Ubavu uliopotea

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
(verse 1)

Ubavu wangu wa kushoto umeniachia kidonda
Napitia msoto na mwili wote nimekonda
Sina tena furaha zaidi ya stress nahuzuni
Sina raha kama nimelala juu ya kitanda cha kunguni

Ni kweli hali duni ndio yalikuwa maisha
Ni wazi majaribuni ndio mrembo ulipita
Hizi sumuni hazikukidhi haja zako
Pesa za saluni na codes za kuchora tako

Haikuwa bahati yangu kuwa nawe
Nikimiliki manati huku mikononi sina mawe
Umenifanya nipagawe kama chizi
Silali nikikesha kama mlinzi sa hizi

Nadata nikikumbuka your face look
Sina pa kukupata zaidi ya kukucheki mafacebook
kucheki picha zako sema sina data ni stress tupu
Rudi tena baby kweli nahitaji your rescue
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom