Ubalozi wa Marekani wekeni Akiba ya Maneno

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
3,398
2,990
Kama wengi tunavyojua, mlipuko wa ugonjwa wa coronavirus umeuweka uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 katika mazingira magumu sana. Ugumu huo unatokana na kauli za mara kwa mara za Bwana Trump za kuonesha kukosa utayari wa kukubali matokeo ya kushindwa uchaguzi.

Bwana Trump na wafuasi wake wanaamini kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa rigged in favor of Bwana Biden. Imani hiyo inatokana na hatua ya baadhi ya states kuufanya utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya posta kuwa default method. Kwa mujibu wa Bwana Trump na wafuasi wake, utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya posta umesheheni udanganyifu mkubwa sana, ambao unamnufaisha zaidi Bwana Biden

Bwana Trump tayari ameshapanga safu ya mapambano. Kuna kila dalili kwamba uchaguzi wa mwaka huu utakuwa an amplified replay ya uchaguzi wa mwaka 2000 uliowahusisha Bwana Gore na Bwana Bush, Jr.

Ingawa uchaguzi wa mwaka 2000 ulikuwa na mvutano kwenye state moja tu, bado uliweza kuutia doa mfumo wa demokrasia ya magharibi. Mvutano katika uchaguzi wa mwaka huu utahusisha several states na unaweza kufanya damage kubwa zaidi kwa reputation ya Marekani na mfumo mzima wa demokrasia ya magharibi.

Ubalozi wa Marekani, wekeni akiba ya maneno. Mkijifanya mnajua sana kunyoshea vidole mataifa mengine, mtaumbuka muda sio mrefu. Fainali za ligi zenu zinachezwa leo November 3, 2020. Kwa hali ilivyo, ni vigumu kuamini kwamba mtamaliza hii ngoma bila doa kubwa. Rais wenu anafahamika vizuri sana kwa narcissism yake. Hakuna maslahi ambayo ni makubwa kuliko maslahi yake mwenyewe. Hata maslahi ya Marekani sio makubwa kuliko maslahi yake. Kwa hiyo, jiandaeni kisaikolojia kwa yatakayojiri!
 
Kwanini Trump na yeye hao wafuasi wake wasimpigie kura kwa njia ya posta, kwani wamekatazwa?

Kama ana ushahidi wa udanganyifu wa kupiga kura kwa njia ya posta aende mahakamani, aache kelele za kujitangaza mshindi.

Lastly, wamarekani hawawezi kutuwekea sisi akiba ya maneno; usijidanganye, kwasababu mfumo wetu mzima wa kupiga kura mpaka kutangaza matokeo umeoza.

Marekani wana mahakama huru, kwetu mahakimu ni vibaraka wa jiwe, kule wana tume huru, kura zinahesabiwa kwa uwazi kila mtu anaona, kwetu kina Mahera ni waimba mapambio ya kumtukuza jiwe.

Sisi ni taifa la wajinga sana linaloweza kunyooshewa kidole na dunia nzima kama mfano wa taifa ambalo mifumo yake mingi ya kiuongozi na kiutawala imeoza kabisa inanuka, inatakiwa reform ya hali ya juu sana.
 
Kwahiyo na uchaguzi wa Marekani mawakala watafyekwa mapanga na green guard ili wapore masanduku ya kura?
 
Sieelewi unapolenga au labda hujui historia unayotaja hapa? Uchaguzi wa Marekani ulikwenda upande wa Bush dhidi Gore kwa sababu Bush alishinda jimbo la Florida. Bwana Gore alipinga ukweli wa matokeo hasa kwa sababu kulikuwa na kura maelfu ambazo zilitupwa kando kama si halali katika wilaya kadhaa za Florida.

Chama chake cha democrat walienda mahakamani mara kadhaa walipata ushindi kuhusu kura hizo kuangaliwa upya. Mchakato huo wa kuangalia karatasi za kura hapa na pale uliendelea wiki 4 hadi mwanzo wa Desemba 2000, wakati ule Bush alibaki tu na kura 537 zaidi kuliko Gore. Wakati ule Mahakama Kuu ilisimamisha mchakato wote ikasema muda umeenda, kikatiba rais mpya anahitaji kutangazwa karibuni hivyo basi ibaki ilivyo.

Sasa mkuu sijui unataka kusema nini kama ni doa kubwa kwenye sifa za Marekani. (Sina shaka ya kwamba mambo ya Bwana Trump hayaongezi sifa za nchi hiyo). Lakini ninajua nchi kadhaa ambako watu wengi wangemshukuru Mungu kama wangekuwa na haki na nafasi kupinga matangazo ya uchaguzi, kama wangeruhusiwa kupeleka jambo kwenye mahakama (hata zaidi ya mara 1 tu) na kama karatasi za uchaguzi zingeangaliwa kweli kutokana na azimio la mahakama, pamoja na wawakilishi wa kila chama kama watazamaji rasmi.

Unaonaje?
 
Sasa mkuu sijui unataka kusema nini kama ni doa kubwa kwenye sifa za Marekani. (Sina shaka ya kwamba mambo ya Bwana Trump hayaongezi sifa za nchi hiyo). Lakini ninajua nchi kadhaa ambako watu wengi
Usipate taabu na mleta mada. Anajaribu kuhalalisha ya jiwe kwa kujenga picha hasi ya uchaguzi wa Marekani.
 
Trampu Kwa nini asitumie tume na Polisi yeye si ndio chama Dola?.
Nadhani wewe ni clueless kuhusu Marekani. Kila state inaratibu na kusimamia chaguzi zote kwa sheria zake yenyewe. Kila state ina police wake yenyewe. Rais hana say yoyote kwa mamlaka za state!
 
