Ubalozi wa CCM UK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubalozi wa CCM UK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmakonde, Mar 9, 2010.

 1. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naona ubalozi wetu huko London unawakilisha CCM zaidi ya serikali ya Tanzania.Tangu balozi wa sasa ateuliwe balozi nyingi zimefunguliwa karibu nchi nzima.Juzi alihudhuria mnuso wa CCM huko mjiniu Reading na Mdugu Msekwa,ambapo Ndg Msekwa alitoa kadi za CCM kwa waTz kama 70 hivi.

  Hii trend ya Politisation ya balozi zetu na kuwa part ya CCM propaganda inakwenda kubaya.Kuna thread ya watu wa NewYork wanataka kuanzisha Chama chao cha wa Tz ,surely wawe makini maana UK hakuna tofauti ya Serikali/CCM/Bunge.
   
 2. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM Uingereza[​IMG]Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa ambaye anadaiwa kugawa kadi za chama chake usiku nchini Uingereza.[​IMG]Sadick Mtulya

  MAKAMU mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa juzi alikaa hadi usiku wa manane katika mkutano wake na Watanzania waishio Uingereza akigawa kadi za chama hicho tawala.

  Habari kutoka Uingereza zimelieleza gazeti hili kuwa katika mkutano huo Msekwa alikabidhi katiba ya CCM kwa tawi la CCM la jijini London, kadi kwa zaidi ya wanachama 70 na vifaa vingine kadhaa.

  Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Uingereza zimeeleza kuwa Msekwa alikabidhi vifaa hivyo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Warehouse mjini Reanding ulioanza saa 11:00 jioni ambao pia ulihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini humo, Mwanaidi Maajar.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Msekwa alishangazwa na jinsi Watanzania hao walio ughaibuni walivyoweza kuimudu salamu ya chama hicho ya ‘kidumu Chama Cha Mapinduzi,… Kidumu,… CCM mshikamano mnatoa’.

  Katika hafla hiyo Msekwa aliinadi CCM kwa kueleza historia yake na kuwataka Watanzania hao wakienzi chama hicho kwa vitendo.

  “Mkutano wetu na Msekwa ulianza saa 11:00 jioni na kumalizika usiku wa manane, alikabidhi kadi mpya za uanachama zaidi ya 70, katiba ya CCM na vifaa mbalimbali kwa ajili ya matawi mapya yaliyofunguliwa huku," chanzo cha habari kutoka Uingereza kilidokeza.

  "Wakati akikabidhi vitu hivyo alikuwa na Balozi Maajar na kabla ya yote hayo alitoa historia yake na ya chama kisha akatuhimiza tukidumishe chama hicho, lakini alishangazwa sana na salamu ya wanaCCM wa huku ya ‘kidumu Chama Cha Mapinduzi... Kidumu. CCM mshikamano mnatoa" alieleza mtoaji huyo wa habari.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa wanachama waliohudhuria ni kutoka katika matawi ya Manchester, Reading, Birmingham, na London.

  Hata hivyo kwa ujumla wanaCCM wote wanaoishi Uingereza wanajulikana kama CCM tawi la London.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati alisema Msekwa alikwenda London kwa mwaliko wa wanaCCM wanaoishi Uingereza kwa ajili ya kusherehekea kutimiza miaka 33 ya chama hicho.

  "Huu ndio wakati wenyewe wa maandalizi... kila chama kinahangaika kutafuta ushindi. Hakuna anayelala," alisema Chiligati juzi.

  Aliongeza kusema: “CCM ina wanachama wengi nje ya nchi na hasa katika bara la Ulaya. Pia ina mashina na viongozi wake huko na hata hii safari ya Msekwa ni mwaliko maalumu kutoka kwa wanachama wetu wa Uingereza. Wamemwita kwa ajili ya kusherehekea CCM kutimiza miaka 33.”

  Awali baadhi ya vyanzo vyetu vilidai kuwa Msekwa alikwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya kampeni juu ya uchaguzi mkuu wa Oktoba.

  "Ukweli ni kuwa Watanzania wengi waishio huku, wamepanga kurudi nyumbani Tanzania kabla ya Oktoba ili kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi," kilisema chanzo chetu.

