Ubalozi wa Tanzania US ni vituko tupu

balozi zetu zote ni vituko, tofauti kabisa na balozi za wenzetu. unajua kwamfano mmarekani akija hapa tz akaamua kutembelea ubalozi wake, treatment anayopewa ni nzuri ila mbongo ukiwa nje ukatembelea ubalozi wetu wowote ule, cha kwanza wanakuona kama umeenda pale kuomba msaada labda maisha yamekupiga, wanaanza kujidistance awali kabisa wakikuona. niliwahi kutembelea ubalozi mmoja hivi tena nikiwa mwanafunzi,nina hela yangu na sikwenda pale kuomba hela ila kuongewa tu mhuri kwenye nyaraka fulani ambayo ilitakiwa nirudi nigongewe bongo, nikasema niende tu ubalozini hapa wanigongee...nilihisi kama mtu akipata tatizo bora ukimbilie ubalozi wa mzungu kuliko ubalozi wao. hawa madiplomat wetu wanatakiwa wafundishwe kabla hawajaenda huko wajue wameenda huko kwa kodi zetu na ndizo zinazowalipa mishahara. over.
Tanzania hakina diplomat ni wapumbavu fulani wanaojinafikisha kwa Utawala ndio hupewa hivyo vyeo kama Chaka lao wakale maisha au wengine hupewa kama adhabu wapotee nchini wanapelekwa nchi za hovyo kama Togo huko unakaa hauna kazi hakuna hata mtanzania mmoja.

We jiulize yule alikuwa miss anapewa ubalozi anajua nini kuhisi diplomasia???? Mabalozi walikuwa zamani akina mzee Lusinde nk.
 
Siri usio ijua mabalizi wakipangiwa kwenda sehemu mara nyingi wanaajiri watoto waonau ndugu zao ambao hawana knowld6 hata kidogo ya wanachofanya.

Kuhusu watu wa kuja kwenye gala usishangae ndio mfumo wa huu utawala hata kwenye musafara ya chief wamo watu ambao wako humu sio watumishi wa serikali lakini wamewekwa kama wafanya biashara huku hata biashara qanazofanha hazieleweki

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Huu unaweza kuwa ukweli mtupu
 
Hakuna kitu mtanzania anaweza fanya kwA ufasaha iwe huo ubalozi, ubalozi wa nyumba kumi, udaktari, ualimu, uongozi, kulima, viwanda, yaani hakuna kitu mtanzania anajua.

Huko wamekaa tu hata ukiwauliza kazi zao ushishangae pia hawajui wanafanya nini
 
Mambo hayo yanaanzia Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuia ya Afrika Mashariki Dar na Dodoma. Kumejaa watoto na jamaa za viongozi wa zamani na sasa wa serikali, majeshi na Chama cha Mapinduzi ambao wengi sifa zao kuu ni wazazi kuwa kwenye system. Ukitembelea hizo ofisi ukitaka huduma ni kama una beg! Foreign Affairs office ndio kioo cha nchi kama ilivyo ubalozini. Msituangushe amkeni au mtumbuliwe na kusafishwa kama Wizara ya Nishati, japo mafanikio bado tunayasubiri.
 
Yaani maafisa wa ubalozini kwa balozi za Tanzania, ni Zero brain. Wako so local yaani hata hawafai kuitwa Diplomats. Wanafanya mambo kama ofisi za mtendaji wa kijiji.
Nilishawahi kukataliwa kuingia ubalozini kisa wanakikao. Yaani ilibidi nitumie nguvu, na kuuliza ni sheria ipi inayozuia nisiingie ubalozini kisa wanakikao? Kama natishiwa usalama wangu nikaona nikimbilie ubalozini, na wao hawataki niingie si ndiyo unauwawa hapo hapo nje ya ubalozi. Sasa huduma niliyoifuata hata sikupewa kwanza hawajui hata utendaji wa serikali katika nyanja za idara kadhaa nchini. Ilikuwa ni vituko. Si huo ubalozi mmoja ni balozi nyingi kadhaa. Ubalozi fulani dada mmoja namuhifadhi huyu analugha za ajabu kwenye simu, na anaongea kwanyodo, unauliza jambo ati hajui, sasa unashangaa hivi hawa watu hawana uzoefu wa kiserikali? Wanapopelekwa huko nje, je nini kinazingatiwa?

Kwasasa napokuwa nje nimeamua kujiona sina balozi, wala sihitaji kuwaona, nachofanya ni kupiga simu moja kwa moja Tanzania katika wizara husika au Idara ambayo nahitaji huduma. Kuliko hawa madiplomats wa kuzuga.
 
Tatizo jumuiya zenyewe za watanzania ni ovyo. Wakiambiwa wapeleke orodha unakuta wana chama hai awazidi 10. Na kama wapo wengi mara nyingi kuna mgogoro wa uongozi.

Ubalozi ukiongea na uongozi mmoja, anatokea mwingine kusema awamtambui huyo bwana/bibi kama kiongozi wao.

Sasa hapo kuna issue ya kujipendekeza kuna watanzania ughaibuni wana penda kujikuza na ukikutana na balozi waovyo mfano Kalaghe au wale wanaopenda mialiko ya misosi wanajiingiza kwenye migogoro ya diaspora isiyowahusu na kuchukua upande.

Lakini mabalozi wapya overtime washajifunza kutoingilia migogoro ya diaspora provided kundi linajielewa wao wanashirikiana nao; na as far as they are concerned kila mtanzania ana haki sawa mbele yao uwe diaspora mbeba boksi au Phd na lecturer at top university kwao wote sawa.

Watu wakijapanga na kuwa na uongozi mzuri awana shida, kasheshe sasa kuna sakapoko wanajionaga wao bora kushinda wengine upuuzi huo ndio ubalozi autaki tena.

PS maswala ya passport ni uhamiaji Tanzania. Ubalozi wao awahusiki na lolote siku hizi zaidi ya kufacilitate tu, ukipangiwa siku ya finger print ubalozini ukaenda system ikiwa down sio wao ni Tanzania na awawezi fungua ofisi kila mji sababu awana hiyo budget na watu; ila kuna mapendekezo ya diaspora kufungua ofisi zao wenyewe na kuziendesha ubalozi utashirikiana nao kwa namna moja au nyingine kutatua changamoto zao.

Haya maswala mama Migiro kayatolea ufafanuzi kwa kina UK kuna watu ni vichwa maji tu katika diaspora wao kila siku wanatakupeleka upuuzi wa jumuiya zao ubalozini mambo ambayo siku hizi awataki tena.

Ukiona kiongozi mkubwa anakuja kuna diaspora viherehere wanagawa tshirt na kusafiri elewa siku hizi balozi ahusiki huyo anatumwa na kavuta mpunga kwa kupitia either watu wa usalama, serikalini au CCM (wahusika nyuma ya pazia wanaishi nchi hizo hizo na awapo ubalozini) lakini ubalozi auna raia bora kushinda mwingine.
 
Tatizo wamejaa mahawala, chawa na ndugu wa wazee wa nchi, usitegemee chochote zaidi ya frustrations tuu
 
Msitutie aibu kama dinner itakua hotelini lipa uende.
Kwani lazima?huna hela kausha tu we umepewa mwaliko baada ya kuloloma sana bado unaloloma tu.muwage na mipaka
 
Nashauri uwe mwazi zaidi kwenye jamiiforums hapa usiogope kutaja ubalozi gani ili tusaidie. Tukificha ficha hatusaidii nchi yetu
 
Msitutie aibu kama dinner itakua hotelini lipa uende.
Kwani lazima?huna hela kausha tu we umepewa mwaliko baada ya kuloloma sana bado unaloloma tu.muwage na mipaka

Hatujaalikwa mpaka sasa labda wabadilishe mawazo. Community yetu ya Dallas tuna uwezo hatuwezi kushidwa pesa ya kula. Tatizo ni kwamba hatujaalikwa mwenyekiti alipiga simu akaambiwa wanaruhusu watu wanne tu labda baada ya malalamiko ibadilike. Lakini tukiachana na hiyo gala watu wengi wanahitaji passport sio ma gala ! Balozi ije ifanye finger print.
 
Tunasikitika ubalozi wetu wa Tanzania US unejaa wafanyakazi wasiojua wanachofanya. Ili watu waelewe hili nimewapa barua mbili hapa. Barua yenye kumbukumbu namba moja imetumwa kwenye miji miwili tofauti. Ukipiga simu wanasema Dallas eti hawaendi. Cha kushangaza vilevile pamoja na viongozi wa Dallas kuwepo kwenye list ya viongozi wa jumuia walipata barua kwenye mitandao.

Pamoja na kusema kwenye simu sasa kwamba hawaji Dallas kwenye website ya ubalozi wanasema watakuja Dallas kwenye Gallas hotelini. Baada ya viongozi kuona kwenye mitandao wakafikiri watanzania na balozi anakuja kushererekea sikukuu wa uhuru wa miaka 60 na Watanzania. Cha ajabu baada ya viongozi kuhoji waliwaruhusu viongozi wanne tu kuwepo kwenye gala hii tarehe 3. Ingawa ubalozi huohuo sasa unasema hautaweza kuja tena kuwasaidia Watanzania kupata passport zao hapa Dallas,Texas. Cha kujiuliza ni nani anaenda kwenye gala? gharama ni za nani? kwanini sasa wanasema hawawezi kukutana na watanzania?. Hata kama ni wafanya bishara ni kwanini watanzania wasiambiwe wazi ili wahimize wafanyabiashara kuwepo kwenye huu mkutano na wameweka siri mpaka mwenyekiti wa jumuia apige simu. Cha ajabu kingine hawajui tofauti ya jimbo na mji!

View attachment 2027518

View attachment 2027519

Hii hapa watanzania wamepigwa stop hawaja alikwa kabisa! baada ya kelele nyingi wakaruhusu mwenyekiti na wengine wawili lakini eti ni sherehe za miaka 60!!

The Embassy of Tanzania in the USA would like to cordially invite you to the inaugural Tanzania-USA corporate GALA dinner in honor of the 60th Anniversary of independence for Tanzania mainland , as well as the 60th Anniversary of Diplomatic relations between Tanzania and the USA.

VENUE: OMNI DALLAS HOTEL , 555 S Lamar St. Dallas, Tx 75202

DATE: Friday, 3 December 2021.

For more Information please visit : Tanzania at 60 | Tanzania Imara, Kazi iendelee
Hao watu waliopo hapo ubalozini nahisi si Watanzania sababu hata historia rahisi tu ya Tanzania hawaijui.

Kwanza waelewe hakuna nchi iliyoitwa/inayoitwa Tanzania Bara(Tanzania Mainland).

Kwa kuwakumbusha hao watu waliopo hapo Ubalozini ni kwamba sherehe za miaka 60 ni kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika.
 
Tatizo jumuiya zenyewe za watanzania ni ovyo. Wakiambiwa wapeleke orodha unakuta wana chama hai awazidi 10. Na kama wapo wengi mara nyingi kuna mgogoro wa uongozi.

Ubalozi ukiongea na uongozi mmoja, anatokea mwingine kusema awamtambui huyo bwana/bibi kama kiongozi wao.

Sasa hapo kuna issue ya kujipendekeza kuna watanzania ughaibuni wana penda kujikuza na ukikutana na balozi waovyo mfano Kalaghe au wale wanaopenda mialiko ya misosi wanajiingiza kwenye migogoro ya diaspora isiyowahusu na kuchukua upande.

Lakini mabalozi wapya overtime washajifunza kutoingilia migogoro ya diaspora provided kundi linajielewa wao wanashirikiana nao; na as far as they are concerned kila mtanzania ana haki sawa mbele yao uwe diaspora mbeba boksi au Phd na lecturer at top university kwao wote sawa.

Watu wakijapanga na kuwa na uongozi mzuri awana shida, kasheshe sasa kuna sakapoko wanajionaga wao bora kushinda wengine upuuzi huo ndio ubalozi autaki tena.

PS maswala ya passport ni uhamiaji Tanzania. Ubalozi wao awahusiki na lolote siku hizi zaidi ya kufacilitate tu, ukipangiwa siku ya finger print ubalozini ukaenda system ikiwa down sio wao ni Tanzania na awawezi fungua ofisi kila mji sababu awana hiyo budget na watu; ila kuna mapendekezo ya diaspora kufungua ofisi zao wenyewe na kuziendesha ubalozi utashirikiana nao kwa namna moja au nyingine kutatua changamoto zao.

Haya maswala mama Migiro kayatolea ufafanuzi kwa kina UK kuna watu ni vichwa maji tu katika diaspora wao kila siku wanatakupeleka upuuzi wa jumuiya zao ubalozini mambo ambayo siku hizi awataki tena.

Ukiona kiongozi mkubwa anakuja kuna diaspora viherehere wanagawa tshirt na kusafiri elewa siku hizi balozi ahusiki huyo anatumwa na kavuta mpunga kwa kupitia either watu wa usalama, serikalini au CCM (wahusika nyuma ya pazia wanaishi nchi hizo hizo na awapo ubalozini) lakini ubalozi auna raia bora kushinda mwingine.

Hizi ni fikra zako ukweli ni kwamba jumuia ya dallas imejitambulisha toka 2009. Imesajiliwa rasmi, viongozi wametoa mawasiliano yao balozini. Isitoshe wametuma list ya watu zaidi ya 120 wanataka passport tena wiki jana tu. Wamefanya kila kitu hivyo hakuna kisingizio. USA kuna jumuia za Watanzania nyingi sana ni nchi kubwa hivyo ukitoa mifano toa mifano kamili na uwe na facts.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom