Ubalozi wa tanzania beijing watoa tahadhari kuhusu mionzi ya nyuklia inayovuja japani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubalozi wa tanzania beijing watoa tahadhari kuhusu mionzi ya nyuklia inayovuja japani

Discussion in 'International Forum' started by Gamba la Nyoka, Mar 18, 2011.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Ni matumaini yangu , Pindi serikali yetu itakakapofahamu kwamba mionzi ya nyuklia imeanza kuelekea china,korea na vietnam itatimiza jukumu lake la kikatiba la kuwalinda raia wake kwa kuhakikisha inawarudisha Nyumbani Mara moja kabla mionzi haijafika huku. na ni matumaini yangu serikali ishaanza mchakato wa kuhakikisha Watanzania walioko Japani wanakuwa Salama.

  China kuna Watanzania wengi sana waliokwenda kimasomo kwa hiyo ni matumaini yangu kwamba serikali italifuatilia suala hili kwa umakini na uharaka unaotakiwa pindi hali itakapokuwa si nzuri.
   

  Attached Files:

 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...unaongelea serikali gani ya Tanzania?
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  wamejitahidi at least wametoa japo hilo Tamko.
  Tunaelewa fika kuwa TZ kila mtu anatakiwa atumie "bongo" kivyake vyake.

  Wakati mwengine hata hilo Tamko huwa hawatoi.
   
 5. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Wanafiki hawa lolote hao watu wa ubalozini,
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  1. Ni imani ya Ubalozi wa Tanzania Beijing kwamba Watanzania wanaoishi China na nchi za uwakilishi za Vietnam, Korea Kaskazini na Mongolia wanafuatilia maendeleo baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Japan tarehe 11 Machi, 2011 na kufuatiwa na sunami na kusababisha uharibifu katika vinu vya kuzalisha umeme vya nyuklia vilivyopo katika mji wa Fukushima nchini humo.

  2. Mamlaka za Japan zikisaidiwa na jumuiya ya kimataifa zimo katika jitihada kubwa kudhibiti uvujaji wa mionzi ya nyuklia ambao kama utatokea kwa kiwango kikubwa, utaweza kuathiri eneo kubwa ndani na nje ya Japan na kuhatarisha afya na maisha ya watu katika maeneo yataoweza kufikiwa na mionzi hiyo. Wote tunaomba juhudi hizo zifanikiwe ili kuepuka janga kubwa zaidi ya lililokwishatokea. Kama juhudi hizo zitashindikana, na kutegemea mazingira mbali mbali ya hali ya hewa, China itaweza pia kuathirika kwa kufikiwa na mionzi ya nyuklia kama itavuja kwa wingi huko Japan.

  3. Ingawa China na Japan zinatenganishwa na masafa marefu ya bahari, mionzi ya nyuklia kama itavuja kwa wingi Japan itaweza kufika China ingawaje kwa viwango vya chini baada ya kuchujuka njiani, kama pepo za baharini zitavuma kuelekea Kusini Magharibi kutoka sehemu yenye vinu vilivyoathirika. Hadi sasa pepo hizo zinavuma kuelekea Kusini Mashariki ambako ni eneo la bahari ya Pacific, lakini mwelekeo huo unaweza kubadilika wakati wowote.

  4. Kwa kuzingatia ukweli huo, Ubalozi unawashauri Watanzania wanaoishi China na nchi za uwakilishi wa Ubalozi huu, kuwa katika hali ya tahadhari.

  Tahadhari hizo ni pamoja na:-
  (a) Kufuatilia wakati wote hali ya mambo inavyoendelea kuhusiana na uvujaji wa mionzi ya nyuklia huko Japan.

  (b) Kujiwekea akiba ya kutosha ya chakula na maji ili kujiweka taari na ushauri wa kujifungia majumbani kama utabidi kutolewa na mamlaka za China. Zaidi ya vyakula vya kawaida vya kupika, ni muhimu pia kujiwekea akiba ya vyakula vikavu vya aina ya biskuti, “cookies” na vingine vinavyoweza kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.
  (c) Kujiwekea akiba ya kutosha ya dawa za msingi hasa kwa wale wenye magonjwa sugu kama vile shinikizo la damu na kisukari.
  (d) Kuweka tayari nyaraka za kusafiria ili kama utatokea ushauri wa kuondoka kwa dharura, mtu awe tayari mara moja.
  (e) Kwa wale ambao hawajajiandikisha Ubalozini, wafanye hivyo haraka iwezekanavyo, kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Ubalozi ?? ?? ?? ? ? official website of Tanzania embassy-beijing NO.8 liang ma he nan lu,beijing. Wanaweza pia kujindikisha kwa kuwasilisha taarifa zao Ubalozini kwa njia a barua pepe kutumia anwani za beijing@foreign.go.tz, ekitokezi@hotmail.com, manongign@yahoo.com au nukushi (fax) namba +86 10 65324351 au +86 10 65321695. Miongoni mwa taarifa za msingi zinazohitajika ni pamoja na:
  Jina
  Anwani ya Unapoishi
  Kazi Unayofanya
  Anwani ya Unapofanya kazi
  Anwani ya Barua pepe (e-mail)
  Namba za simu (mkononi; kazini; nyumbani)
  Paspoti: Namba
  Ilipotolewa
  Tarehe iliyotolewa
  (f) Kuarifu Ubalozi kuhusu jamo lolote lenye umuhimu katika kujiandaa na/au kukabili hali inayohusu janga la mionzi ya nyuklia au jambo jingine lolote. Zifuatazo ni miongoni mwa namba za simu za Ubalozi na Wanaubalozi zinazoweza kutumika:-
  +86 10 65321491/ 65321408/ 65322153
  +8613641337072
  +8613691408047
  +8613522860308

  Angalizo Muhimu :-
  Tangazo hili halimaanishi hata kidogo kuwa hali imeanza kuwa mbaya nchini China au kuna dalili za hali hiyo. Madhumuni yake ni kuwaweka Watanzania katika hali ya tahadhari na mwamko wa kufuatilia hali inavyo endelea. Kwa hivyo, hakuna haja wala sababu ya taharuki na fadhaa. Watanzania wanatakiwa wawe watulivu na waendelee na shughuli zao za kila siku na kuzingatia ushauri uliotolewa. Ubalozi utaendelea kuwa karibu na mamlaka husika za China na kutoa taarifa kupitia tovuti yake ?? ?? ?? ? ? official website of Tanzania embassy-beijing NO.8 liang ma he nan lu,beijing na/au njia nyingine yoyote, kila haja itapotekea.


  Ubalozi wa Tanzania, Beijing
  18 Machi, 2011
   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Tungekuwa tunapata feedback kama hizi hapa nyumbani kuhusu umeme tungekuwa mbali sana.
   
 8. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tunaomba Mungu hivyo vinu vipoe,wadhibiti mionzi tuepukane na janga hili.
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  duh,mungu apishie mbali kadhia hii
   
 10. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Acha kuwa hater kiasi hicho.. information ni muhimu kwa ndugu zetu wanaoshi china.. Ushawahi kufika china?!! hadi unaongea maneno hayo?!! you sounds like some one anyenunuwa bidhaa zao na kuanza kuwa ponda, nilifika china mwaka jana jiji la beijing! CHINA Imeendelea kupita kiasi and sure anga yao ipo polluted lakini wanajitahidi.. nadra sana kukuta hata karatasi iliyodondoka chini katika mitaa ya beijing! pale bongo pamoja na anga yetu ni ya blue! kipindipindu hakiishi.

  Ndugu zetu mlio china zingatieni hilo tangazo, mungu awabariki watanzania popote pale mlipo
   
Loading...