Ubinafsi ni kansa inayovimaliza vyama vikuu vya upinzani

Developer IOS

JF-Expert Member
Jun 20, 2017
1,457
1,409
Habari wakuu natumaini wote ni wazima na wenye afya nzuri kama kuna mtu anasumbuliwa na maradhi mwenyezi mungu amponye haraka.Tangu nchi yetu iingie katika mfumo wa vyama vingi hakuna chama cha upinzani kilichowahi kushinda uchaguzi mkuu tumeshuhudia vyama vikiibuka na kuwa ya soda ambayo haidumu kwa miaka mingi na vinakosa mwendelezo wa mipango ya kushinda uchaguzi zaidi vinaonekana kila uchaguzi vinajaribu jaribu tu.Je ukiachana kazi nzuri anayoifanya mh Rais na ccm mpya je upinzani unakwama wapi?

Ubinafsi umekuwa kansa kubwa sana kwenye vyama vyetu vya upinzani ukianza kwenye swala la madaraka ndani ya vyama vyao hadi kwenye sera zao,Tukianza kuangalia kwenye swala la madaraka utagundua kuwa waliokuwepo madarakani wameshajiaminisha na kuwaaminisha wengine hakuna mwenye uwezo wa kuongoza zaidi ya wao hivyo hawana utaratibu mzuri wa kuwaandaa vijana kuja kushika nafasi zao.Tuangalie kwa cdm kwenye nafasi kama mwenyekiti amabaye hana dalili za kutoka,Issue ya zito kabwe pamoja na jinsi mrithi wa slaa alivyopwaya cuf hvyo hvyo kwa maalim seif analivyopambana na hamad rashid na kumuua duni kisiasa.

Tukija kwenye sera zao utagundua sera zao ni za kibinafsi zina lengo kubwa sana la kuwajenga kisiasa sio kuwasaidia wananchi.Mfano mkubwa utaona hoja kubwa cdm na upinzani ambayo wanaiongea na kuitegemea kuingia nayo kwenye uchaguzi wa 2020 ni uminywaji wa demkrasia.Uminywaji huo ni kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima jambo ambapo ukiangalia hoja hii ina political interest sana sio public interest ilihali kwa kiasi kikubwa ccm watakuja na hoja kama kupeleka umeme vijijini hoja ambayo ni public interest sio political interest je unahisi mwananchi atachagua nini kati ya mikutano ambayo ni porojo tu au umeme vijijini ambao ni maendeleo?

Mwisho upinzani wapo tayari kufanya lolote hata kuuza nchi ili wapate madaraka bila hata ya kujiuliza je wataweza kuafford kulipa price.Ukiangalia viongozi wa upinzani wapo radhi kuona hata watanzania wakiteseka kufa au hata kuungana na shetani kama kitawawezesha kuingia madarakani bila kuangalia impact yake.Tumeshuhudia kilichotokea 2015 kwa lowassa wakakubali kumpoteza dr slaa kwa ajili ya lowassa.Pia tumeshuhudia lissu akijitahidi kuomba mataifa makubwa kuwekea nchi yetu saction ili wananchi wateseka waichukie serikali yao na wao wapate mtaji wa kisiasa bila kuangalia watanzania wangapi watakufa kwa kukosa arv,wamama wangapi watakaokufa kwa kukosa huduma za mama na mtoto pamoja na malaria.Ubinafsi utafanya wananchi tukose imani na vyama vyetu vya upinzani
 
kwa siku unaanzisha mada ngapi za kuhusu upinzani, na je huwa unajipa muda wa kuzifanyia tathmini mada zako ili kuona jinsi ambavyo jamii imezipokea?
 
Mbona hueleweki Mara JamiiForums ,Mara wapinzani wanataka nchi iwekewe vikwazo ,ccm iliingia mikataba ya madini na gesi ya nchi kupata 3% ya mrahaba wapinzani ndio waliotia sahihi mikataba ?uwe na aibu mataga wa Lumumba .
 
Back
Top Bottom