Ubalozi wa Tanzania wamzungumzia mtu aliyeweka picha ya maiti mtandaoni

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,433
7,055
Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza umesema hauna taarifa zozote za mtu anayedaiwa kuwa Mtanzania, Omega Mwaikambo ambaye alifungwa miezi 3 jela kwa kosa la kuweka picha ya maiti mtandaoni.

Habari hizo zilisambaa kwa kasi na kumtaja mtu huyo kuwa ni raia wa Tanzania.

Mtz.jpg
 
Sheria hazichagui dini, kabila wala Utaifa..... Ni vyema akaitumikia adhabu kwanza.

Maswala ya utaifa ktk uhalifu hayana umuhimu
 
Watanzania hasa upinzani ndo wa shamba yaa wanaona kuweka mapichapicha kwenye mtandao ndo democrasia hiyo
 
jela za wenzetu full bata yaan miezi mitatu pia hatafaidi vizuri,, jela ulaya ni sawa na kuwa huru Africa
 
Sasa Hapa kwetu ambao tumerithi sheria mbali mbali toka kwa waingereza yaani common laws tupo kimya, Utafikiri hakuna sheria, watu wana post picha za ajali zikionyesha marehemu katika ajali, sheria za mitandao zipo kazi kukamata wanaomkosoa Magu tu, nchi ya laana kabisa hii.
 
Sasa huyu mnyakyusa aliendaga kufanya nini huko?

Angejikalia tu hapa kyela anajilimia viazi na mahindi na kumsadia bibi take kutwanga mpunga

Ona sasa yanayomkuta kwenye nchi ya hao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom