Ubinafsi wetu, chanzo kikubwaa cha umasikini wa Tanzania

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Kwa watanzania wengi ukiuliza kwanini Tanzania bado ni masikini watakuambia ni UONGOZI MBAYA. Lakini binafsi nimegundua kuwa, licha ya uongozi wetu, tatizo letu kubwa zaidi ni tabia ya ubinafsi. Watanzania wengi tunapenda kushughulikia matatizo yetu binafsi na hatujali kabisa matatizo ya wengine bila kujua kwamba MATATIZO YA WENGINE YANA IMPACTS KWENYE MAISHA YETU.

Mathalan, wakati wa mgomo wa madaktari, watanzania tumeliacha suala hili kwa madaktar licha ya madhara yaliyojitokeza kwa watanzania, ikiwa ni pamoja na vifo. Hata CHADEMA ambao machoni mwa watanzania wengi wanaonekana kama watetezi wao, bado hawajaungana na madaktari kutoa sauti ya pamoja kulani tatizo hili. Badala yake watanzania tumekuwa mashabiki tu wa MADAKTARI VS SERIKALI.

Hata wakati walimu wanagoma bado suala hili lilibaki kuwa la walimu vs serikali.

Hakuna mkulima anayegoma kwasababu mwalimu anaonewa, mwalimu hagomi daktari akionewa , au mwanafunzi akionewa.
 
Wazee wa siku 100 mpo wapi?. Au ilikuwa geresha? Zimetimia au bado? Watu tumepigika kinoma? WaTZ wamejengewa hofu ili wasihoji udhaifu wa viongozi!. Umaskini na ujinga imekuwa nguzo kuu ya watawala kubaki madarakani.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom