Ubelgiji yampeleka Ufaransa mshukiwa wa Paris Abdeslam

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
160318202547_sp_bruselas_abdeslam_640x360_ap_nocredit.jpg

Abdeslam akikamatwa na maafisa wa polisi wakati wa operesheni kali iliofanyika mjini Brussels
Ubelgiji imempeleka mshukiwa wa shambulio la Paris Salah Abdesalam nchini Ufaransa.

Alijeruhiwa na kukamatwa katika operesheni iliofanywa na maafisa wa polisi mjini Brussels baada ya kutoroka kwa miezi minne.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 alizaliwa mjini Brussels na aliishi mjini humo kabla ya shambulio la Paris.

Takriban watu 130 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya kupangwa yaliotekelezwa na kundi la Islamic State mjini Paris mnamo tarehe 13 mwezi Novemba.

Chanzo: Swahili
 
Huyo jamaa kweli boya. Aliweza vipi kushawishi wenzake kujitoa mhanga halafu yeye akaruhusu kukamatwa kibwege namna ile!? Au naye muoga Wa kifo!? Wacha wakamfunge chumba cha peke yake miaka mia.
 
wamfunge mabomu yao yale ya kujitoa mhanga, halafu awekwe sehemu ya wazi tuone show jinsi anavyopasuka vipande
 
Back
Top Bottom