Ubaya wangu ni nini?

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Hamjambo wana JF . Naomba ushauri wenu katika hili suala.

Mimi nimeishi na mdogo wangu wa kike mtoto wa mama mdogo. Baada ya kumaliza Form IV alikuja Dar kwanngu na kuanza shule ya mambo ya Hoteli. Na gharama za shule nililipa mimi. Baada ya kumaliza masomo ya hotel aliungana na mwenzie katika biashara ya mambo ya stationery na wakapangisha nyumba ambayo ilikuwa ni ofisi na kuna sehemu ya kuishi, hivyo alihama kwangu na kuniomba mtaji wa laki tatu kuongezea \manunuzi ya ptocopy machine.

Katika kufupisha hii story, wamepanga sehemu mbalimbali, baadaye walikorofishana na mwenye nyumba kwani aliahidi kuwawekea umeme lakini ikawa story. sasa nikawambia nina nyumba mahali wanaweza kupanga na kunilipa kodi. Baada ya kukaa muda wakaanza kutolipa na huyo mwenzie.

Nilichukua hatua ya kuwauliza matokeo yake akawa ananijibu vibaya. Hivyo nikaamua kuwafukuza kwenye nyumba yangu.

Sasa imekuwa ugomvi mkubwa mpaka mama mdogo (mama yake ) hanisemeshi , na yeye ndio kabisa?

Naqomba ushauri wenu hapa nifanyeje? Nami niuchune au niendelee kuwabembeleza?
 
Pole sana kwa kumpangisha ndugu kwenye nyumba, ni ndugu wachache sana waaaminifu kukulipa kodi yako. Ukimwambia ukweli utaonekana mbaya kama hivyo sasa wanakuchunia.

Na wewe wachunie bana kwani ndio wanakupa kula yako hadi uwabembeleze? Kama unaona muhimu sana kuwa na mahusiano nao nenda ukaawambie wazazi wako/wazee wenu wawakalishe kikao ili mpatanishwe.
 
Biashara na undugu wapi na wapi????????? Tanzania Bwana!
 
...malenga walisema "tenda wema nenda zako!",
uchune tu, ipo siku ukweli utadhihiri...
 
...malenga walisema "tenda wema nenda zako!",
uchune tu, ipo siku ukweli utadhihiri...

Wao kama ndo wamekuchunia we wasubiri tu watakuja wenyewe kukuomba msamaha,kazi yako ya msingi uliishaimaliza wema tayari umeisha watendea...
 
pole sana ndugu!!
tafuta wazee wawapatanishe kwani hapo tayari kuna bifu!!
 
Kama mlikubaliana toka awali kwamba watalipa, the wasikutishe na wala usione shida kununiwa.Si unaona shida ya ndugu, pamoja na kumsomesha kote hiyo elimu ya Hotel bado akatemana nayo, na mbaya anakuja kukudharau kwa ishu ya nyumba!We achana nao bana, watazunguka wee, lakini giza litapoanza watarudi nyumbani?
 
Sikiliza "Ten crack commandments" kuna moja inasema never keep family and business mixed. Kama unayosema ni sawa wewe tenda wema uende zako, usingoje shukurani wala kubabaishwa na lawama za kijinga.
 
Yani achana nao kabisa wala wasishughulishe akili yako, ndo maana africa hatuendelei sababu ya huu ujinga. be real and ishi maisha yako, ulifanya nafasi yako na inatosha.
 
Kibaya zaidi wanaombea nifulie tu wanione nitakavyoadhirika.
 
Ni ndugu wachache sana unaoweza kufanya nao biashara msiishie pabaya.
Pole kwa yaliyokukuta ila ndio TMKwanaume family walisema ubinadamu kazi.
Kuchuniwa isikusumbue hata kidogo keep in ur mind kuwa huwezi kumfurahisha kila mtu.
Tulia kimya kama huelewi kinachoendelea ili uwape mda kuelewa wanachokifanya si vyema.
 
yaani siku zote usifanye business na ndugu yako mwisho ni kuishia ugomvi kama wako, huyo mama mdogo wako alitaka mwanae akae bure wakati wewe ume struggle kujenga
Tafuta ndugu wa karibu wenye hekima wasuruhishe hili swala lenu mpendwa
 
Kibaya zaidi wanaombea nifulie tu wanione nitakavyoadhirika.

kama sir god ameweka tiki ..hao nduguzo waache tu wakuombee mabaya hayatakupata ila binadamu habebeki hata umuweke kwenye mbeleko ya chuma
 
wajinga sana hao ndugu,

they cannot think beyond the next meal!

kaa utulie ufanye mambo yako ya maendeleo kaka,
wala wasikutishe, mama mdogo nae ni tatizo.
 
Kukaa na ndugu ni shida sana , acha kuwapangisha kama una moyo mdogo unaweza kumfukuza hata usiku wa manane akuone mbaya, muache akuchunie kwani nini?umemsomesha inatosha kabisa.
 
Biashara na undugu wapi na wapi????????? Tanzania Bwana!

Kweli kabisa mkuu biashara na ndugu wapi na wapi? we kama unataka kuutesa moyo wako fanya biashara na ndugu kila siku utaishia kwenye kulalamika na kuisononesha roho yako bure,tangu lini ndugu wakawa na shukrani? Hata umtendee mazuri elfu siku iko siku tu atakuona mbaya.Umemsomesha amepata kazi sasa hivi anakuona wa nini,nawe mwone wa kazi gani.

Achana nae we songa mbele.
 
mimi nasema hivi wala usibabaike, maana wao sio waliochangai kwenye maendeleo, mbona ulipomsomesha hawakuwa wananuna, yeye si tayari umempa elimu sasa kwa nini asijitegemee, je kama ingekua nyumba ya mtu asiyemjua asingelipa kodi kweli. kama vp wewe wapotezee tu maana sio waliokuweka mjini, hawakulishi, wewe muombe mungu aendelee kukupa pumzi ya uzima na sio binadamu mwenzio anayekuombea mabaya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom