Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa tahadhari nyingine ya shambulio la kigaidi nchini humo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,291
2,000
Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda.

Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara .

Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi.

Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo

Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,666
2,000
Hizj habari wanazipata wapi?
Kwanini wasiwakamate hao magaidi
Hiyo ndiyo inaitwa intelligence ndugu yangu. Puuzia shauri yako. Mara nyingi yakitokea unasikia tulikuwa tumewaambia lakini walipuuza. Hata kule Sri Lanka walikuwa wametonywa, wakapuuzia na makanisa yakashambuliwa! Nafikiri kuna watu hatimaye walifukuzwa kazi.
 
Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
996
1,000
Lakini binafsi ninaona Ubalozi husika umekosea bwana.Sasa walishindwa nini kuwashirikisha watu wa usalama wa nchi wenyeji? Kweli unabaini taarifa nyeti kama hizi kisha unalipuka kwenye media as if nchi hii haina mamlaka yake?Au jamaa zetu waligoma nini kutoa ushirikiano?
 
Dalalims

JF-Expert Member
Apr 6, 2019
235
250
Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda.

Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara .

Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi.

Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo

Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.
NI YALE YALE TUU.
 
Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
4,770
2,000
Lakini binafsi ninaona Ubalozi husika umekosea bwana.Sasa walishindwa nini kuwashirikisha watu wa usalama wa nchi wenyeji? Kweli unabaini taarifa nyeti kama hizi kisha unalipuka kwenye media as if nchi hii haina mamlaka yake?Au jamaa zetu waligoma nini kutoa ushirikiano?
wanajua akili zetu tutakanusha na kulaumu...na wazungu walivyo wajanja mkikomaa na kelele zenu ...wanaweza kuomba hata samahani ...lakini ukweli ndio huo!
 
Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
996
1,000
wanajua akili zetu tutakanusha na kulaumu...na wazungu walivyo wajanja mkikomaa na kelele zenu ...wanaweza kuomba hata samahani ...lakini ukweli ndio huo!

Dah! wametuweza. Ninaona jamaa zetu hawakufurahishwa lakini wamejidhibiti katika kuwaka.Ingekuwa vibonde fulani, mfano, nchi jirani hapo ama mtanzania mmoja tu hivi angekiona cha mtemakuni.
 
KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,996
2,000
Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda.

Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara .

Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi.

Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo

Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.
Hao ni wakenya wanahangaika na biashara ya Utalii siyo Wamarekani.Si unajua kuwa usalama wa watalii nchini Kenya in shida.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom