Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Securelens

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
316
541
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha habari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo.

Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge.

Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii

Zaidi soma:

Wazungu tunawategemea ila kutwa kuwasimanga kwa kuwaita mabeberu! Kuweni na shukurani na sio kuleta kejeli na dharau huku watu wenyewe sisi ni tegemezi.

Kwa jinsi tunavyowakejeli, wazungu hawa wangekuwa na mavichwa kama yetu, hata hiyo misaada na mikopo wangeshaisitisha, ila wamegundua baadhi ya watu wetu ni wajinga na wameamua kuwapuuza ili kusaidia masikini wa hii nchi wasio na hatia.

Isitoshe kwa hapa JF, uzi uliopo unaongelea kamati na si Bunge zima.

Alafu elezeni pia mlikopeleka hela za Covid.

Sisi tunasubiri taarifa rasimi ya hilo Bunge ila mpaka sasa teyari ni aibu tosha kwani hatukwahi kuwa na status mbovu na mbaya kiasi hiki.

Awamu hii ni shida tupu!

No wonder hata JK aliwahi sema watu waache "kujimwambafai."
 
MARA YA MWISHO UBALOZI WA BELGIUM KUPOST TWITTER NI TAREHE 16 OFFICIAL ISSUES ZOTE LAZIMA WAPOST TWITTER
PILI BUNGE LA ULAYA WABUNGE 705 SIYO 71

TATU UBALOZI WA UBELGIJI HAUWEZI KUTOA TAARIFA KUHUSU EU PARLIAMENT HATA KAMA MAKAO MAKUU YAPO BRUSSELS KUNA

OFISI YA EU HAPA TANZANIA WAO NDIYO WANATAKIWA KUTOA TAARIFA KWANZA KILICHOPO WAO(WAKO KIKAANGONI WAELEZE ILKUWAJE WAKATOA HIZO BILIONI 63
 
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha vhabari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo. Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge. Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi ni walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii
Ni jambo jema kwamba sasa serikali yasikiliza maoni chanya juu ya kujibu tuhuma na taarifa zisizo na ukweli zitolewazo mitandaoni.

Pia, kwa faida ya wengi khasa majukwaa ya kimataifa, ni budi pia kutumia lugha ya kiingereza ili kuwekana sawa pande zote za dunia.
 
Umoja wa mabeberu haujafuta misaada?😂
 
Ni jambo jema kwamba sasa serikali yasikiliza maoni chanya juu ya kujibu tuhuma na taarifa zisizo na ukweli zitolewazo mitandaoni.

Pia, kwa faida ya wengi khasa majukwaa ya kimataifa, ni budi pia kutumia lugha ya kiingereza ili kuwekana sawa pande zote za dunia.
Huyo balozi wa Ubelgiji siyo mzalendo hata kidogo. Kwanini anaendelea kulilia pesa za mabeberu? Mnadanganya wananchi eti wanalazimishiwa ushoga na mabeberu.

Halafu anasema “hatupokei msaada kila mwaka”, na hapo hapo anasema “msaada haujasitishwa”
 
https://twitter.com/BelgiumTanzania
MARA YA MWISHO UBALOZI WA BELGIUM KUPOST TWITTER NI TAREHE 16 OFFICIAL ISSUES ZOTE LAZIMA WAPOST TWITTER
PILI BUNGE LA ULAYA WABUNGE 705 SIYO 71

TATU UBALOZI WA UBELGIJI HAUWEZI KUTOA TAARIFA KUHUSU EU PARLIAMENT HATA KAMA MAKAO MAKUU YAPO BRUSSELS KUNA

https://twitter.com/EUinTZ

OFISI YA EU HAPA TANZANIA WAO NDIYO WANATAKIWA KUTOA TAARIFA KWANZA KILICHOPO WAO(WAKO KIKAANGONI WAELEZE ILKUWAJE WAKATOA HIZO BILIONI 63
Naona wajichanganya sana.

Kama shida ni kubwa sana basi muombe taarifa rasmi kutoka ubalozi wa EU Tanzania.

Wao watatoa ufafanuzi wa kutosha na wenye tija.
 
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha vhabari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo. Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge. Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi ni walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii
Kuna tofauti kubwa sana kati ya vikao vya kamati ya Bunge na kikao cha Bunge la EU.

Ubalozi wa EU upo pale Umoja House tafuteni ukweli.
Nimemsikiliza. Ni kilaza. Yuko kisiasa zaidi. Nafasi aliyopo hana uwezo nayo.
 
Mabeberu mnawategemea ila kutwa kuwasimanga!Kuweni na shukurani na sio kulate kejeli na dharau huku watu wenyewe ni tegemezi.

Uzi ulioko hapa JF unaongelea kamati na si Bunge zima.

Elezeni pia mlikopeleka hela za Covid.

Sisi tunasubiri taarifa rasimi ya hilo Bunge ila mpaka sasa teyari ni aibu tosha kwani hatukwahi kuwa na status mbovu na mbaya kiasi hiki.

Awamu hii ni aibu tupu!
Huyo balozi ni muongo, na Pia ni kilaza! Eti anathubutu kubeza maoni ya wabunge 5?! Tena wa kamati ya mambo ya nje? Eti kuwa siyo bunge lote, hajui kuwa bunge lote husikiliza hizo kamati? Ama anadhani ni bunge la Ndugai?
 
Back
Top Bottom