Ubinafsi na Dharau ya Washkaji/Machalii wa Arusha kwa WanaDSM

Kule Kwetu

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,157
1,893
Habarini Wadau,

Kwa uzoefu wangu binafsi na utafiti (usio rasmi sana) nimegundua kuwa Washkaji wengi wa Arusha huwa hawawakubali sana wana wa Dsm, huu ni utafiti uliotoka kwenye locations nyingi za Arusha, na nimegundua kuwa watu wa Arusha wana tabia zifuatazo,ambazo pia wanadsm wanazilaumu:-

1) UBINAFSI NA DHARAU KWA WANADSM:- Machalii wengi wa Arusha wanawadharau sana wanadsm, yaani hata kwenye shule za boarding na mitaani ni rahisi sana Chalii wa Arusha kuwa close na washkaji wa kanda ya ziwa kama Mwanza kuliko wa Daslam.

Yaani masela wa Arusha wanawaona wanaume wa Dar kama wanawake vile.

2) UBABE KWA WANADSM:

Kuna ukweli kabisa kuwa wana wa dsm wakipoa Arusha huwa hawawi na amani kivile. Mfano mzuri kuna siku tulikuwa pande za kule sakina bar na washkaji kadhaa tuliosoma nao chuo,sasa kuna mshkaj wetu alikuwa na lafudhi ya kidarislam akawapa hi fresh masela flan wa Arusha walioingia na migololi ya kimasai ila chalii mmoja wa Arusha akajibu

"usinletee usoro we boya" mara akasema "Huku ni hiphop sio bongofleva kama kwenu"

wakati hata hakujaongelewa habari ya muziki.

3) MAPOZI KWA WATU WA MIKOANI:

Sio siri kuna tabia wanayo washkaji wa Arusha...ukiwa wa mkoani halafu ukienda pande hizo zao kama huna pesa au hakukubali kivile hata kukukaribisha pande zao wanazoishi au kukushirikisha kwenye Areas za kulia bata hakuna, yaani wako kivyao. Sisi wote ni wanaume hizo ni pozi ambazo sizo kabisa.

Nawasilisha,
 
Unaowaita wa dar es salaam wanadharaukika na kila mtu wa mikoani..i,e wengi wenu ni wajinga,waoga,viherehere,wapuuzi,hamjitambui,...etc.
Anyway_hata mimi ninaishi dar ila wakaazi wa dar na hasa wanaume wengi wao ni bure kabisa.
Cc
@Preta,Filpo,Easymutand,Lp,..
 
Hapa na mie niwe mkweli; huwa nikimsikia mwanaume anaongea kwa sauti ya kuchonga chonga/ya kimayai mayai/ya kulegea legeaa.k.a. ya ki daslam daslam zaidi ya salamu huwa sijisikii kupiga nao stori yoyote huwa najua wanaume wa hivi sio watu wa kazi na hata akinipiga mwiba wa hela ya kula huwa nawapa bila hata kinyongo naona kama wanastahili kuhudumiwa.
 
arusha wanapenda story za kiume ngumuu kwa expirience yangu ya kukaa nao kusoma nao sasa wengi wao wa kutoka dar pwani na moro wanakuwa waongeaji sanaa af wnakuwa easy kuongea story za jokes mademu mademu kucheka cheka sasa like unakuta wa atown wanapenda story maybe "kuzungumzia jins ya life hustling kama mwanaume" lakin unakuta huyu wa mikoa ya pwani analeta mambo ya kutaka kuwekwa ndani na jimama au sjui dume zima unakuta linasifia chps za kinondoni kwa mpemba tamu kshenzi...na kuna mtu kacoment abt unakuta wana kwambia sjui mtu wa dar sjui kaza huku ni hiphop huyo mtu aliyecoment kuwa sjui hiphop inatoka wapi kati hawazungumzii mziki tambua kwmba hiphop anayoongelea pale ni ni lifestyle thts y hiphop si mziki tu.vjana wengi wa arusha wanaamini ktka hiphoplifestyle.so matokeo yake yanakuja kuzalisha hizo impact kma kuona upande mmoja wanadharau...sasa cha kushngaza ukutane na mkurya aliyetoka kanda ya huko na wa kaskazini..
 
Kwani uwongo?
Wanaume wa daslamu wengi wao "Mayai mayai" Nakumbuka ile issue ya jamaa aliingia na kisu kwenye daladala wanaume wote wakamkimbia mpaka mwanamke akakikamata akamnyang'anya. Angekuja arachuga aonyeshwe. Halafu, issue za panya road , vitoto viko na mapanga vinatishia mji mzima, wanaume na vitambi vyao wanaingia chini ya meza za bar. (Huo upuuzi hauwezi kutokea Arachuga) Komaeni watoto wa kiume, sijui ni hizo chipsi yai? Njooni mnywe "trupa" na nyama kwa Morombo muone kama hamtakuwa morani.
 
kuna ka ukweli fulani ila kanatokana tu na baathi ya watu wachache sana kutokujiamini wawapo ndani ya arusha ambao wao huwa na fikra tofauti kuhusu arusha.
pia vijana wengi wa arusha ujiamini sana kulingana na kazi zao ambazo huwakutanisha na watu mbalimbali kutoka hata mataifa mbalimbali.
jambo jingine ni hata mazingira ya ya arusha,wengi walizaliwa huku wamekuwa na tabia ya kijichanganya sana bila ya kujali uwezo wa mtu.
lakini wa dzm wote kama ukijiamini utaonekana wa kawaida sana na hata mtu wa arusha akienda dar na akiwa muoga muoga ni lazima tu aonekane mshamba.
 
Back
Top Bottom