Kwahiyo na uchaguzi wa Marekani mawakala watafyekwa mapanga na green guard ili wapore masanduku ya kura?

Usiwe na haraka; drama ndiyo kwanza imeanza!

Hata hivyo, hakuna wakala anayeshuhudia uhesabuji wa kura Marekani, isipokuwa kama mgombea/wagombea (w)ameomba recount!
 
Sieelewi unapolenga au labda hujui historia unayotaja hapa? Uchaguzi wa Marekani ulikwenda upande wa Bush dhidi Gore kwa sababu Bush alishinda jimbo la Florida. Bwana Gore alipinga ukweli wa matokeo hasa kwa sababu kulikuwa na kura maelfu ambazo zilitupwa kando kama si halali katika wilaya kadhaa za Florida. Chama chake cha democrat walienda mahakamani mara kadhaa walipata ushindi kuhusu kura hizo kuangaliwa upya. Mchakato huo wa kuangalia karatasi za kura hapa na pale uliendelea wiki 4 hadi mwanzo wa Desemba 2000, wakati ule Bush alibaki tu na kura 537 zaidi kuliko Gore. Wakati ule Mahakama Kuu ilisimamisha mchakato wote ikasema muda umeenda, kikatiba rais mpya anahitaji kutangazwa karibuni hivyo basi ibaki ilivyo.

Sasa mkuu sijui unataka kusema nini kama ni doa kubwa kwenye sifa za Marekani. (Sina shaka ya kwamba mambo ya Bwana Trump hayaongezi sifa za nchi hiyo). Lakini ninajua nchi kadhaa ambako watu wengi wangemshukuru Mungu kama wangekuwa na haki na nafasi kupinga matangazo ya uchaguzi, kama wangeruhusiwa kupeleka jambo kwenye mahakama (hata zaidi ya mara 1 tu) na kama karatasi za uchaguzi zingeangaliwa kweli kutokana na azimio la mahakama, pamoja na wawakilishi wa kila chama kama watazamaji rasmi.

Unaonaje?

In a tight race, marginal votes become very important. Kwa sababu ya partisanship, Mahakama ilishindwa kutumia busara kutatua hiyo dispute. The Court’s reputation suffered, na hilo historia imelibeba. I am not going to spoonfeed you; do your own little research!

Kitu kingine kilichopata attention kubwa ni ule mfumo wao wa electoral college. Mshindi anapatikana kwa wingi wa electoral votes badala ya wingi wa popular votes ambazo ndizo kielelezo cha utashi wa mpigakura mmoja mmoja. Kila inapotokea kwamba mshindi wa electoral votes sio mshindi wa popular votes, vidonda vya watu vinatoneshwa na watu wanaanza kuhoji legitimacy ya Rais aliyepatikana!

Utaratibu wa Tanzania wa kutokupinga matokeo mahakamani ni urithi uliopitwa na wakati. Hata hivyo, hilo ni swala la kikatiba ambalo lina mchakato wake tofauti na mchakato wa uchaguzi. Katiba Pendekezwa ilikuwa na jibu la hii shida.
 
Usipate taabu na mleta mada. Anajaribu kuhalalisha ya jiwe kwa kujenga picha hasi ya uchaguzi wa Marekani.

Mkuu, hebu jaribu kuwa mtu asiyekuwa muadilifu na kila mtu nyumbani kwako alijue hilo. Then, jaribu kuwafundisha wanao uadilifu huku ukiendelea na tabia yako ya kutokuwa muadilifu. Mwisho, fanya evaluation ya juhudi zako za kufundisha wanao madili mema!
 
Kwanini Trump na yeye hao wafuasi wake wasimpigie kura kwa njia ya posta, kwani wamekatazwa?

Kama ana ushahidi wa udanganyifu wa kupiga kura kwa njia ya posta aende mahakamani, aache kelele za kujitangaza mshindi.

Lastly, wamarekani hawawezi kutuwekea sisi akiba ya maneno; usijidanganye, kwasababu mfumo wetu mzima wa kupiga kura mpaka kutangaza matokeo umeoza.

Marekani wana mahakama huru, kwetu mahakimu ni vibaraka wa jiwe, kule wana tume huru, kura zinahesabiwa kwa uwazi kila mtu anaona, kwetu kina Mahera ni waimba mapambio ya kumtukuza jiwe.

Sisi ni taifa la wajinga sana linaloweza kunyooshewa kidole na dunia nzima kama mfano wa taifa ambalo mifumo yake mingi ya kiuongozi na kiutawala imeoza kabisa inanuka, inatakiwa reform ya hali ya juu sana.
Kwa nini asiandamane kama kina Mbowe?
 
Huna akiri wewe, hapa kwetu unataka uingie barabarani sasa kwa nini usiseme Trump nae aingie barabarani ila unasema aende mhakamani?
Mbona nyie hapa mnataka kuingia barabarani badala ya kwenda mahakamani?
Kwa hiyo hao wamalekni ni bora zaidi kuliko ninyi wao waende mahakamani ila nyie muingie barabarani, huo ni ujuha kabisa.
Fateni sheria nanyi nendeni mahakamani.
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania inafuatilia kwa ukaribu sana mchakato aa uchaguzi wa marekani, kumekuwa na malalamiko mengi sana juu ya wizi wa kura, tunaitaka marekani ichukue hatua za haraka kufanyia kazi malalamiko hayo. Tanzania itachukua hatua kwa maofisa wote wa marekani watakaobainika kuvuruga uchaguzi huo.
 
Back
Top Bottom