Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda uwasiliane na utoe msaada wa haraka kwa Watanzania waliopo Rubavu eneo linaloathiliwa na volcano ya mlima Nyiragongo

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Wapo madereva na wafanyabiashara wanaohitaji msaada wakati huu pale mpakani mwa Rwanda na Kongo,Gisenyi almaarufu GRAND BARRIER.

Watumishi wengi Watanzania wahudumuo kwenye mission maalum ya Usalama upande wa Kivu kaskazini wanaweza kutumiwa kuwaokoa ndugu zao endapo team leader atawasiliana na mamlaka za UN na za kwetu kidiplomasia ili kuwaokoa ndugu zetu.

Ikumbukwe, Nchi za wenzetu mara yatokeapo majanga kama hayo huwa hawachelei kusaidia ndugu zao.

Mfano Nchi zote za magharibi tokea jana usiku raia wao wamewahifadhi maeneo salama juu ya Goma huku wakisubiri utaratibu maalum wa kuvushwa kwa helicopter upande wa Rwanda,Gisenyi na huko wataabiri ndege maalum zilizoandaliwa na watapelekwa Kinshasa hadi pale dhahama hiyo itapokoma.
 
Sijui hata kama balozi wetu wa DRC ametoka taarifa yoyote maana sijaona. Ila umetoa angalizo jema sana ni wakati muafaka balozi Mulamula kuwasiliana na balozi wa Tanzania nchini Congo kuangalia namna ya kutoa msaada wa watanzania waliokwama katika eneo like lenye athari kubwa ya volcanic action.

Rais huu ndio wakati wa kupimwa kwenye mambo kama haya sio kusubiri akina Dangote wake ikulu, Hawa watu uliowateua ndio wakuwakilishe vema otherwise fukuza mapema sana.
 
Back
Top Bottom