Ubalozi wa Tanzania US ni vituko tupu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,542
8,630
Tunasikitika ubalozi wetu wa Tanzania US unejaa wafanyakazi wasiojua wanachofanya. Ili watu waelewe hili nimewapa barua mbili hapa. Barua yenye kumbukumbu namba moja imetumwa kwenye miji miwili tofauti. Ukipiga simu wanasema Dallas eti hawaendi. Cha kushangaza vilevile pamoja na viongozi wa Dallas kuwepo kwenye list ya viongozi wa jumuia walipata barua kwenye mitandao.

Pamoja na kusema kwenye simu sasa kwamba hawaji Dallas kwenye website ya ubalozi wanasema watakuja Dallas kwenye Gallas hotelini. Baada ya viongozi kuona kwenye mitandao wakafikiri watanzania na balozi anakuja kushererekea sikukuu wa uhuru wa miaka 60 na Watanzania.

Cha ajabu baada ya viongozi kuhoji waliwaruhusu viongozi wanne tu kuwepo kwenye gala hii tarehe 3. Ingawa ubalozi huohuo sasa unasema hautaweza kuja tena kuwasaidia Watanzania kupata passport zao hapa Dallas,Texas. Cha kujiuliza ni nani anaenda kwenye gala? gharama ni za nani? kwanini sasa wanasema hawawezi kukutana na watanzania?

Hata kama ni wafanya bishara ni kwanini watanzania wasiambiwe wazi ili wahimize wafanyabiashara kuwepo kwenye huu mkutano na wameweka siri mpaka mwenyekiti wa jumuia apige simu. Cha ajabu kingine hawajui tofauti ya jimbo na mji!


31930986-d630-4a7e-935e-6f035c4e11b3.jpg


unnamed.jpg




Hii hapa watanzania wamepigwa stop hawaja alikwa kabisa! baada ya kelele nyingi wakaruhusu mwenyekiti na wengine wawili lakini eti ni sherehe za miaka 60!!

The Embassy of Tanzania in the USA would like to cordially invite you to the inaugural Tanzania-USA corporate GALA dinner in honor of the 60th Anniversary of independence for Tanzania mainland , as well as the 60th Anniversary of Diplomatic relations between Tanzania and the USA.

VENUE: OMNI DALLAS HOTEL , 555 S Lamar St. Dallas, Tx 75202

DATE: Friday, 3 December 2021.

For more Information please visit : Tanzania at 60 | Tanzania Imara, Kazi iendelee
 
balozi zetu zote ni vituko, tofauti kabisa na balozi za wenzetu. unajua kwamfano mmarekani akija hapa tz akaamua kutembelea ubalozi wake, treatment anayopewa ni nzuri ila mbongo ukiwa nje ukatembelea ubalozi wetu wowote ule, cha kwanza wanakuona kama umeenda pale kuomba msaada labda maisha yamekupiga, wanaanza kujidistance awali kabisa wakikuona.

niliwahi kutembelea ubalozi mmoja hivi tena nikiwa mwanafunzi,nina hela yangu na sikwenda pale kuomba hela ila kuongewa tu mhuri kwenye nyaraka fulani ambayo ilitakiwa nirudi nigongewe bongo, nikasema niende tu ubalozini hapa wanigongee...nilihisi kama mtu akipata tatizo bora ukimbilie ubalozi wa mzungu kuliko ubalozi wao.

hawa madiplomat wetu wanatakiwa wafundishwe kabla hawajaenda huko wajue wameenda huko kwa kodi zetu na ndizo zinazowalipa mishahara. over.
 
balozi zetu zote ni vituko, tofauti kabisa na balozi za wenzetu. unajua kwamfano mmarekani akija hapa tz akaamua kutembelea ubalozi wake, treatment anayopewa ni nzur...
Nakubaliana na wewe yaani wanakuja Dallas kwenye mkutano Gala bila hata kujulisha uongozi wa jumuia!. Yaani wawekezaji wataongea na Wanzania kujua nchi yetu huwezi kufanya vitu bila kuhusisha jumuia ya watanzania. Lakini kitendo cha balozi kuja mji bila hata kusalimia wananchi ni dharau ambayo sio nzuri kwa watanzania.
 
Nakubaliana na wewe yaani wanakuja Dallas kwenye mkutano Gala bila hata kujulisha uongozi wa jumuia!. Yaani wawekezaji wataongea na Wanzania kujua nchi yetu huwezi kufanya vitu bila kuhusisha jumuia ya watanzania. Lakini kitendo cha balozi kuja mji bila hata kusalimia wananchi ni dharau ambayo sio nzuri kwa watanzania.
Kwani kwasasa balozi wetu ninan uko?
 
balozi zetu zote ni vituko, tofauti kabisa na balozi za wenzetu. unajua kwamfano mmarekani akija hapa tz akaamua kutembelea ubalozi wake, treatment anayopewa ni nzuri ila mbongo ukiwa nje ukatembelea ubalozi wetu wowote ule, cha kwanza ...
Ulikosea ungeenda na kadi ya Chama.

Wapemba hujuana kwa vilemba
 
Nakubaliana na wewe yaani wanakuja Dallas kwenye mkutano Gala bila hata kujulisha uongozi wa jumuia!. Yaani wawekezaji wataongea na Wanzania kujua nchi yetu huwezi kufanya vitu bila kuhusisha jumuia ya watanzania. Lakini kitendo cha balozi kuja mji bila hata kusalimia wananchi ni dharau ambayo sio nzuri kwa watanzania.
Mmemripoti huyo balozi kwa Mulamula au mama kabisa ili amzingue??
 
Siyo USA tu. Ni dunia nzima. Sisi ambao tumeishi nchi mbalimbali ughaibuni tunalijua hilo. Wala huwa sina mpango nao. Nikiwa nje wala huwa sitaki kufahamiana nao. hawan msaada wowote. Wapo kwa ajili ya kujihudumia wenyewe na familia zao tu.
Duuuh kumbe?? Hii sasa ni hatari sana maana haina msaada...
 
Siri usio ijua mabalizi wakipangiwa kwenda sehemu mara nyingi wanaajiri watoto waonau ndugu zao ambao hawana knowld6 hata kidogo ya wanachofanya.

Kuhusu watu wa kuja kwenye gala usishangae ndio mfumo wa huu utawala hata kwenye musafara ya chief wamo watu ambao wako humu sio watumishi wa serikali lakini wamewekwa kama wafanya biashara huku hata biashara qanazofanha hazieleweki

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom