WanaJF,
Wakati wabunge wengine wakitumia pesa za mkopo wa gari kiasi cha milioni 90 za Kitanzania kufanya shughuli za maendeleo na zile za huduma za kijamii majimboni mwao kama vile: kusomesha, kuchimba visima na hata kujenga zahanati, hiyo imekuwa kinyume kabisa kwa Mnyika, maana yeye amedhihirisha ni kwa namna gani ni mbinafsi linapokuja suala la pesa!
Taarifa rasmi kutoka DSE ni kwamba baadhi ya Watanzania waliojaza fomu za kutaka kununua hisa za makampuni mbalimbali, ndugu Mnyika nae ni miongoni mwao! Inasemekana amepanga kununua hisa zenye thamani ya Tsh 90 millioni ambayo inaaminiwa ni pesa aliyoipata kutoka kwenye mkopo wa gari kwa wabunge.
Ifahamike kuwa, Mnyika ni kati ya wabunge vihiyo katika bunge la JMT akifuatana na Kubenea, kwa kuwa wanaamini kuwa ni serikali tu ndio yenye wajibu wa kutoa huduma za kijamii majimboni ila wabunge kazi yao ni kupiga mayowe tu mjengoni. Fikra hii ni potofu sana!
Aidha, baadhi ya wananchi wa Kibamba wameeleza masikitiko yao kufuatia tabia hiyo mbovu ya ubinafsi wa mbunge wao kwa kutoa mifano kuwa, wapo wabunge kadhaa wa CCM wamesikika wakitumia posho zao na pesa ya mkopo wa gari kufanyia miradi mbalimbali ya maendeleo majimboni na pia kutoa huduma za kijamii. Iweje hiyo iwe ngumu kwa mbunge wetu!? Walihoji wananchi wa Kibamba.
Nimalize kwa kutoa wito kwa ndugu Mnyika kwa kujifunza kutoka kwa Zitto na Nassari. Hawa wabunge uwa hawana kawaida ya kusubiri serikali ifanye.Badala yake wao utumia kila raslimali waliyonayo kuchochea maendeleo majimboni mwao. Kafulila, Wenje, Kiwia na Mkosamali wapo kwenye mabenchi kwa sasa hawana ajira. Sasa wewe Mnyika elimu tu ni kidato cha sita, huna uzoefu wa kazi. Hivi ukipigwa chini ubunge utafanya kazi gani mjini hapa? Kuwa makini bwana mdogo.