Ubinafsi na Uvumilivu haba baina ya wazazi vinapelekea idadi ya Single-parent children kuongezeka.

JustusAugust

Member
Oct 5, 2019
18
20
Salaam wanajamvi la JF.
Ukienda kwenye vituo vya elimu za watoto wadogo, awali, msingi na kuendelea ukapata wasaa wa kuzungumza na watoto au walimu utapata kufahamu kuwa watoto ambao wanaishi au kulelewa na mzazi mmoja au mzazi wa kambo au mzazi wa kufikia inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Ukienda kwenye vituo vya hudumaza kliniki ya mama na mtoto vya kabla na baada ya kujifungua pia utaona kuwa idadi ya wanaopata kigugumizi kwenye kuandika jina la baba wa mtoto linavyoongezeka.

Ukikaa kwenye ofisi za ustawi wa jamii, serikali za mitaa, mahakamani na kwenye madawati ya jinsia na watoto napo utaona vuta nikuvute kwenye kupigana kupata matunzo ya watoto ambao wanalelewa na mzazi mmoja.

Ukienda kwenye nyumba za ibada, sehemu za maombezi, na kwa washauri wa masuala ya kiroho nako utakutana na kundi la watu wanaovutia upande wao kwenye kutaka kubaki na uhalali wa kulea watoto wao peke yao...

Kundi la watoto hawa siliunganishi na wale ambao ni yatima (ambao wazazi wameshatangulia mbele ya haki).

Sababu zilizo nyuma ya suala hili la Single Parent Children ni nyingi sana na baadhi ya sababu hizo zina urandani au ufanano kama zikiangaliwa kwa undani. Kwenye uzi huu nitajikita kwenye hizo mbili ambazo nimezitaja hapo mwanzo 1. Ubinafsi wa kujiangalia wewe na kupuuza hali na nafasi ya mtu mwingine: pamoja na 2. Uvumilivu haba kwenye yale ambayo hayaendani na matarajio yetu; ambavyo zinapelekea watoto kubaki wakijiuliza maswali mengi ya kwanini mimi sihishi na baba yangu au kwanini yule anaishi na baba yake: kwanini huyu mama ananiambia kuwa mimi siyo mtoto wake au kwanini nimuite huyu mama wakati mama yangu namfahamu au kwani mtu anakuwa na mama wangapi...???

Uhai ni zawadi kutoka penye chanzo cha maisha yetu na zinahitajika nafsi mbili zizlizo hai zikutane na kuleta matokeo ya uhai wa kiumbe kingine cha aina ya hizo nafsi zilizoungana. (Hii inaweza kuelezwa kisayansi na kiimani pia). Hakuna mtoto ambaye anapatikana kutoka kwa mzazi mmoja, bali wazazi wawili iwe kwa kukubaliana au vinginevyo. Zipo sababu mbalimbali zilizo nyuma ya kuzaliwa kwa kila umuonaye hapa duniani. Ila kwa hapa hatutajikita kwenye sababu hizo, bali kwenye kutunza, kulea na kukuza huyu aliyekwisha patikana kwa sababu yoyote iwayo.

1. Ubinafsi wa wazazi. Mtu anapokosa hisia za kujali hali, hisia na mahitaji ya mtu mwingine, ataamua kufanya kile ambacho kinamfurahisha au kumfariji kwa wakati ambao anajifikiria yeye. Mara nyingi faraja au furaha ambayo imekuwa ikipatikani imekuwa ni ya muda mfupi ikilinganishwa na uzito wa maumivu au madhara yatokanayo na kutaka kujifurahisha. Wazazi ambao wamekuwa wakijiangalia wao wenyewe wamekuwa wakiwanyima watoto wao haki au uhuru wa kuwa karibu na mzazi mwingine kwa sababu mzazi mmoja ni mbinafsi. Hii inaendana na kupuuza matokeo ya maamzi yao kwa watoto wao. "... nilikaa nikajitafakari sana, nikafikia uamzi wa kufunga na kuomba ili Mungu anioneshe njia katika hili, kweli badae nikafunuliwa wazo la kwamba natakiwa niachana na huyu mwenza wangu...niendelee na maisha yangu... sitakosa uwezo wa kumtunza mwanangu... na hata hivyo sikuwahi kuona anachonisaidia kwenye matunzo ya mtoto wangu... hafai kuwa mzazi... ananifanya nakosa amani muda wote... hanipendi... japo anajifanya kumpenda mtoto..."

