Ubeberu na Upinzani wa Mazingaombwe

Dec 16, 2017
12
14
Hivi yale makubaliano ya mabeberu na vibaraka wake chini ya mwamvuli wa vyama vya upinzani yaliishia wapi? Naulizia makubaliano yaliyobatizwa kwa jina la Azimio la Zanzibar. Ndio, mtakumbuka tulivyoelekea kumaliza wa mwaka 2018 vyama vinavyopinga kila kitu vilikutana Zanzibar na kutoa tamko lenye kaulimbiu ya ‘Kurudisha Demokrasia’ wanayodai imeminywa kwa miaka mitatu sasa

Lengo si kutaka kueleza makubaliano yaliyofikiwa na vyama hivyo au kuchambua kile ambacho kilielezwa, La hasha..! Lengo ni kutaka kujua yaliishia wapi? Au ulikua usanii? Tuliaminishwa mwaka 2019 utakua mwaka wa mshikemshike kudai domokrasia, Ni kweli, nasema DOMOKRASIA..!

Kwa sababu DEMOKRASIA ya kweli katika nchi yetu ipo na hatuwezi kudai kitu kilichopo. Labda DOMOKRASIA iliyozoeleka ya vyama vya upinzani hasa kile kikundi cha ujasiriamali kutoka Kanda ya Kaskazini kinachoaminisha watu kuwa nacho ni Chama cha Siasa.

Nilidhani mwaka 2019 utaanza na kivumbi cha mikutano ya hadhara. Ndio, nilidhani hivyo kwa sababu mara baada ya Azimio hilo, vyama hivyo vilikuja na ratiba ya mikutano ya hadhara. Mpaka sasa tumeshikwa na butwaa, hatuoni hiyo mikutano!!!

Hivi yule kiongozi wa chama kutoka Kigoma ambaye ndio PAYMASTER GENERAL wa MIAMALA YA MABEBERU kutoka ughaibuni mpaka sasa kafanya mikutano mingapi ya hadhara? Nilidhani angekuwa wa kwanza kufanya mikutano hiyo kutokana na namna alivyowaongoza vipofu wenzake. Nasema vipofu si kwa sababu ya macho yao kutokuona, La hasha!

Hawa ni vipofu wa mazingaombwe tu, wanaona mambo makubwa yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano na kujifanya hawaoni. Mabeberu wamekamata fikra zao, wamezibinya, wamezibana, hawajitambui. Wengine tunawaona huko ughaibuni wakijizatiti kuwaonyesha Mabeberu hao kuwa muamala uliotolewa unatumika na kazi waliyotumwa wanaitekeleza.

Wanaichafua nchi yao kwa namna wanavyoweza huku wakishangiliwa kwa vifijo na nderemo na vibaraka wenzao walioko Tanzania. Wanamsifia mtu ambaye bado anasumbuliwa na dawa za usingizi…! Mtu ambae amewahakikishiwa kuwa madaktari wake bado hawajamruhusu kurudi Tanzania, Madaktari wanajua kabisa bado hajapona. Maana yake ni kuwa hata anachoongea anaongea akiwa mgonjwa, hajitambui.

Ni mtu ambae akili zake zimeshikiliwa na dawa za usingizi (Yupo unsound mind). Lakini Watanzania wachache wanashangilia maneno ambayo ni zao la madhara ya dawa za usingizi

Watanzania sio wajinga. Wanajua Serikali yao inafanya mambo makubwa kwa maslahi yao. Hii ni serikali ya watu, ni serikali ya wananchi. Watanzania wanajua kuwa ndugu John Pombe Magufuli ni mzalendo wa kweli, anapigana vita ya kiuchumi. Na sisi tupo pamoja nae. Hakika Tutashinda

#UbeberuNiUnyama
 
Hii mada yako umeiandika kishabiki na imejaa vijembe kiasi kwamba ni vigumu sana kuwavutia wachangiaji ambao hawaegemei upande wowote. Zaidi ya hapa, tutegemee tu kutukanana na kutoleana tu kejeli.
 
Serikali ya watu!
Wauza vitumbuwa kodi 20,000
Hakuna kufanya siasa
Korosho ziiii
Pamba ziii
Tumbaku ziii
Kahawa ziii
Gas ziii
Watu kupigwa
Watu kupotezwa
Watu kupigwa risasi
Bunge live kufungiwa

Labda serikali tuite ya manyanyaso kwa watu wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom