#COVID19 Ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa unahatarisha mafanikio yanayopatikana kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111334783225.jpg


Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson na serikali yake, wameonyesha msimamo wa ajabu ambao pia unaweza kuonekana kuwa ni ubinafsi, baada ya kuweka kipaumbele zaidi kwenye uhuru wa watu na hali ya uchumi, na sio maisha na usalama wa afya ya wananchi.

Mwanzoni Bw. Boris Johnson alishutumiwa vikali kwa kusema “acha maiti zijazane” lakini ataendelea na njia zake za kupambana na COVID-19, njia ambazo wanasayansi walishutumu kuwa haziendani na uhalisia wa changamoto za janga hili. Bw. Johnson na wanasiasa wenzake wa mrengo wa kulia, walikuwa wakisikiliza zaidi maoni ya waungaji mkono wao kisiasa ya kutaka vizuizi vya COVID-19 viondolewe, maoni ambayo si sahihi.

Kisingizio kinachotumika ni kuwa, kama hatua za kuzuia zikiendelea kwa muda mrefu hata baada ya chanjo kutolewa uchumi utaathirika. Imekuwa ni rahisi kwa Bw. Johnson kutumia kisingizio hicho ambacho kinaeleweka kwa wataalamu wa uchumi, lakini wataalam wa afya wanajua kuwa kama watu wakiambukizwa na kufa kwa ugonjwa huo uchumi kwao unakuwa hauna maana yoyote.

Lakini hivi karibuni yametokea mambo mawili ambayo yanafanya mapambano ya jumla ya janga la COVID-19 duniani kuwa na utatanishi zaidi, na kufanya ushindi dhidi ya janga hilo kwa dunia uwe mbali zaidi. Kwanza ni matukio yaliyotokea wakati wa fainali za EURO 2020 Julai 11 mjini Wembley, ambapo mashabiki wa soka walionyesha vitendo ambavyo ni kinyume kabisa na kanuni za kupambana na COVID-19, ikiwa ni pamoja na kufanya mkusanyiko mkubwa kupita kiasi na kutovaa barakoa. Hali hii bila shaka ni hatari kubwa katika kueneza maambukizi, na kweli baada ya hapo serikali ilitangaza kutokea kwa ongezeko kubwa la maambukizi ya kila siku.

La pili ambalo limewasikitisha wanasayansi, ni kuwa, tarehe 19 Julai, siku 8 tu baada ya fainali za EURO 2020 na wakati serikali imetangaza kuwa kuna ongezeko la maambukizi ya COVID-19 aina ya Delta, Bw Johnson alitangaza kuondoa vizuizi vyote vya kupambana na janga hilo, na kutaka watu wachukue tahadhari wenyewe. Ameamua hivyo wakati takwimu zinaonesha kuwa idadi ya maambukizi imekuwa kubwa zaidi tangu mwezi Februari, na katika wiki iliyopita watu zaidi ya 44,000 likiwa ni ongezeko la 35.8% waliripotiwa kuambukizwa.

Inawezekana ni rahisi kusema kuwa kila nchi ina haki ya kujiamulia yenye njia yake ya mapambano dhidi ya COVID-19, lakini tusisahau kuwa janga hili ni msiba kwa dunia nzima. Muda mfupi baada ya taarifa za kuongezeka kwa maambukizi nchini Uingereza, baadhi ya nchi (Marekani) zilianza kutoa tahadhari kuhusu kwenda au kupokea watu kutoka Uingereza, kwa hofu kuwa Uingereza itakuwa chanzo kikuu cha kuenea kwa virusi aina ya Delta.

Inawezekana kuwa Bw. Johnson amefanikiwa kuwafurahisha wapiga kura wake kwa kufanya uamuzi wanaotaka. Lakini ukweli ni kwamba hata yeye mwenye anajua uamuzi huo alioufanya kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa, ni hatari kwa usalama wa afya ya umma duniani, na pia inaonekana kuwa ni hatari hata kwa afya yake mwenyewe, kwani inasemekana kuna hatari ameambukizwa kwa mara ya pili na anatakiwa kujitenga.

Hatua za pamoja za dunia nzima, ikiwa ni pamoja na utoaji wa chanjo vimeonekana kuleta matumaini kuwa janga hili linaelekea ukingoni, lakini ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa, unaleta utatanishi kwenye juhudi za dunia kupambana na janga la COVID-19.
 
Kama watanzania tujiandae vyema kwenda kuchomwa chanjo dhidi ya Corona.

#NaisuburiKwaHamuChanjoHiyo
 
Back
Top Bottom