiyo na kwenye mahesabu ya benki hazikuwa zimeonyeshwa kuwa ni hasara (not provided for) kwa hiyo mizania ya benki ilikuwa inaonyesha mambo safi wakati kuna hasara. Zilipokuja kuwekwa kwenye mizania (imparement), hifadhi (reserve) ya Benki ikaliwa kwa jumla ya shilingi bilioni 50, Benki Kuu ikaingilia kati na kutoa agizo la kuongeza mtaji. Hiki ndio chanzo cha hali ya sasa kwamba kila mbia aweke fedha kulipia mtaji na serikali kuchukua mkopo kulipia mtaji huo. Masuala ya msingi ya kujiuliza ni: Mbia mmoja ni mwendeshaji na kaleta hasara kwa Benki. Ni kwa nini wabia wengine waumizwe na uendeshaji mbovu wa mbia mmoja? Huu mkataba wa uendeshaji hauna adhabu kwa mbia huyu mwendeshaji? Taasisi za uchunguzi wa jinai zilifanya uchunguzi kuhusu mikopo hii ya magari? Haya ni masuala ambayo hayana majibu ingawa kampuni iliyokuwa inatoa mikopo hiyo inajulikana na wakuu wa benki waliohusika na mradi wa hovyo namna hiyo wanajulikana na walipewa bonus zao na kurudi Afrika Kusini. Kamati ya PAC imeagiza mapitio ya mkataba wa mauzo wa Benki na mkataba wa msaada wa kiufundi. Hata hivyo kwa hali ilivyo kuna mengi ndani ya NBC hatuyajui na tunapaswa kuyajua. Kwa wanazuoni, tunaweza kujifunza makubwa zaidi kama mtu akifanya utafiti wa kitaaluma kuhusu kuuzwa kwa Benki ya NBC. Kwa vyovyote vile, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na sababu ya kuwa na nongwa kuhusu suala hili. Alijua tusiyoyajua. Soma zaidi kuhusu: Mwalimu NyerereNBCABSAPAC

Share to:
 
Salaam,

Nimesoma ushauri wako. Nashukuru Sana. Hata hivyo ni vema kujielimisha kwanza mifumo inavyofanya kazi kwanza kabla ya kuona kuwa ushauri wako ni lazima ufuatwe. Naona unatutaka tubadilike, ni jambo zuri lazima tubadilike. Nashauri kuwa na wewe jitazame ubadilike. Umetolea Mfano wa Nasari na Lema kuhusu madiwani kuhongwa. Nadhani mwenyewe umeona matokeo yake ni nini. Jambo hilo limefika wapi? Zaidi ya headlines limeshughulikiwa? Unadhani tuendelee kufanya hivyo hivyo tukijua matokeo ni nini?

Hoja binafsi Bungeni ni rahisi kuitamka kuliko uhalisia wake. Hili ni Bunge la 11, sio la 10 wala la 9. Mimi hapa nina miswada 2 binafsi bungeni toka nimewasilisha haijapiga hatua yeyote. Muswada wa sheria ya Maadili ili kuweka tamko la Mali na Madeni wazi una miaka 2 sasa na muswada wa kuondoa mafuta na gesi kwenye masuala ya Muungano umefika mwaka sasa.

Sisi wabunge tunajua Bunge la sasa lipoje na suala la Hoja Binafsi ni mazoea tu ya kutamka Lakini hakuna litakalotokea.

Kwa kuwa hivi sasa Rais ndio kila kitu na mihimili mingine haifanyi kazi inavyopazwa tuache afanye yeye. Presidential Commission of Inquiry ni njia nzuri sana kwani ni njia ya kisheria kwa mujibu wa sheria. Sio Kamati au Tume za kawaida hizi kama Makanikia nk. Commission of Inquiry ni kama ile ya Jaji Kipenka kuhusu kesi iliyokuja kumshika Zombe. Sio jambo dogo. Nadhani ungejisomea kidogo ungeelewa nini ninapendekeza.

Asante kwa ushauri. Hoja Binafsi Bungeni Kwa sasa haina maana yeyote kwani Bunge ni kibogoyo. Labda kama unataka tusikike tu na sio jambo lifanyike. Endelea kutushauri.