  "Kutokana na sisi (Watanzania) kujuana mahali tulipo huku na pia viongozi wa CCM kujua hilo ndio maana wamewaita viongozi hao ili waweke mambo sawa."

  Uamuzi huo wa CCM kufanya kampeni nje ya nchi umekuja huku bado sheria zikiwa haziruhusu Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupiga kura.

  Hata hivyo, Chiligati alisema mchakato wa utaratibu wa jinsi Watanzania waishio nje ya nchi watakavyoshiriki kupiga kura wakiwa nje ya Tanzania upo katika hatua nzuri.

  "Mchakato wa uwekaji utaratibu wa jinsi Watanzania waishio nje ya Tanzania kupiga kura wakiwa huko unakwenda vizuri japokuwa sina uhakika kama hili litafanyika uchaguzi huu wa Oktoba," alisema Chiligati.

  Mwenyekiti wa CCM wa tawi la Birmingham, Uingereza, Peter Gabagambi alithibitisha kufanyika kwa sherehe hizo pamoja na kutolewa kwa kadi mpya kwa ajili ya wanachama pamoja na kukabidhiwa kwa vifaa na katiba ya CCM kwenye matawi mapya. Alipotakiwa kuzungumzia taarifa za awali kwamba moja ya mambo yaliyompeleka Msekwa Uingereza ni kampeni za uchaguzi mkuu, Gabagambi alijibu, "Haa haa, sio kweli, ni sherehe tu za CCM."
  Tuma maoni kwa Mhariri
  [​IMG]Facebook Contact Us
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Subiri CUF ingiie Madarakani nao itakuwa hivyo hivyo!
   
 4. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natanguliza samahani kwa kuuliza hili swali (maana it might be the most stupid question)

  Swali: Hivi ni legal kuanzisha tawi la chama cha siasa cha nchi nyingine kwenye another country. Mfano Tanzania inavyoanzisha matawi ya CCM abroad kama UK and US?
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kidumu Chama Cha Mapinduzi..
   
 6. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Weka pic yako wazi!
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wewe umeweka yako wazi?
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I mean your file attched is hard to download!
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Linahitaji marekebisho "size editing" kabla sijaliweka...soon
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  wakuu habari hizi zinanisikitisha sana. Kama tumeanza kuhalalisha shughuli za kisiasa nje ya nchi tutakuwa tujatigea bomu ambalo siku likilipuka tutakuwa hatuana wa kimlaumu. I wonder kama sheria za UK zinaruhusu mambo kama hayo, na iwonder kama waingereza wanaruhisiwa kuwa wanachama wa CCM na kuichangia CCM (watanzania waliojilipua ni waingereza, na baadhi yao ndio waanzishaji na wachangiaji wa matawi hayo).

  Who will have balls to point fingers at CUF kwa kuanzisha matawi Afghanstan, Yemen na Pakistan. Who will point fingers at CUF if funded by hizbulah and Mujahdeen? Nashangaa sana kusikia watu wenye vyei vya juu sana CCM wanafanya mambo ya ajabu, na ssi wengine tunachekelea.
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umesema point kabisa kwa sasa inaonekana kama fasheni na sifa kwa viongozi wakuu kufungua matawi nje ya nchi lakini itakapofikia hatua ya hayo matawi kuanza kuchangia harakati za vyama nchini kwa kutumia fedha chafu na haramu tusilaumiane kama ulivyosema hii itatoa loop hole kwa vikundi hata vile viovu vya kigaidi kujiingiza kwenye siasa za nchi yetu kwa mgongo wa matawi ya chama

  mfano hii sheria ya uchaguzi kuzuia misaada kutoka nje itafanyaje kazi kama misaada itatolewa na tawi la chama lililo nje ya nchi basi itabidi itungwe sheria nyingine ya kubainisha misaada inayotolewa na matawi ya nje haitakiwi kitu ambacho nadhani hakitawezekana
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  We bonglander ikawaje ukaequate CUF na Hezbollah? yani sababu gani iliyofanya uone CUF ndio itapata funding za kutoka kwa terror organizations. That is profiling is it not? That is a rather stupid type of comment.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wewe ndio unaonekana mypic hapa. Bongolander ameonesha tu kwamba kufungua mlango kwa shughuli za vyama nje ya nchi vinaeza kuzua tatizo kubwa zaidi, na mfano akautoa hapo. Sasa sioni comment hii inaezaje kuwa ya kipumbavu kaa sio wewe ndio mpumbavu.
   
