Ubalozi wa Marekani nchini watoa mafunzo kwa FFU ubalozini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Amb+with+Police+Officers+008.jpg

Balozi wa Marekani nchini Alfonso akiwa kwenye picha ya pamoja na Israeli Makongo wa tatu toka kulia waliosimama mstari wa mbele tarehe 10 walipokuwa ubalozi wa Marekani mafunzo ya FFU na kikozi kizima kufundwa utendaji kazi uweje katika matukio ya dharura.

  • Je, wamefunzwa kutesa wananchi au kuokoa wananchi?
  • Je, wamefunzwa kuua wananchi au kulinda uhai wa wananchi?
  • Je, wamefunzwa maana na nafasi ya matumizi ya silaha za kujihamu inapotokea dharura?
 
Angalia picha hizo huyo askari mmarekani alivyosimama na tazama yake tofauti na waliojaa magwanda wa FFU. Halafu na ule mpini kiunoni lakini nadra sana kuutumia, na huenda hajawahi hata kuvuta trigger yake maishani ila awapo kwenye mazoezi ya kulenga shabaha.

Hawa wa kwetu na magobole yao laiti wangekuwa na hizi trigger za hawa jamaa tungekoma ubishi kwenye maisha yetu na ujambazi, ndo maana hawa wakuu wao wameamua waendelee kutumia yale magobole aka shemeji ningoje.
 
Amb+with+Police+Officers+008.jpg

Balozi wa Marekani nchini Alfonso akiwa kwenye picha ya pamoja na Israeli Makongo wa tatu toka kulia waliosimama mstari wa mbele tarehe 10 walipokuwa ubalozi wa Marekani mafunzo ya FFU na kikozi kizima kufundwa utendaji kazi uweje katika matukio ya dharura.

  • Je, wamefunzwa kutesa wananchi au kuokoa wananchi?
  • Je, wamefunzwa kuua wananchi au kulinda uhai wa wananchi?
  • Je, wamefunzwa maana na nafasi ya matumizi ya silaha za kujihamu inapotokea dharura?

Mzungu aliye kwanza kushoto kwa balozi ndiye mtoa nadharia ya mafunzo, na huyo young white guy mwenye trigger kiunoni mwenye vumilia vumbi mbili ndiye mtoa mafunzo kwa vitendo.
 
watakuwa wamefunzwa kupambana na wanaopinga uwekezaji wa wamarekani migodini
 
Kozi muhimu kwa hawa ingekuwa "Haki za Binadamu", maana mafunzo kwa vitendo tayari wako kamili, tulishaona jinsi wanavyoshughulikia matukio yote kama vile Majambazi, Wazee wa Afrika Mashariki na Wanafunzi wa UDSM.
 
Huenda ndilo la muhimu zaidi lililokaziwa katika mafunzo yao, vinginevyo kuacha hali endelee ilivyo utendaji wao ni utata tu.

FFU wanakwenda kusaidia waathirika na mafuriko wanarandaranda na bunduki huku wamezishika mikononi kama wapo kwenye mapigano, mafunzo gani haya kama si vitisho kwa waathirika na mafuriko? Badala ya kwenda kusaidia kuhamisha vitu na kuokoa maisha yao wao wanarandaranda na maji ya kuwasha na bunduki na mabomu maeneo ya waathirika, haina mantiki hata kama watatoa utetezi dhaifu kwamba kulinda mali za waathirika si kwa utaratibu na mwendo huu kama wako vitani.
 
Marekani wana hulka ya kumlinda kiongozi mwenye masilahi kwao, asingkuwa na masilahi kwao wangeshalalamika ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Duh hao jamaa wa Fanya Fujo Uone wanapenda kupiga weee acha tu. Wakisikia kuna kavalangati sehemu wanaibuka na mirungu kazi yao kupiga. Kenya walikuwa wakipiga kama hawa wa Tz lakini katiba mpya imewanyoosha, hawapigi tena. Kuna kisa kimoja hivi karibuni mama mmoja alipigwa TV zikaonyesha ikabidi polisi mpigaji akamuombe msamaha mama baada ya kuwa amefutwa kazi!!
 
Americans are strategic!! Lazima waivute human resources inayotumiwa hata njee ya ngome yao!!

Nimesema wawavute vute maana FFU wetu wanachokijua ni kusubiri mtu mwingine amsaidie kufikiri cha kufanya!! Heko US Embassy Dar- Tusaidieni tu maana mabakuli ndo staili yetu!!
 
..msisahau kwamba WAMAREKANI wanaruhusu USHOGA, tena wa waziwazi, ktk MAJESHI yao.

..nadhani Watanzania tukatae mafunzo ya aina yoyote ile toka kwa majeshi yanayoendekeza ushoga.
 
..msisahau kwamba WAMAREKANI wanaruhusu USHOGA, tena wa waziwazi, ktk MAJESHI yao.

..nadhani Watanzania tukatae mafunzo ya aina yoyote ile toka kwa majeshi yanayoendekeza ushoga.
Wale wanaobana bana makalia na kuweka mwiko wa kuyazungumzia ndio MASHOGA KITAAMBO... tusiisau pwani ya afrika mashariki yenye mila ya arabuni. mafunzo ni freshi, lakini isiishie jeshi tu
 
Wale wanaobana bana makalia na kuweka mwiko wa kuyazungumzia ndio MASHOGA KITAAMBO... tusiisau pwani ya afrika mashariki yenye mila ya arabuni. mafunzo ni freshi, lakini isiishie jeshi tu

Pharaoh,

..at least pwani ya afrika mashariki na uarabuni wanaonyesha kujikakamua kuukataa ushoga.

..wamarekani wenyewe wameukubali na kuufanya moja ya maadili yao.

..kwa kweli hapa waziri membe amelala usingizi, ukizingatia alivyompayukia Cameroun.

..Waziri Membe alitakiwa amuite balozi wa marekani na kumuonya!!
 
Tatizo la bara la Afrika na Middle East wanakataa kwa maneno lakini kwa matendo hufanyika kila kukicha, huu ni usaanii tu.
 
Siasa ni moto wa kifuu na Kujinga jina ni kazi ngumu ndo sababu inahitaji umueleze kitu anachokipenda.
 
Wakuja,

Lazima kwanza ujuwe, balozi zote za USA zinalindwa na US Marines na siyo FFU wa USA.

US Marines ni wanajeshi na FFU ni POLISI na hapo ni vitu viwili tofauti. Mmoja anatuliza fujo wakati mwngine ANAUWA.

Huyo kijana unayemuona hapo, ni mlinzi wa ndani ya jengo maana kwenye mageti hawasimami, ni US Marine.

Nenda kaangalie hata film ya THE BORNE IDENDITY utawaona wengi ndani ya jengo.

Marines.jpg

Simply Because It Is: Navy SEALs Vs. US Marines
Mzungu aliye kwanza kushoto kwa balozi ndiye mtoa nadharia ya mafunzo, na huyo young white guy mwenye trigger kiunoni mwenye vumilia vumbi mbili ndiye mtoa mafunzo kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom