Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Hii nchi chini ya watawala Wala rojo tunadanganyanya! Ilitakiwa iendelee kuwa chini ya mvuta bangi mmoja atunyooshe sema yaonesha Mungu Malaika walimzinguua Sana kuliko Watanzania hapa Duniani akamchukua kichaa wetu akawachunge Malaika.
 
Mtoa mada umeona vyema. Lakini tufanye nini ili mambo kama haya yakomeshwe. Wapi tunakosea kiasi cha kuchezewa na wawekezaji uchwara?
Tunahitaji katiba mpya.. Hizi sheria mbovu za uwekezaji zinatumiwa vibaya na wawekezaji wahuni kwa msaada wa watu wetu wenyewe tuliowakasimu nafasi za kusimamia tunu za taifa.. Hatuwajibishani wala hatuna uwezo wa kuwafukiza wawekezaji wahuni na waongo
 
Mkuu Uber hana Gari hata moja. Kifupi huna taarifa sahihi za hii biashara.
Asante maana yangu ni wale wanaojisajili kwa vigezo vyao ... Wao wana miundo mbinu taratibu na sheria walizoweka ili waweze kujisajili.. Mpunga unaingia kwao gari yako unalipwa kamisheni.. Nakubali unikosoe zaidi kwa nia ya kuelimishana
 
Madereva wameandamana kushinikiza kampuni mtandao ziongeze nauli, Uber inasemekana kagoma kuongeza wakati huo kuna baadhi zimetii.

Leo unapomnanga Uber, jiulize upo upande wa madereva au abiria?
Nipo upande wangu nadhani ila sina hakika
 
Madereva wanaolalamika malipo siyo wamiliki wa vyombo wanavyofanyia biashara...Uber imejijenga kwa wewe mmiliki wa gari ku share usafiri wako kwa muda wako na mhitaji wa usafiri kwa rate fulani, wabongo wameamua kuifanya kama kazi ya taxi, rate zilizokuwepo ikiwa gari ni yako na unaendesha mwenyewe unapata faida vizuri tuu, ila ukimuajiri dereva lazima apate machungu
 
Tumepigwa tena na kitu kizito kichwani watanganyika!

Uber ni bepari ... Bepari sifa yake ni uchoyo uliopitiliza(craving) anapenda mno kupokea lakini kutoa japo kidogo ni mchungu mno na anaumia mno..!

Sababu alizotoa Uber kufungasha virago baada ya MIAKA 6 ya kufanya biashara nchini naweza kusema ni nyepesi na za kijinga mno... Kapiga ndefu ndani ya miaka mitano ya bila kodi kama sheria inavyosema kwa wawekezaji wakubwa.. Huu ni mwaka wa sita anatakiwa sasa aoneshe hesabu zake kwa ujumla kama alipata faida ili aanze kulipa kodi stahiki sasa.. ANAKIMBIA

Tumeliwa kwa miaka mitano mtu kaja na mkoba anaondoka na utajiri mkubwa.. Uber hayuko peke yake katumia udhaifu wa sheria ya kuvutia uwekezaji na wawekezaji kama wengine walivyofanya kwenye
Makampuni ya madini
Kwenye mahoteli makubwa nchini
Kwenye viwanda mbalimbali vya wageni
Kwenye uwekezaji wa kina aina..!

Tumeshuhudia kwa uchungu mno tangu enzi za Mkapa watu waki DECLARE LOSS baada ya miaka mitano ya uwekezaji lakini hapo hapo walichokisema hakina faida wakawauzia 'wenzao' (kumbe ni wenyewe) kisha nao wakapata msamaha wa miaka mitano.. Ndio maana kila baada ya miaka mitano makampuni yanabadili majina biashara inaanza upya..! Tunaliwa mpaka sehemu za aibu wallah

Na haya yote yanafanyika kwa msaada wa wazawa wenyewe..watu wetu waliokosa uzalendo na uaminifu ... Lakini kama mamlaka zinaiba kura ili zibaki madarakani wao ni nani wasile kwa urefu wa kamba zao?? Tanganyika yangu iko mnadani

Uber sio pekee anayefanya biashara ya usafiri nchini.. Matatizo kwenye mamlaka ni kweli yapo mengi tu lakini hayajafikia kiwango cha sababu walizotoa uber
Wana gari almost mpya
Gari zao ni za cc ndogo sana
Gari zao karibia zote zimefungwa mfumo wa gesi
Wanawabana mno madereva
Kodi wanazolipa si halisi wanachakachua mno.. Leo wanasema wameshindwa phyuuu... Mtuhurumie jamanim..!

Na ukijua bado wanatatutamani wamesema kanuni zikirekebishwa watarejea .. ni wahuni sana hawa jamaa.. Wanajua wazi baada ya bunge la bajeti kupita kuna sheria na kanuni mbalimbali zitafanyiwa marekebisho.. Hapo ndipo wanaposubiri wapate kisingizio cha kurejea na kupata miaka mingjne mitano kama sheria ya kuvutia uwekezaji inavyotaka

Wangeweza kubadili jina kidogo tu wasingeondoka.. Lakini inaelekea huko jikoni magazijuto yaligoma maana jina lao ni brand world wide!.. Sasa hesabu zote zinafungwa waliopiga wamepiga kila mtu kwa urefu wa kamba yake!

Ninayemuonea huruma ni mtanganyika kwa hali zote kuanzia huduma muhimu za jamii mpaka future yake kama mwananchi.. Mimi wewe yule na sisi sote tunaoendelea kupigwa na vitu vizito kwa ghiliba za watawala na mapebari kupitia chama chawala...
Tatizo mmelileta wenyewe na uswahili wenu, kila Ramadhani ikifika mnatangaza hasara mnatoa talaka mnaoa mke mpya! Wazungu wamewaiga imekuwa shida.
 
UJANJA HUO HUO WA KUKWEPA KODI BAADA YA MIAKA MITANO ulitumiwa na HOME SHOPPING CENTRE WALIPOBADILI JINA KUWA GSM?
 
Back
Top Bottom