Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 43,905
- 150,212
Kwa kwa kwa kwah kwah kwah ...makofiiiiiPoint ya Nyerere ya kwamba ili maendeleo yawe ni maendeleo ya watu ni lazima kuwe na uhuru wa watu pamoja na demokrasia unaikwepa ndiyo maana unaiita ni "mengineyo".Unaikwepa kwa sababu unajua maendeleo anayofanya Magufuli yanapinga uhuru wa watu pamoja na demokrasia.Point hiyo haiwezi kuwa ni "mengineyo" kwa sababu hata Nyerere mwenyewe amesema kuwa huwezi kusema kuwa una maendeleo wakati watu wanaishi kwa hofu.Uhuru na demokrasia ndiyo point kubwa na point namba moja katika kujenga uhuru wa watu na siyo "mengineyo" kama unavyojinasibu hapa.
Halafu suala la kwamba kugandamizwa kwa uhuru na demokrasia inazuia haki zangu za kufanya maendeleo au laa ni pointless.Nina haki ya kupata uhuru wangu kamili pamoja na demokrasia ninavyotaka ila mradi sivunji sheria halali.Ni haki yangu kuwa na uhuru kamili.Huwezi kugandamiza uhuru wangu kwa kigezo kuwa hainiathiri katika kufanya maendeleo.