M
MegaPyne
Guest
na juma Pinto, london
JUMUIYA ya Wanzania waishio Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, imemualika Rais Jakaya Kikwete katika kongamano kubwa la kujadili maendeleo ya Tanzania litakalofanyika mwezi Aprili, mwakani.
Hayo yalisema na Balozi wa Tanzania nchi Uingereza, Mwanaidi Sinare Maajar katika sherehe ya sikukuu ya Uhuru wa Tanzania zilizofanyika Jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa Wembley.
Balozi Maajar ambae ametokea kwa kipenzi cha Watanzania waishio hapa, alisema kongamano hilo litakalosilikisha Watanzania wenyewe waishio Uingereza, wasomi wa vyuo,wafanyabishara na watu wengine maarufu waliokwishawahi kuishi au kufanyakazi Tanzania.
"Nataka kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa sisi Ubalozi kwa kushilikiana na Jumuiya ya Watanzania tumemualika Rais na amekubali kuja kushiliki katika kongamano letu, lengo lake ni kujadili mambo mbalimbali ya Tanzania,"alisema Ballozi Maajar.
Katika sherehe hizo iliyohudhuliwa na halaiki kubwa ya Watanzania, iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza, ikiwa ni shughuli yao ya kwanza kuifanya tangu uongozi mpya uchaguliwe mwaka jana.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Bw. Abubakar Faraji alisema hatua hiyo ni mwanzo wa uongozi wake kuangalia ni vitu gani ambavvyo vinaweza kufanyika lakini vikaisaidia serikali huko nyumbani kwa faida ya Watanzania wote.
"Kweli tuna mikakati mingi ambayo kama mambo yatakwenda kama tulivyopanga tunaweza kufanya mambo mengi na makubwa kwa faida ya Watanzania wa hapa Uingereza na huko nyumbani," alisema Faraji.
Alisema kongamano hilo litaweza kuwa mfano kwa jumuiya nyingine za Watanzania duniani kote na kuondoa dhana kazi kubwa ya jumuiya hizo ni kusaidiana kwenye misiba na kuandaa sherehe, bali na kuandaa makongamano makubwa kama haya ambayo yataweza kuisaidia nchi.
Katika sherehe hizo, mbali na Balozi Mwanaidi Maajar, wengine ni mbunge wa viti maalumu wa Singi, Mh Martha Mrata aliyekuwa kiongozi wa kuimbisha wimbi wa" happy birthday Tanzania", Naibu meya wa Wilaya ya Ilala, Mohammed Yakub,Mwenyekiti wa CCM London,Bw. Maina Owin, na muasisi wa tawi la CCM Uingereza, Bw. Sharrif Maajar.