Ubalozi wa China Nchini waishukia BBC kwa kutunga Uongo, ni kuhusu China kufungua vituo vya polisi Tanzania

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,413
7,678
Ubalozi wa China nchini Tanzania umeikituhumu chombo cha habari cha Uingereza(BBC) kwa kutunga habari. Ubalozi huo umesema habari ya China kufungua vituo vya polisi Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania ni uthibitisho unaoonesha jinsi BBC inavyosambaza taarifa zisizo za kweli kuhusu China ili kuvunja uhusiano wa China a Afrika.

Ubalozi umesisitiza China na Tanzania wanafurahia urafiki wa muda mrefu kwenye nyanja zote ambao hauwezi kutikiswa na tetesi au kuharibu taswira kwa taarifa za uongo.

Hata hivyo ubalozi huo haukueleza ukweli ni upi katika taarifa hiyo.

BBC China.jpg
 
Ukweli ni kwamba Zambia kuna mpaka Polisi Wachina.

BBC wanajuwa vizuri njama za Wachina wala hakuna fabrication story yoyote hapo, ni ukweli mtupu
 
Wanakanusha nini hawa Wakomunisti wakati mambo wanayofanya Zambia yako hadharani.

Wakijifanya kufungua Kituo hapa kinyume na Katiba tunakitia kiberiti.
 
Wanakanusha nini hawa Wakomunisti wakati mambo wanayofanya Zambia yako hadharani.

Wakijifanya kufungua Kituo hapa kinyume na Katiba tunakitia kiberiti.
Magu ndio anaweza hivyo. Hawa wengine watawapa na ardhi kabisa wafungue na chuo cha kipolisi cha kichina.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom