Ubalozi usiwe tena ni eneo la kuwapa makada wa CCM waliokosa vyeo

Oct 7, 2019
51
156
January mwaka huu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi alisema bila juhudi za Rais John Magufuli, fursa za kufundisha lugha ya Kiswahili Afrika Kusini in getupita… “Fursa hiyo ingepita si kwasababu nyingine yoyote ile, uzembe wetu wenyewe”
Aliyasema haya katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi wapya akiwemo Dr Benson Bana.

Hii ni fursa Moja kati ya nyingi ambazo taifa hupoteza kutokana na uzembe wetu wenyewe. Anachokiongea Kabudi hapa kinamaanisha (Mabalozi) wetu hawaifanyi kazi yao ipasavyo huko njee ya nchi.

Mwezi wa tano MWaka huu wakati Rais wetu Dr JPM akiwaapisha kina Moleli Kama Naibu Waziri pale Dodoma alisema kuwa Balozi wa Kenya Nchini amefanya Mambo makubwa Sana. Rais alifikia mahali akachombeza kuwa anatamani angelikuwa Mtanzania ampatie kazi ya kufanya.

Hii ni kwasababu alisimamia vizuri Sana maslahi ya Taifa lake kuhusu mgogoro uliotaka kuibuka katika mipaka yetu katika kipindi hichi cha Korona.

HEBU TWENDE SAWA HAPA.
Tuachane na hiyo fursa ya Kiswahili aliyoiokoa Mh Rais kule Africa kusini, mwaka 2018 wakati tunakimbizana na wanajeshi kubeba Korosho kule Mtwara na Lindi kwa kukosa soko, Ghana ilikuwa ishauza njee ya nchi yao Korosho za dola Milioni 455.75 Nigeria ikifuatia kwa kuuza Korosho za Dola milioni 190.97 Senegal ikiwa inafuatia nk, wakati huo tuambie ni Balozi gani aliweza kufanikisha hata dili la dola laki mbili la Korosho?..

Mwaka Jana tukipata shida pia ya soko la Pamba lilikuwa haliendi vizuri. Si kwamba Pamba ilikuwa haiuzwi huko njee, kuna mataifa yaliyoongoza kwa kusafirisha Pamba njee ya mipaka yao na kupata fedha ya maana, mwaka 2019 China, India, Marekani, Italy, Benin, Ivory Coast nk ni mojawapo ya nchi zilizoingiza fedha nyingi kutokana na kusafirisha Pamba.

NATAKA KUSEMA NINI
Wakati mabalozi wa mataifa mengine wakihaha na kukamilisha dili mbalimbali kwa manufaa ya mataifa yao kwa Tanzania mwaka 2019 mabalozi wetu badala ya Ku deal na vitu sensitive vya nchi walikuja nchini kuja kutalii kwenye miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Kuna jambo la kujifunza hapa hasa kwa mabalozi wetu ambao wanatuwakilisha kwenye mataifa mengine.

Wanafanya kazi gani huko? Ni dili ngapi nchi yetu inapoteza kwa mabalozi wetu hawa kutokuwa makin? Pamoja na kulinda diplomatic immunity wana majukumu mengine hasa ya kutafuta wawekezeji na fursa kwa watanzania. Wana jukumu pia la kutafuta masoko kwa bidhaa zetu hasa mazao nk.

Tatizo lipo pale pale, tumewapa retired officers kwenda kutuwakilisha kama mabalozi. Kinachotokea wanakuna vipara na matumbo yao tu huko njee na kunywa wisky . Tufike mahali idara zetu ziwapime kwa Impact wanayoiletea nchi si kwa kiingereza wanachokiongea. Hizi balozi ni za kufumua ziendane na mabadiliko ya dunia na hasa ya nchi yetu. Tuna fursa nyingi sana zinatupita...

Kwao Ubalozi ni zawadi si majukumu, ni mahali pa kwenda kumalizia uzee wao nk.

USHAURI.
Ubalozi usiwe tena ni eneo la kuwapa makada wa ccm waliokosa vyeo ndani ya nchi maeneo ya kuongoza. Kama kweli tunataka kukimbia na kasi ya Dunia hapa tuwekeze kwa wataalamu haswa na watu wenye maono. Ni eneo nyeti sana ambalo kama tukilitumia vizuri linaweza kutupandishia thamani mazao yetu haswa. Linaweza Kuongeza Ajira nchini, linaweza kuboost viwanda vyetu Sana.

Eneo hili lisiwe ni la kuwapa watu waliostaafu kwenye majeshi na maeneo mengine. Mtu aliyestaafu akapumzike Labda kama ana kitu cha kipekee sana. Tupeleke watu fresh kabisa kichwani kwenye maeneo haya. Tuwekeze kwenye Ujasusi wa Kiuchumi kwenye hizi ofisi zetu, tupeleke watu wenye uwezo wa kufanya negotiations na kunusa fursa na kuwazidi maarifa mataifa mengine huko njee.

Tuwe na evaluation form kila baada ya mwaka kupima nani ameweza Ku meet mahitaji yetu. Tuwe na vigezo vya upimaji, tunataka balozi afanye nini?
Kama eneo hili litaendeleza utamaduni wa Kale kuhusu kuwapa makada na wastaafu bado tutakuwa na safari ndefu sana.... Ndio maana Kenya aliweza kutupiga hapo S.A.....

Tujitafakari kupitia kauli ya Mh Rais kuhusu Balozi wa Kenya Nchini. Kuna la kujifunza hapa....pamoja na mapungufu ya wakenya ila Wana kitu kikubwa Sana ambacho sisi watanzania tunapaswa kukiiga. Wanajituma Sana kwenye kazi, wanaheshimu muda, wanajua kuchungulia fursa nk. Ndio maana kwenye interview huwa wanatuacha hili ni la kuiga Kutoka kwao. Balozi wao hapa nchini kaonyesha mfano...

TUIJADILI.
Screenshot_2020-05-30 (1) Thadei Ole Mushi Facebook.png
 
com haikwepeki hata pale ufipa wapo wengi ndio maana unaona wanarudi kila siku
 
Mda wa kutawala diplomacy na PR kwa mabalozi hasa wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tz. umepita. Mabalozi wa nchi hizi wanatakiwa kufanya kazi za kutafuta fursa (search for economic opportunities), kukidhi fursa (craft the opportunity value), kuwasilisha fursa (communicate the opportunity value), na kuifikisha thamani ya fursa kwa walengwa (deliver the opportunity value to target society). Ili kufanya kazi hii tunahitaji watu wenye ujuzi na elimu ya leo, wanyumbufu, na wenye uwezo mpana (highly qualified in modern management, versatile, and pervasive). Naunga mkono hoja yako.
 
Back
Top Bottom