Ubalozi wa India wawatahadharisha raia wake dhidi ya ajira za MeTL

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Ubalozi wa India nchini Tanzania umewatahadharisha raia wake wote kutokubali kuajiriwa na kampuni ya MeTL ya Mo Dewji.

Hatua hiyo imekuja baada ya kupata taarifa za manyanyaso kwa wafanyakazi hao ikiwemo kulazimishwa kulazimisha kujaza kesi za uwongo na kukamatwa.

Katika taarifa yao Ubalozi wamesema walipokuwa wakipata malalamiko na kuwasiliana na uongozi wa MeTL wamekuwa wakipata majibu yasiyo na staha.

Katika taarifa yao waliyoandika Facebook wamesema kumekuwa na vishawishi wafute ‘post’ hiyo lakini kwa kuheshimu utu wa wahindi wamesema hawatafuta.
==

PIA, SOMA=> Ubalozi wa India wazungumza na Mo Dewji


9E9B894F-FF71-45D1-A9E5-B977CEDC78E7.jpeg


 
Kina Dewj ni Wabongo sio Wahindi.

Hapo tu ndio Wahindi wa India wanapojichanganyaga wakidhani ni Wahindi wenzao.

Kumbe ni Wabongo tena wa mikoani.
Kwa hio wana ule ukorofi wa kibongo.

Wakenya wanatutambua sana wabongo balaa letu.
 
Kuna Magheto ndani ya viwonder vyake. Pale wanakaa ma supervisor wa viwandani Ila hawaruhusiwi kutoka nje ya geti maana hawana vibali vya kukaa nchini.

Ni ma supervisor lakini ni slave labourers. Wana roho mbaya kuliko ya mbwa Koko dhidi ya vibarua wa kiswahili. Mo au ndugu yake akiingia kiwanda utadhani ni vimbwa vinatingisha mkia boss akiwatupia mfupa uliooza.
 
Zamu ya Mo sasa
Kuna magheto ndani ya viwonder vyake. Pale wanakaa ma supervisor wa viwandani Ila hawaruhusiwi kutoka nje ya geti maana hawana vibali vya kukaa nchini.

Ni ma supervisor lkn Ni slave labourers. Wana roho mbaya kuliko ya mbwa Koko dhidi ya vibarua wa kiswahili. Mo au ndugu yake akiingia kiwanda utadhani Ni vimbwa vinatingisha mkia boss akiwatupia mfupa uliooza.
 
Hawa wahindi wanaoajiriwa Tz huwa sielewi nikwanini wamejazana Tz huku, kuna watz kibao wenye sifa. Nampongeza Magufuli kwa kuanza kukataa ku renew vibali vyao vya kazi mara wamalizapo mikataba yao, nahili limeanza December hii.
Hahaha wakondoka mkabaki peke yenu mtaanza kuwatafuta na kuwalinda.

Mlisema hamtaki hata harufu ya Chadema, leo covid-19 wanalindwa kwa nguvu zote.

Hawa wahindi mtawatafuta na mtawalinda, hiyo ndo ccm tunayoifahamu.
 
Back
Top Bottom