Ubinafsishaji Mashirika ya Umma ulifanyika ili kumuenzi Mwalimu Nyerere?

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
BWM. rest in peace.

Moja ya mambo makubwa aliyofanya hayati Mkapa bila kujali kama yalileta tija au yalitia hasara ni Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.

Kama ilivyozoeleka kwa marais waliofata baada ya Mwalimu Nyerere, mambo mengi wamekuwa wakiyafanya kwa ajili ya nchi na kujinasibu kuwa wanafanya hivyo kumuenzi Baba wa Taifa.

Je, ubinafsishaji wa mashirika ya umma ulikuwa ni sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere?
 
leo ndio nimemuelewa mkapa kabla ya hapo nilikuwa namuona mtu aliyekosea sana,bila kufanya hivo unadhani pesa ingetoka wapi ? ilikuwa lazima abinafsishe ameitoa hii nchi kwenye umasikini sana.tafuta uzi unaoelezea mafanikio yake
 
Je, ubinafsishaji wa mashirika ya umma ulikuwa ni sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere?
Haikuwa, kwani kuna baadhi ya ubinafsishaji JKN alipinga hadharani lakini raisi kama mtu mwenye maamuzi ya mwisho kwenye hili alitaifisha.
 
BWM. rest in peace.

Moja ya mambo makubwa aliyofanya hayati Mkapa bila kujali kama yalileta tija au yalitia hasara ni Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.

Kama ilivyozoeleka kwa marais waliofata baada ya Mwalimu Nyerere, mambo mengi wamekuwa wakiyafanya kwa ajili ya nchi na kujinasibu kuwa wanafanya hivyo kumuenzi Baba wa Taifa.

Je, ubinafsishaji wa mashirika ya umma ulikuwa ni sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere?
Asante kutukumbusha. Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?.
Nawatakia maadhimisho mema na mapumziko mema ya Nyerere Day.

P
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom