Ubinafsi katika matatizo unatuumiza Watanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubinafsi katika matatizo unatuumiza Watanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, Jul 31, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kila kona ya nchi sasa hivi kuna vilio. Sio watoto sio wazee, si kina mama si kina baba wote wanalia. Wanalia juu ya hatma ya maisha yao yatakuwaje. Wengi hawajui kesho wataamka vipi.

  Lakini cha kushangaza kila mmoja amekuwa akilia kivyake. Madaktari walipolia kada zingine walidhani ni msiba wa madaktari tu, wafanyakazi wamelia juu ya sheria ya pensheni sauti zimewakauka wamebaki kimya, wazee vijijini wamelia kupanda kwa bei ya sukari mpaka mishipa ya usoni imewasimama hakuna mtetezi. Leo walimu wanalia tunadhani ni msiba wa walimu tu. Hivi inakuwaje watanzania tusiguswe na matatizo ya jamii nzima. Hivi hatujui kwa njia moja ama nyingine msiba wa jirani ni msiba wako pia?

  Wananchi tuamke, tumetoa sauti makoo yametukauka, tuungane pamoja kudai haki zetu hata kwa kuingia barabarani. Mvuvi wa samaki ukerewe akipata matatizo hata wewe ulie songea unaathirika pia.
   
Loading...