Bila kujali wewe ni Zitto kweli au Zitto photocopy kwani sioni kama ni verified user acha tu nikupe ushauri wangu. Kwa sasa hakuna demokrasia na wananchi wote tunaona. Ila mimi nimeshauri, ninashauri na nitaendelea kushauri kwa sasa ni vyema mkipata nafasi ndogo hiyo hiyo inayopatikana jaribuni kujikita kwenye siasa za maendeleo wangalau kwa 65% na asilimia iliyobaki 35% ndio iwe siasa za madaraka.

Kwanini nasema hivyo? Rais wa sasa sio muumini wa demokrasia na sehemu kubwa taasisi hazifuati sheria bali anachotaka rais. Ndio maana unaona siasa sasa hivi mnafanya anavyotaka rais na sio sheria inavyotaka. Kuna mambo mengi ya kunadi mnapokuwa majukwaani. Mfano kuhakikisha kila familia ya mkulima inakuwa na wangalau heka 2 za kilimo cha kisasa. Kushusha bei za vifaa vya ujenzi ili kila mtu ajenge nyumba bora. Upande wa afya ahidini mtakapopata madaraka mtajenga kila kijiji/kata zahanati. Elimu ni mpaka chuo kikuu bure, kurejesha mahusiano mema kati ya serekali na wafanya biashara. Ajira kwa wingi

Kwenye siasa za madaraka ahidini kufufua mchakato wa katiba mpya tena ya rasimu ya Warioba. Kurejesha demokrasia kama ilivyokuwa kabla ya awamu hii ya tano kuingia madarakani. Hakikisheni mnaweka watu kwenye vipindi vya televisioni na redio wenye kuweza kuhubiri maendeleo na siasa za madaraka. Sasa hivi mnaonekana kuhubiri siasa za madaraka zaidi kwani ccm sasa hivi inawafanya kujihami zaidi kuliko kushambulia huku ccm chini ya Magufuli ikiwa na madhaifu kibao. Maisha ni magumu kumebaki vitisho na uchumi unazidi kudorora.
NB: siku hizi wewe huonekani kwenye mijadala ya TV, sijui shida ni nini. Jipangeni japo tunajua ni ngumu ila tumieni nafasi hiyo finyu kwani tayari udhaifu wa Magufuli kiuchumi na kidemokrasia sasa uko wazi zaidi. Huku kwenye mitandao njoo na hizo verified ID wekeni mambo na sisi tuko nyuma yenu.
 
hii ni hotuba nilitoa bungeni mwaka 2011 kuhusu ubinafsishaji na kuundwa kwa public inquiry

UBINAFSISHAJI WA MASHIRIKA YA UMMA TANZANIAMheshimiwa Spika,
Wizara ya Fedha na Uchumi kupitia Shirika la CHC inasimamia sera ya ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma. Sera ya ubinafsishaji iliyoanza kutekelezwa mwanzoni mwa miaka ya tisini pamoja na kuleta baadhi ya manufaa imekuwa ikilalamikiwa sana siku hadi siku na wananchi. Malalamiko mengi ni kwamba nchi yetu imetekeleza zoezi la ubinafsishaji vibaya, liligubikwa na Rushwa (briberization as termed by Joseph Stiglitz) na uuzaji holela wa mali za yaliyokuwa mashirika ya Umma kama majengo nk.Mheshimiwa Spika, Mashirika ya Umma mia tatu sitini (360) yalibainishwa (specified) kwa ajili ya ubinafsishaji mpaka Disemba 2009.Kati ya Mashirika hayo, Mia Tatu Thelathini na Moja (331)yamebinafsishwa na ishirini na tisa (29) yalikuwa katika hatua mbalimbali za kubinafsishwa. Mpaka muda huo pato la serikali kutokana na ubinafsishaji huo yalikuwa Shilingi billion 482. Hii maana yake ni wastani wa shilingi 1.5 bilioni kwa kila Shirika lililouzwa! Mheshimiwa Spika, ni takribani miaka ishirini sasa toka tuanze kutekeleza sera hiyo na mashirika mengi yakiwa yamebinafsishwa, na hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya tathmini ya kina juu ya utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma (Public Inquiry on Privatisation). Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kuanza mchakato wa kufanya uchunguzi huu ili tuone mafanikio na matatizo ya sera hii kwa ajili ya kujifunza na pale inapowezekana kurekebisha makosa. Wananchi washirikishwe vya kutosha katika mchakato huu.Mheshimiwa Spika, utafiti uliofanywa mwaka 2007 na asasi ya AFRODAD (African Forum and Network on debt and development) ukitolea mfano wa Tanzania katika sera ya ubinafsishaji uligundua kuwa pamoja na matarajio ya serikali kuhusu ubinafsishaji bado haukuwashirikisha wananchi hata katika hatua ya kuwapa taarifa na kuwaelimisha kuhusu sera hiyo na pia wananchi wamekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kuwa hawanufaiki na mafanikio ambayo serikali imekuwa ikiyatoa.Mheshimiwa Spika, zaidi ya hayo ubinafsishaji pamoja na uwekezaji kwa ujumla haujaweza kutanzua tatizo la ajira ambalo linawakumba vijana wengi huku kukiwa na malalamiko kuwa wabia hao wa maendeleo huwaajiri wageni wengi zaidi kinyume na sheria kama ambavyo ilijadiliwa katika hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira.Mheshimiwa Spika, pia mashirika mengi ya umma yaliyobinafsishwa wawekezaji wameshindwa kutekeleza mambo/masharti waliyokubaliana na serikali hii ikiwa ni pamoja na wao kufanya mambo mengine kinyume na makubaliano kwa mfano Kiwanda cha Urafiki Dar es Salaam ambapo mwekezaji kutoka China amekuwa akiuza baadhi ya mashine kama vyuma chakavu, Kiwanda cha kuzalisha mbao cha Tembo Chip board cha Mkumbara mkoani Tanga ambapo mwekezaji alianza kwa kuuza miti ya msitu bila kuendesha kiwanda na hivyo kusababisha mgogoro na wananchi baada ya kuvamia maeneo yao.Mheshimiwa Spika, hiyo ni baadhi ya mifano ambayo inaonyesha kushindwa kwa mashirika/taasisi zilizobinafsishwa hii ikiwa ni pamoja na baadhi ya wawekezaji/wabia kutoa taarifa za uongo/ zisizo sahihi juu ya uwezo wao kufufua na kuendesha taasisi zilizobinafsishwa kwao mathalani kiwanda cha kusindika nyama kilichopo Kawe Dar es Salaama cha Tanganyika Packers.Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza, kama ilivyoelezwa hapo juu, kufanyika kwa uchunguzi maalumu kuhusu Utekelezaji wa sera ya Ubinafsishaji (Public Inquiry on privatisation).Mheshimiwa Spika, Mwezi Juni mwaka huu na katika Mkutano huu wa Nne, Bunge lako tukufu lilijadili na kupitisha Azimio la kuongeza muda wa Shirika la CHC baada ya kufanyia marekebisho Azimio lililoletwa na Serikali ambapo awali kulikuwa na nia ya kuunganisha Shirika hili na Ofisi ya Msajili wa Hazina. Uamuzi huu wa Bunge haukuwafurahisha baadhi ya watendaji wa Serikali. Hivi sasa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la CHC (kaimu) ndugu Methusela Mbajo amesimamishwa kazi kwa tuhuma za majungu kutoka kwa wanaojiita Wafanyakazi wa CHC. Tuhuma hizo ziliwasilishwa kwangu binafsi na kunakiliwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Kufuatia maagizo ya Waziri wa Fedha kwa Bodi ya Wakurugenzi wa CHC Mtanzania huyu kasimamishwa kazi na kwamba CAG ameombwa kuchunguza majungu yale kutoka kwa wanaojiita wafanyakazi wa Shirika la CHC.Mheshimiwa Spika, nilikuandikia barua kukuomba hatua mwafaka zichukuliwe kwani suala hili bado lipo katika mamlaka ya Bunge na kwa mujibu wa Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, sheria namba 3 ya mwaka 1988 Maamuzi haya ya Waziri wa Fedha ni sawa na ‘contempt of Parliament’. Barua ya wanaojiita wafanyakazi wa CHC (niliyoandikiwa tarehe 24 Juni 2011, siku moja baada ya kupitishwa kwa Azimio la Bunge na kutuhumu Mawaziri kuwa walishawishiwa), Barua ya maelekezo ya Serikali (iliyosainiwa na ndugu Mmbaga, Msaidizi wa Waziri Mkuu ya tarehe 10 Agosti 2011) na Barua yangu ya majibu (18 Agosti 2011) niliyowapa zimewasilishwa mezani kwako kama vithibitsho na kwa hatua zaidi utakazoona inafaa.Mheshimiwa Spika,Bunge hili linapaswa kusimama imara kuzuia kuingiliwa kwa mamlaka yake na tawi la Utendaji. Mijadala ndani ya Bunge inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tusipokuwa makini Bunge litaendelea kudharauliwa na hivyo kushindwa kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali ipasavyo. Ninataka maelezo ya kina ya Waziri wa Fedha kwa nini amechukua hatua nilizoeleza hapo juu ilhali akijua jambo hili lipo mezani kwa Spika wa Bunge.
 
Tumeshafanya hivyo sana ndani ya Bunge. Hiyo hoja Binafsi ndugu yangu hata kupangiwa haitapangiwa, nafasi ya kujadiliwa.

Acha tutimize wajibu wetu hivi pia.

Mwaka 2009 Bunge lilipitisha kufanyika kwa post privatization audit kufuatia hoja ya Kamati ya POAC wakati ule. CAG na POAC/PAC tulishatoa Taarifa kadhaa Bungeni kufuatia mashirika mbalimbali ikiwemo hili la Airtel. Wakati tunamaliza Bunge la 10 tulikuwa na Taarifa ya special audit ya privatization ya mashirika 10 ya Umma aliyofanya CAG. NBC ilikuwa kwenye Taarifa hiyo na SPM mgololo. Pia tulifanya extensive work kuhusu ukodishwaji wa Airbus kwa ATCL na Madeni makubwa famba tunayodaiwa. Nasikia Bombardier nyengine ile kubwa C300 imeshawekwa chini ya ungalizi kufuatia deni hili la hawa wa airbus. Tatizo Watanzania wana short memory span lakini ukweli ni kwamba haya mambo yanayosemwa sasa sio mapya maana tulishayaibua na yana maazimio ya Bunge

Hiki ulichofanya sasa ndio kinatakiwa, himiza na wabunge wengine waanze kumwaga mambo yaliyokuwa huko bungeni na yametupiliwa mbali. Zitto sio siri wewe una ushawishi, uzi wako hapa jukwaani unapata wachangiaji wengi. Jaribu kurushia hayo mambo hapa ili kila jambo liwe wazi. Sasa hivi serekali na watu wote waelewa wa mambo wako huku kwenye social media. Rusha jiwe gizani utaona tunavyoshambulia. Huko kwenye magazeti andikeni makala za kukumbushia tena jitahidini zipate front page. Sasa hivi wapinzani tunapambana na serekali inayotumia mabavu ila ina mbinu chache sana za kufanikiwa. Sasa ni nyie kutumia udhaifu huo. Inatakiwa ccm igeuke kuzuia mashambulizi na sio kushambulia kwa propaganda wakati ukweli hauko hivyo. Kama hutojali jaribu kuanzisha uzi kila baada ya wiki kuhusu mambo mliyopigania haswa hayo makampuni. Tutachangia kwa nguvu na tutawapoteza hao ccm. Usishinde Twitter zaidi kwani kule kuna word limit hivyo huwezi kufunguka vizuri.
 
Bila kujali wewe ni Zitto kweli au Zitto photocopy kwani sioni kama ni verified user acha tu nikupe ushauri wangu. Kwa sasa hakuna demokrasia na wananchi wote tunaona. Ila mimi nimeshauri, ninashauri na nitaendelea kushauri kwa sasa ni vyema mkipata nafasi ndogo hiyo hiyo inayopatikana jaribuni kujikita kwenye siasa za maendeleo wangalau kwa 65% na asilimia iliyobaki 35% ndio iwe siasa za madaraka.

Kwanini nasema hivyo? Rais wa sasa sio muumini wa demokrasia na sehemu kubwa taasisi hazifuati sheria bali anachotaka rais. Ndio maana unaona siasa sasa hivi mnafanya anavyotaka rais na sio sheria inavyotaka. Kuna mambo mengi ya kunadi mnapokuwa majukwaani. Mfano kuhakikisha kila familia ya mkulima inakuwa na wangalau heka 2 za kilimo cha kisasa. Kushusha bei za vifaa vya ujenzi ili kila mtu ajenge nyumba bora. Upande wa afya ahidini mtakapopata madaraka mtajenga kila kijiji/kata zahanati. Elimu ni mpaka chuo kikuu bure, kurejesha mahusiano mema kati ya serekali na wafanya biashara. Ajira kwa wingi

Kwenye siasa za madaraka ahidini kufufua mchakato wa katiba mpya tena ya rasimu ya Warioba. Kurejesha demokrasia kama ilivyokuwa kabla ya awamu hii ya tano kuingia madarakani. Hakikisheni mnaweka watu kwenye vipindi vya televisioni na redio wenye kuweza kuhubiri maendeleo na siasa za madaraka. Sasa hivi mnaonekana kuhubiri siasa za madaraka zaidi kwani ccm sasa hivi inawafanya kujihami zaidi kuliko kushambulia huku ccm chini ya Magufuli ikiwa na madhaifu kibao. Maisha ni magumu kumebaki vitisho na uchumi unazidi kudorora.
NB: siku hizi wewe huonekani kwenye mijadala ya TV, sijui shida ni nini. Jipangeni japo tunajua ni ngumu ila tumieni nafasi hiyo finyu kwani tayari udhaifu wa Magufuli kiuchumi na kidemokrasia sasa uko wazi zaidi. Huku kwenye mitandao njoo na hizo verified ID wekeni mambo na sisi tuko nyuma yenu.
Umesoma vzr ulichoandika Kabla hujaposti? hebu rudia tena kusoma kama hujaelewa nitakusaidia
 
Mkuu Salary Slip leo naona umekuja na hoja Hadi umemuibua mwana mpotevu. Naomba Mheshimiwa Rais aendelee kupiga moja baada ya lingine. Ameanza na Madini na sasa ameingia huko kwenye mawasiliano. Naamini baada ya hapo atasonga kwingine. Akipenda na yote Kwa pamoja itakuwa ngumu. Piga moja baada ya jingine. Angusha moja moja twende.
 
Onyesha kosa lilipo kwani tunajifunza kutokana na makosa. Karibu sana kwa ukosoaji.
Okay Kosa nikuwaambia wapeleke
Mijadala kwenye TV natamani kujua ni TV ipi mpaka Sasa inaruhusu kujadili issues Serious zakujenga NCH zaidi yakusifia hata mambo yakijinga... pia kwenye Magazeti mpaka Sasa kuna Gazeti gani la Maana linaruhusu Mijadala Seriously ndugu Kwanza tuwaunge Mkono akina Zitto kwa kufanya kazi kwenye Mazingira magumu ukweli Nchi ningumu sana
 
Mkuu Salary Slip leo naona umekuja na hoja Hadi umemuibua mwana mpotevu. Naomba Mheshimiwa Rais aendelee kupiga moja baada ya lingine. Ameanza na Madini na sasa ameingia huko kwenye mawasiliano. Naamini baada ya hapo atasonga kwingine. Akipenda na yote Kwa pamoja itakuwa ngumu. Piga moja baada ya jingine. Angusha moja moja twende.
Mpaka sasa kuna Tija yoyote? tuanze na Madini
 
NIimesoma kupitia gazeti la Citizen na nimeona unamshauri Raisi aunde Tume kuchunguza ubinafsishaji wa mashirika yote ya umma badala ya kudili na swala la kampuni ya Airtel pekee.

Wapinzani,ifike mahali mbadilike na zaidi mjifunza kwa Nassari na Lema juu ya wito walioutoa kwa mheshimiwa wa kutaka awachukulie hatua wateule wake waliotuhimiwa kuhonga madiwani na alichokuja kufanya mheshimiwa kwa wateule hao.

Nilishawahi kusema na leo narudia,nyinyi kama wabunge wa upinzani pelekeni hoja zenu Bungeni bila kujali zitapokelewa au laa cha msingi wananchi waone juhudi zenu na kisha wapime dhamira ya wana-CCM katika hiki wanachokiita ni vita vya kupambana na rushwa.

Mkipeleke hoja zenu zikakatakiwa au kama Bunge litazipokea na baadae kuja na maazimio alafu serikali ikashindwa kuyatekeleza, basi wananchi watakuwa wamepata majibu na hata nyinyi mtakuwa na hoja za kuwaeleza wananchi kuwa Bunge au serikali imekata hoja zenu hivyo si kwelu hawa mabwana wana nia ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi kama wanavyojinadi.

Zitto unachopawa kufanya ni kupekeka hoja binafsi Bungenj kutaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza mchakato mzima wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma au kulitaka Bunge lipitishe azimio la kuitaka serikali iunde Tume huru kuchunguza huo mchakato.

Tumieni nafasi zenu kama wabunge na wananchi wataona juhudi zenu ndani na nje Bunge na pia watapata nafasi ya kupima dhamira ya wana-CCM.

Yako mambo mengi sana yanakuja na kupita ambayo Bunge lilipaswa kuingilia kati hivyo nyinyi kama wabunge wa upinzani timizeni wajibu wenu wa kupeleka hoja binafsi Bungeni bila kujali kama walio wengi ndani ya Bunge watakwamisha hoja zenu au watazikubali.

Badilikeni.
Wapinzani gani unaowazungumzia?!!
 
Tumeshafanya hivyo sana ndani ya Bunge. Hiyo hoja Binafsi ndugu yangu hata kupangiwa haitapangiwa, nafasi ya kujadiliwa.

Acha tutimize wajibu wetu hivi pia.

Mwaka 2009 Bunge lilipitisha kufanyika kwa post privatization audit kufuatia hoja ya Kamati ya POAC wakati ule. CAG na POAC/PAC tulishatoa Taarifa kadhaa Bungeni kufuatia mashirika mbalimbali ikiwemo hili la Airtel. Wakati tunamaliza Bunge la 10 tulikuwa na Taarifa ya special audit ya privatization ya mashirika 10 ya Umma aliyofanya CAG. NBC ilikuwa kwenye Taarifa hiyo na SPM mgololo. Pia tulifanya extensive work kuhusu ukodishwaji wa Airbus kwa ATCL na Madeni makubwa famba tunayodaiwa. Nasikia Bombardier nyengine ile kubwa C300 imeshawekwa chini ya ungalizi kufuatia deni hili la hawa wa airbus. Tatizo Watanzania wana short memory span lakini ukweli ni kwamba haya mambo yanayosemwa sasa sio mapya maana tulishayaibua na yana maazimio ya Bunge
Zitto,ni hivi my brother,kwakuwa wanajinadi awamu hii ni tofauti na awamu zilizopita,mnachopaswa kufanya nyinyi kama wapinzani ni ku-take advantage ya hali hii na kuibua upya kashifa zote Bungeni na kuitaka serikali ichukue hatua na si kusubiri bwana mkubwa aibue hizi kashifa alafu na nyie ndio muanze kuzijadili.

Mkikomaa na kuibua hizo hoja ndani na nje ya Bunge, najua hawa mabwana hoja hizi kuzishughulikia zitawashinda na ile hoja yao dhaifu kuwa wapinzani kazi yenu ni kupinga kila kitu itakufa kifo cha mende.

Tena ikibidi muwe mnaita waandishi wa habari na kuibua hizo hoja yakiwemo na maazimio kadhaa ya Bunge yaliyotelekezwa kabla ya kwenda kuziibua upya hoja hizj Bungeni ili wananchi wawe na hamu ya kufuatilia.
 
We jamaa bwana! Hizo hoja wakiibua Lowassa na Sumaye wanakuwa wapi?

Yaani unataka kina Zitto waanze kutoboa mtumbwi(Lowasa na Sumaye) ambao wao wenyewe wamepanda?
 
Tumeshafanya hivyo sana ndani ya Bunge. Hiyo hoja Binafsi ndugu yangu hata kupangiwa haitapangiwa, nafasi ya kujadiliwa.

Acha tutimize wajibu wetu hivi pia.

Mwaka 2009 Bunge lilipitisha kufanyika kwa post privatization audit kufuatia hoja ya Kamati ya POAC wakati ule. CAG na POAC/PAC tulishatoa Taarifa kadhaa Bungeni kufuatia mashirika mbalimbali ikiwemo hili la Airtel. Wakati tunamaliza Bunge la 10 tulikuwa na Taarifa ya special audit ya privatization ya mashirika 10 ya Umma aliyofanya CAG. NBC ilikuwa kwenye Taarifa hiyo na SPM mgololo. Pia tulifanya extensive work kuhusu ukodishwaji wa Airbus kwa ATCL na Madeni makubwa famba tunayodaiwa. Nasikia Bombardier nyengine ile kubwa C300 imeshawekwa chini ya ungalizi kufuatia deni hili la hawa wa airbus. Tatizo Watanzania wana short memory span lakini ukweli ni kwamba haya mambo yanayosemwa sasa sio mapya maana tulishayaibua na yana maazimio ya Bunge
nchi inapigwa vita kutoka majirani na within. kuna hawa wauza ndege na maajenti wao
ambao karibu watoane roho kuhusu kupata kandarasi ya kuuza ndege. kuna nchi jirani wanaogopa ushindani usafiri wa unga toka nchi yenye vivutio kama tanzania. azma ya tz kuingia usafiri wa anga hakika inakutana na vikwazo vya kutengenezwa wasiyoitakia nchi yetu wema.
 
Back
Top Bottom