Ubinafsi wa kitaaluma katika vyuo vyetu-mfano uzamili kwa miaka mitatu (master degree for 3 years) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubinafsi wa kitaaluma katika vyuo vyetu-mfano uzamili kwa miaka mitatu (master degree for 3 years)

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by haki na usawa, Mar 31, 2012.

 1. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwanini vyuo vikuu vyetu vina usanii katika masuala ya msingi na hasa yanayohusu gharama kwa mdhamini anasaidia mlalahoi wa kiafrika kujikomboa kielimu?

  Je wasimamizi wanaowachelewesha wanafunzi kwa kazi zao binafsi kwanini gharama zihamishwe kwa mwanafunzi ili hali mhadhiri kamchelewesha kwakuwa yeye (mhadhiri) kuwa hayupo chuoni kwa kufanya kazi za miradi anayoisimamia kwa manufaa yake?

  Je kwanini na kama si makubaliano wanafunzi walipe gharama ya muda wa ziada baada ya kucheleweshwa na mhadhiri au mhadhiri analipwa kwa idadi ya mwanafunzi kumchelewesha na hivyo kusaidia chuo kupata mapato na yeye kujiongezea kipato?

  Je Mhadhiri mwaafrika anakazi nyingi kuliko Mhadhiri wa kizungu?
  Je kama baadhi ya wahadhiri wao walisoma mwaka mmoja masters zao kwanini hapa kwetu ishindikane? Au roho zao zinauwalakini?

  Baadhi waliweza kupata hata PhD bila kupitia masters kwanini kwetu ni mbinde kumpitisha je wanafunzi wanautafauti gani na nyie mliepewa PhD bila masters? na kwanini kwetu haiwezekani?

  Je wao wanaujuzi mdogo kuliko wazungu ndo maana mwaka mmoja haiwezekani mpaka miaka mitatu ili wajiokoteze vifaa vya kufundishia?

  Naomba waweke wazi katika matangazo yao ili wanaojiunga wajue mapema badala ya kuwavizia kwa kuwaghilibu kuwa ni miaka miwili kumbe ni miaka mitatu?

  Na naomba wapendekeze adhabu kwa watakao wachelewesha wanafunzi kuhitimu kwa muda uliopangwa ili kumaliza tatizo hili?

  Na je bodi ya Elimu ya juu haina wachunguzi wake ili kukomesha tabia hii inayokua kwa kasi nchini na kuenea kama kansa ya titi kwa mwanamke?

  Na kama mhadhiri hawezi kufundisha au kusimamia kwanini asiachwe akafanye kazi ya miradi anayayotaka kama inamlipa kuliko kuajiriwa chuoni na hali anaona maslahi mabaya?

  Kuna wengine hawana hata miradi lakini nao wanasubiri mwishoni waje siku moja na kumaliza kufundisha?

  Je wanaoumia kwa elimu ya namna hii wanasaidiwaje ili kuwaondolea matatizo ya kisaikolojia na warizike kujiandaa kwa gharama za miaka mitatu?

  Nashauri vyuo vyetu vifikiri ili waseme mapema muda wa kumaliza MA/MSC na barua waandike masomo yatakuwa ya miaka mitatu na si miwili na wakiweka mitatu isiwe minne tena kwa vile wako bize sana kuliko wazungu.

  Na wakuu wa vyuo wawe wakali kwa barua/matangazo watakayo yatoa hasa kozi na miaka yake na wawalipishe wahadhiri adhabu kama mwanafunzi wake hatamalima kwa muda uliotakiwa bila sababu ya msingi inayomgusa moja kwa moja mwanafunzi.

  "USHAURI WA BURE KUBORESHA ELIMU YETU" na wadau nisaidieni majibu ya maswali yangu ili nitoe ushauri panahitajika ushauri wa haraka kwa vile hata vyuo vyetu vimekosa DIRA,MALENGO na DHAMIRA katika masuala ya taaluma na ubinafsi kama katika mambo ya kisiasa yanaanza kuibuka vyuoni na juhudi za kujituma zinaisha kwa kasi ya ajabu
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Nice piece
   
Loading...