#COVID19 Ubalozi wa Marekani, watoa tahadhari dhidi ya ongezeko kubwa la ugonjwa wa Covid-19

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
1.jpg


2.jpg

Chanzo: Tahadhari ya Kiafya - Ongezeko la visa vya COVID-19 | Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
 
Corona inaua sio utani, rafiki kafariki tumemzika mchana, kaanza kuumwa asubuhi shida kupumua mchana kafariki saa tisa tumetoka kumzika, nilivyoona ile misafara ya Coaster inayosindikiza marehemu wao mikoani sina hamu kabisa.

Kama mpaka sasa bado kuna mtu asieamini Tanzania kuna Corona Mungu amrehemu.
 
Hebu watupumzishe!!! Wameshindwa kuzuia vifo100 vya kupigwa risasi kila siku halafu hapa wanataka kutuongopea wanajali uhai wetuwetu

Tuko zetu busy na kazi huku tukichukua tahadhari na kumwomba Mungu sana.
Sijui unaandika haya ukiwa wapi, inawezekana umejifungia ndani hujui chochote kinachotokea mtaa wa pili, kwa taarifa yako mkiendekeza hizi taarabu Corona itapokuja kupiga hapo sebuleni kwako ndio utapata akili, now unaisikia kwa majirani ndio maana unaleta utani, na usiombe iwatembelee ndani kwasababu haiondoki na mmoja.
 
Tumeshindwa kutoa tahadhari wacha mataifa yenye nguvu wafanye hiyo.

Kutukuwepo kwa dawa na chanjo ya uhakika ni jambo moja, na kutoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ni jambo lingine. Hivyo, kutokuwepo kwa chanjo ya uhakika na dawa ya ugonjwa huu, hakutoia uhalali wa kufuchwa takwimu za ugonjwa pamoja na halihalisi ya maambukizi kwa umma.
 
Sijui unaandika haya ukiwa wapi, inawezekana umejifungia ndani hujui chochote kinachotokea mtaa wa pili, kwa taarifa yako mkiendekeza hizi taarabu Corona itapokuja kupiga hapo sebleni kwako ndio utapata akili, now unaisikia kwa majirani ndio maana unaleta utani, na usiombe iwatembelee ndani kwasababu haiondoki na mmoja.
Naandika nikiwa hospitali nauguza.... kama wewe unaweza kuzuia corona Mungu aendelee kukupigania.
Hakuna anayefurahia magonjwa na vifo, na hakuna anayefurahi au anayeweza kukimbia kifo pia
 
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari ya ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Katika taarifa yake iliyotumwa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ubalozi huo, umesema kuwa kumekua na taarifa za ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona tangu mwezi Januari.

‘’…hatua za kuondosha na kuzuia maambukizi ya Covid-19 bado zimeeendelea kuwa za kiwango cha chini, serikali ya Tanzania haijatoa takwimu zozote kuhusu visa vya maambukizi au vifo vilivyotokana na Covid-19 toka mwezi Aprili 2020’’ inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Ubalozi huo pia unasema hospitali na vituo vya afya nchini Tanzania vinaweza kuzidiwa kwa haraka na idadi ya wagonjwa.

‘’Uwezo mdogo wa hospitali nchini kote Tanzania unaweza kusababisha wagonjwa walio katika hali ya dharura kuchelewa kupatiwa huduma, jambo linaloweza kuhatarisha maisha.’’

Taasisi mbalimbali zimeendelea kutoa tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Tanzania (SUA) ilitoa taarifa hapo jana kwa wanafunzi na wafanyakazi wake kujilinda dhidi ya maambukizi ya corona.

Nacho Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilitoa waraka wa kuchukua tahadhari ya kujilinda na maambukizi ya corona.

Hata hivyo waraka huo ulibatilishwa na wizara ya elimu kwa kukiuka utaratibu uliotolewa na wizara ya afya.

Mwezi uliopita Kanisa Katoliki nchini Tanzania lilitoa tahadhari juu ya wimbi jipya la maambukizi ya corona na kuwataka wananchi kuchukua hatua zote za kujikinga.

Tahadhari hiyo ilitolewa kupitia waraka ulioandikwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga.

Hata hivyo Wizara ya afya nchini humo bado haijathibitisha taarifa za uwepo wa wagonjwa au vifo vinavyo sababishwa na wimbi jipya la virusi vya corona.

Mara ya mwisho kutolewa kwa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona ilikua mwezi Aprili mwaka jana.

Chanzo
BBC
Tovuti ya Ubalozi wa Marekani

 
Sasa ni wazi kua covid Tanzania inaua watu vibaya sana. Magufuli yeye bora watu waendelee kufa kuliko kuwaambia wachukue tahadhari za kisayansi, yeye anahimiza njia za kienyeji na za kishirikina za kujifukiza, kunywa pilipili, sijui kachumbari.

Ni mambo ya ajabu.
 
Back
Top Bottom