"...nilimpenda sana yule mdada... nilitumia nguvu nyingi ili anikubalie... japo nilifahamu kuwa siwezi kumuoa... tulizoea kukutana kimwili hatimaye akapata ujauzito... lakini bado hiyo isingekuwa sababu ya mimi kumuoa... alinichukia hadi sasa sina hata access ya kumuona mtoto wangu..."

"...alikuwa akinipa kila ninachotaka, hatimaye nikapata mimba... niliogopa kumwambia... badae akagundua... hatimaye akajakuniona muhuni ambaye natembea na wanaume wengi... akaniacha na mimba kubwa... mwanangu sasa ana miaka 3 na naendelea kupambana... anavaa vizuri... anakula vizuri na kulala pazuri... hana anachokosa..."

Hiyo hapo juu ni mifano ambayo ukiiangalia kwa undani ina ubinafsi nyuma yake.

2. Uvumilivu Haba.
Kosa linapotendeka haliondoki hivihivi, bali linatuachia alama ya ukumbusho (makovu, majuto, kupoteza kitu au mtu...nk)
Tunapokosea kwenye maisha na kufanya machaguo mabaya inabidi tuwe wavumilivu kwenye matokeo tutakayopata. Hii ni ngumu na inaweza isiingie akilini mwa wengi.

Wazazi wanashindwa kukubali kuwa walikosea wao kwanza na wanakataa kuvumilia matokeo mwisho wa siku wanaishia kufanya maamzi ambayo yanawapa faraja ya muda mfupi na kuwatesa watoto au hata wao kwa miaka nenda miaka rudi. Kushindwa kuvumilia mapungufu ya mwenzako, kushindwa kuvulimilia hali na nyakati ngumu, kushindwa kukubali kuteseka ili kulinda maslahi ya mwingine (mtoto) kishidwa kuvumilia yasiyovumilika basi imepelekea kuongezeka kwa kundi la watoto wanaoishi kwa kumuona au kumtegemea mzazi mmoja.

"...nilimvumilia sana sema tu yeye hakuwa mtu wa kutambua...: hapana kwakweli nisingeweza kuvumilia...: akha mwenzenu sijaiba kwetu...: ...nina kazi yangu na kipato changu, cha kufia nini?...: ...wazazi wake... marafiki zake... tabia yake sasa... "

Nakubali na kuheshimu kuwa nyakati zimebadilika ya sasa siyo sawa na ya zamani... na yajayo hayatakuwa sawa na ya sasa. Ila maamzi ya sasa yatatufanya tuyakumbuke na yawezekana tukayajutia huko mbeleni (siyo wote watakao juta).

Kwa sasa naishia hapa... nikipata wasaa wengine nitakuja kuendelea na sababu nyingine na tutapata mwendelezo kwenye madhara ya kulelewa au kuishi na mzazi mmoja.

Justus August
(Mwanasaikolojia)
0756628773
Dar es Salaam
 
Nitaisoma yote labda Magufuli akishatoka madarakani.
Kwa leo nisamehe tu.
 
Salaam wanajamvi la JF.
Ukienda kwenye vituo vya rlimu za watoto wadogo, awali, msingi na kuendelea ukapata wasaa wa kuzungumza na watoto au walimu utapata kufahamu kuwa watoto ambao wanaishi au kulelewa na mzazi mmoja au mzazi wa kambo au mzazi wa kufikia inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Ukienda kwenye vituo vya hudumaza kliniki ya mama na mtoto vya kabla na baada ya kujifungua pia utaona kuwa idadi ya wanaopata kigugumizi kwenye kuandika jina la baba wa mtoto linavyoongezeka.
Ukikaa kwenye ofisi za ustaei wa jamii, serikali za mitaa, mahakamani na kwenye madawati ya jinsia na watoto napo utaona vuta nikuvute kwenye kupigana kupata matunzo ya watoto ambao wanalelewa na mzazi mmoja.
Ukienda kwenye nyumba za ibada, sehemu za maombezi, na kwa washauri wa masuala ya kiroho nako utakutana na kundi la watu wanaovutia upande wao kwenye kutaka kubaki na uhalali wa kulea watoto wao peke yao...

Kundi la watoto hawa siliunganishi na wale ambao ni yatima (ambao wazazi wameshatangulia mbele ya haki).

Sababu zilizo nyuma ya suala hili la Single Parent Children ni nyingi sana na baadhi ya sababu hizo zina urandani au ufanano kama zikiangaliwa kwa undani. Kwenye uzi huu nitajikita kwenye hizo mbili ambazo nimezitaja hapo mwanzo 1. Ubinafsi wa kujiangalia wewe na kupuuza hali na nafasi ya mtu mwingine: pamoja na 2. Uvumilivu haba kwenye yale ambayo hayaendani na matarajio yetu; ambavyo zinapelekea watoto kubaki wakijiuliza maswali mengi ya kwanini mimi sihishi na baba yangu au kwanini yule anaishi na baba yake: kwanini huyu mama ananiambia kuwa mimi siyo mtoto wake au kwanini nimuite huyu mama wakati mama yangu namfahamu au kwani mtu anakuwa na mama wangapi...???

Uhai ni zawadi kutoka penye chanzo cha maisha yetu na zinahitajika nafsi mbili zizlizo hai zikutane na kuleta matokeo ya uhai wa kiumbe kingine cha aina ya hizo nafsi zilizoungana. (Hii inaweza kuelezwa kisayansi na kiimani pia). Hakuna mtoto ambaye anapatikana kutoka kwa mzazi mmoja, bali wazazi wawili iwe kwa kukubaliana au vinginevyo. Zipo sababu mbalimbali zilizo nyuma ya kuzaliwa kwa kila umuonaye hapa duniani. Ila kwa hapa hatutajikita kwenye sababu hizo, bali kwenye kutunza, kulea na kukuza huyu aliyekwisha patikana kwa sababu yoyote iwayo.

1. Ubinafsi wa wazazi. Mtu anapokosa hisia za kujali hali, hisia na mahitaji ya mtu mwingine, ataamua kufanya kile ambacho kinamfurahisha au kumfariji kwa wakati ambao anajifikiria yeye. Mara nyingi faraja au furaha ambayo imekuwa ikipatikani imekuwa ni ya muda mfupi ikilinganishwa na uzito wa maumivu au madhara yatokanayo na kutaka kujifurahisha. Wazazi ambao wamekuwa wakijiangalia wao wenyewe wamekuwa wakiwanyima watoto wao haki au uhuru wa kuwa karibu na mzazi mwingine kwa sababu mzazi mmoja ni mbinafsi. Hii inaendana na kupuuza matokeo ya maamzi yao kwa watoto wao. "... nilikaa nikajitafakari sana, nikafikia uamzi wa kufunga na kuomba ili Mungu anioneshe njia katika hili, kweli badae nikafunuliwa wazo la kwamba natakiwa niachana na huyu mwenza wangu...niendelee na maisha yangu... sitakosa uwezo wa kumtunza mwanangu... na hata hivyo sikuwahi kuona anachonisaidia kwenye matunzo ya mtoto wangu... hafai kuwa mzazi... ananifanya nakosa amani muda wote... hanipendi... japo anajifanya kumpenda mtoto..."
"...nilimpenda sana yule mdada... nilitumia nguvu nyingi ili anikubalie... japo nilifahamu kuwa siwezi kumuoa... tulizoea kukutana kimwili hatimaye akapata ujauzito... lakini bado hiyo isingekuwa sababu ya mimi kumuoa... alinichukia hadi sasa sina hata access ya kumuona mtoto wangu..."
"...alikuwa akinipa kila ninachotaka, hatimaye nikapata mimba... niliogopa kumwambia... badae akagundua... hatimaye akajakuniona muhuni ambaye natembea na wanaume wengi... akaniacha na mimba kubwa... mwanangu sasa ana miaka 3 na naendelea kupambana... anavaa vizuri... anakula vizuri na kulala pazuri... hana anachokosa..."

Hiyo hapo juu ni mifano ambayo ukiiangalia kwa undani ina ubinafsi nyuma yake.

2. Uvumilivu Haba.
Kosa linapotendeka haliondoki hivihivi, bali linatuachia alama ya ukumbusho (makovu, majuto, kupoteza kitu au mtu...nk)
Tunapokosea kwenye maisha na kufanya machaguo mabaya inabidi tuwe wavumilivu kwenye matokeo tutakayopata. Hii ni ngumu na inaweza isiingie akilini mwa wengi.

Wazazi wanashindwa kukubali kuwa walikosea wao kwanza na wanakataa kuvumilia matokeo mwisho wa siku wanaishia kufanya maamzi ambayo yanawapa faraja ya muda mfupi na kuwatesa watoto au hata wao kwa miaka nenda miaka rudi. Kushindwa kuvumilia mapungufu ya mwenzako, kushindwa kuvulimilia hali na nyakati ngumu, kushindwa kukubali kuteseka ili kulinda maslahi ya mwingine (mtoto) kishidwa kuvumilia yasiyovumilika basi imepelekea kuongezeka kwa kundi la watoto wanaoishi kwa kumuona au kumtegemea mzazi mmoja.

"...nilimvumilia sana sema tu yeye hakuwa mtu wa kutambua...: hapana kwakweli nisingeweza kuvumilia...: akha mwenzenu sijaiba kwetu...: ...nina kazi yangu na kipato changu, cha kufia nini?...: ...wazazi wake... marafiki zake... tabia yake sasa... "

Nakubali na kuheshimu kuwa nyakati zimebadilika ya sasa siyo sawa na ya zamani... na yajayo hayatakuwa sawa na ya sasa. Ila maamzi ya sasa yatatufanya tuyakumbuke na yawezekana tukayajutia huko mbeleni (siyo wote watakao juta).

Kwa sasa naishia hapa... nikipata wasaa wengine nitakuja kuendelea na sababu nyingine na tutapata mwendelezo kwenye madhara ya kulelewa au kuishi na mzazi mmoja.

Justus August
(Mwanasaikolojia)
0756628773
Dar es Salaam
Waumini wa kilokole 75% ni singo maza kwanini ?
 
Sina uhakika sana na data ambazo umezitumia hapa, na hiyo inaninyima uhuru wa kuijibia... lakini ninachoweza kusema ni kwamba Binadamu siku zote hukimbilia penye wepesi endapo watalinganisha upande mmoja mgumu na mwingine pana wepesi. Walio kwenye anguko (crisis) wana tabia ya kukimbilia panapodhaniwa kuwa na faraja hata kama ki uhalisia hakuna faraja.
 
Sio Singo mother tu, wapo na wengine ambao umri umekwenda na hawajaolewa wanakuwa wacha Mungu sana. Ila wakipata wachumba na kuolewa huachana na ulokole.
Sasa olewako uje ukamuoe huyu singo maza wa kanisani, kwa kisingizio cha buana kukuwotesha ndotoni, utajutia the whole of your life.....kwenye kuoa huruma weka pembeni ni ushauri tu
 
Rebeca plz leta mada yako unayo taka..... jf we discuss hot contemporary issue in the society, kama hiyo ya singo maza wathirika ni wengi wengi tunaichukia ila hatuna jinsi

hata km ni contemporary issue,ndio iwe hio kila siku?? hakuna mengine kabisaa ya ku discuss ?
 
Back
Top Bottom