Ubalozi wa Tanzania na Oman Air wana mpango gani?

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,091
10,771
Nina ndugu yangu ambaye ameathirika na kukatikiwa safari nchini Oman kutokana na janga la Corona. Yeye ni mmoja tu wa watanzania wengi waliokwama nchini Oman kutokana na adha hii. Alikata tiketi ya kwenda na kurudi katika kuwatembelea familia. Baada ya muda wa viza kuisha na ndege ya shirika la ndege la Oman Air kukatisha safari, yeye pamoja na wenzake waliamua kwenda ubalozi wa Tanzania kutafuta msaada na wakatakiwa kujisajili. Majuzi akapokea ujumbe ufuatao kutoka ubalozi wa Tanzania :

Habari za leo, tunakutaarifu kuwa Shirika la Ndege la Oman Air litafanya safari kwenda Dar es Salaam Jumapili ijayo tarehe 7/6/2020 kwenda kuwachukua raia wa nchi nyingine kuwapeleka nchini kwao. Ubalozi umefanya mazungumzo na Oman Air liweze kuwachukua raia wa Tanzania waliokosa usafiri kutoka Oman. Kama utakuwa umejisajili Ubalozini kuomba kusafiri kwenda Dar es Salaam utapigiwa simu kuanzia leo tarehe 4/6/2020 uweze kukamilisha malipo ya ticket ambayo yatafanyika kwa kadi ya benki, hakikisha una maelezo ya kadi utayotumia, jina la mwenye kadi, namba 16 za kadi, mwezi na mwaka wa kuisha na security code nyuma ya kadi. Kuwa karibu na simu na kadi yako muda wote. Gharama ya Ticket ni Oman Rials 170. Msafiri atapaswa kununua ticket mpya kwa kuwa ndege hii ni ya dharura. Vilevile, Ubalozi unaendelea na maandalizi ya kupatikana ndege nyingine ambayo itaondoka kwenda Dar es Salaam na Zanzibar katikati ya mwezi June 2020.

1. Jambo la mwanzo linalonitia shaka ni hili agizo la kutakiwa kulipia kwa kadi na mlipaji ataje taarifa zote za kadi mpaka 3 number code zilizo nyuma ya kadi. Je hii haiwezi kutoa fursa ya wizi wa mtandao?

2. Kwanini abiria aliyekwisha kulipia tiketi ya kwenda na kurudi alipishwe tena thamani ya kurudi kwao kwa kiasi takriban kile kile ambacho ni cha kwenda na kurudi. Malipo hayo hayo ati ni kuwarejesha raia wa nchi nyengine kwao. Kwanini wasianze na kuwarejesha hao watanzania walio huko Oman kwao na ndege ni hizo hizo zilizowapeleka mara ya mwanzo

Je uamuzi huu wa Oman air haukiuki sheria za usafiri wa anga wa kimataifa.?
 
Mkuu tumeshawahi lips kwa kadi ya bank? Hizo ndo details zinazotakiwa
 
Gharama ya

Gharama halisi ya ticket kwa fedha ya Tz n ngapi?
 
Back
Top Bottom