 14. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very good point... :D i am not sure kama hawa waTZ wetu wa UK wanajiuliza hili swali (maana kuna watu wapuuzi sana huku, to be honest if you are in abroad ni marakumi uwe na marafiki non tanzanians )? and i am not sure if our government really has thought about the possible Consequence of matawi ya political parties nje ya nchi...
   
 15. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,715
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  sioni jipya katika hii habari....hivi tumewahi kutofautisha kati ya chama na serikali?

  hivi unaweza kumzuia kikwete asiipigie debe ccm wakati yeye ni mwenyekiti?

  kwangu mimi...mstari unaotofautisha ccm na serikali ni mwembamba sana kiasi huwezi kujua sasa kiongozi anafanya shughuli ya chama au serikali.....na ni kwa mantiki hii unaweza kuona umuhimu wa kuondoa suala la kofia mbili....mawaziri kutokuwa wabunge...nk. nk.
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu wewe ndiye unasema Hezbollah ni terror organisation. I did not say that. Najua kwa ukienda Lebanon watu wanajua kuwa hao ni freedom fighters na hapa kwetu watu wanaweza kutumia msingi huo kuchukua funds, mbinu na ujuzi kwao. That is not being myopic, kwanza hapa kwetu Tanzania tuna historia ya chama kama hicho, najua kuna watu visiwani mpaka leo wanakuwa associated na chama hichol kwa sababu za kisiasa.

  So you can call it myopic or stupid comment, (legitimate accusation) but that, in my opinion, does not legitimize activities of Tanzanian political parties abroad. That is depriving those which can not operate abroad. And i would not like to see our parties serving those with money abroad than us we we feel the heat.

  And i was not meant to ally CUF with terror groups, no ally any party for that matter, to the other side of the war on terror. Sorry if i offended you in any way.
   
 17. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Future-Tanzania!
  Inabidi tukupepee tukutoe mapepo sasa kwa akili yako ni ubalozi upi ambao sio wa CCM. You could be one of the chokambaya's. As long as CCM ndio wanatawala Tanzania mabalozi wote wataendelea kuwa wana CCM na harakati za kufungua matawi ni kuwavuta karibu hao wakimbizi wa kuichumi/malimbukeni waweze kuwachangia. Hujiulizi kwa nini Membe anapigia debe dual citizenship ni maudhui hayo ya kuganga njaa na kuwawezesha kupiga kura kutoka huko ukimbizini. Hao popo wanataka recognition baada ya kushindwa kuwa assimilated fully huko ughaibuni!!!
   
 18. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Bomu litalipuka tu hivi karibuni.I am sure kuna watu hawa SISIEM wana motive moja,either kupata madaraka/kazi wanaporudi Tanzania maana tayari wamejenga connection hasa viongozi wa matawi haya.

  Also kuna agenda ya ufisadi,wengi hawa wanaweza kutumiwa kuwa recipients wa dirty money kutoka Tanzania.Siamini kabisa kuwa hawa wanachama ughaibuni
  wana pesa ya kuchangia CCM,rather ni pesa iliyoibwa Tanzania na kuwa recycled tena
   
 19. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I couldnt understand you mate (on the red highlight)!!!

  I personal dont care balozi ni CCM or not.. my question was government imefikiria diplomatic legal issues ambazo zinaweza kutokea kwa kufungua hayo matawi? na je sheria za inchi hizo zinaruhusu nje nyingine kufungua matawi ya polical parties kwenye nchi zao?

  Kuhusu dual citizenship, its not only about kuwafanya watu wapige kura but also to
  attract talented Tanzanians ambao wanauraia wa nchi nyingine kuweza kuja Tanzania kufanya kazi na kuimarisha uchumi.. Tanzania has a shortage of high skilled people na hao high skilled professionals ndio wanaofanya kazi abroad so why not change the law to make it easy for people tanzanian born kuja kufanya kazi tanzania?
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni Bongofever basi. Ukiwa na kadi hilo la kijani basi hutosongwa na mtu na ukifika Bongo mambo yako yatakuwa ni nafuu kwani unakuwa mwenzetu! Si unajuwa wa nje wamekalia kuupinzani pinzani.
   
Loading...