Ubalozi China wagomea Risala kwa Kikwete

HuXiang

Member
Apr 13, 2008
36
1
Kama mzazi na kama mwanajamii mwema sioni haja ya kuhoji kuhusi hili kwani ni utaratibu wa ki utendaji. Wakati mwingine kuhoji kila kitu ni kuwafundisha watoto ukaidi usio na sababu, kwasababu kwangu mimi sioni kwa mfano wakifanya wanavyotakiwa kufanya watapungukiwa na nini.

Maadili ya kweli yatapatikana tu pale ambapo mkubwa kwa mdogo wote wana nia njema katika kufanikisha lengo lao na sio kutiliana mashaka kwa kila kitu.
 
Naam,nimepata umbea kuwa wale ndugu zetu wa China(wanafunzi) risala yao imegomewa na ubalozi kusomwa mbele ya Kikwete.

Mkuu Hu,

Heshima mbele, ninahisi kinachotakiwa ni rais kuiona hiyo risala, waombe hao wanafunzi wakupe in e-mail, I promise you na hao wanafunzi kuwa nitamfikishia mikononi mwake, nirushie kwenye pm, wallahi imefika hiyo, kuna ambayo hatuyawezi lakini yapo tunayoyaweza hapa JF, nirushie hiyo kitu mkuu imefika.

Nitumie mkuu, nitampa mwenyewe mikononi na nitamwambia yaliyotokea mpaka ikaishia kutkosomwa huko China, irushe mkuu tukate mzizi wa fitina, hayo yalishatokea Mozambique, na yule balozi alikipata cha moto.
 
mambo mkali haya.

Ubalozi uko Chini , watu wa ubalozi akili zao ziko kichina .Unategemea nini? JK najua angalicheka na kutoa mambo yake kama kawaida lakini ilikuwa ni muhimu sana JK kujua adha ya watu wa Watanzania hata kama hatajali ila ajue anajenga Taifa la wenye chuki na CCM .
 
Mkuu Hu,

Heshima mbele, ninahisi kinachotakiwa ni rais kuiona hiyo risala, waombe hao wanafunzi wakupe in e-mail, I promise you na hao wanafunzi kuwa nitamfikishia mikononi mwake, nirushie kwenye pm, wallahi imefika hiyo, kuna ambayo hatuyawezi lakini yapo tunayoyaweza hapa JF, nirushie hiyo kitu mkuu imefika.

Nitumie mkuu, nitampa mwenyewe mikononi na nitamwambia yaliyotokea mpaka ikaishia kutkosomwa huko China, irushe mkuu tukate mzizi wa fitina, hayo yalishatokea Mozambique, na yule balozi alikipata cha moto.

JK anaenda UN kwahiyo nafasi ya mkuu ES kupigana vikumbo.

Mwambie Mkulu anaweza kushitakiwa kwa manslaughter maana kuahirisha safari yake UK, kuna watu pressure zimepanda juu mno.
 
Mwambie Mkulu anaweza kushitakiwa kwa manslaughter maana kuahirisha safari yake UK, kuna watu pressure zimepanda juu mno.

Mkulu Mtanzania heshima mbele ndugu yangu, unajua mimi ninasema kuwa JF tutaendelea kupiga mawe tena kiroho mbaya and let the chips fall where they may, ndio maana mimi huwa ninawaomba wakulu hapa JF tuwe waangalifu kwenye kutoa hukumu, maana tukizitoa hukumu kila wakati bila uvumilivu kidogo au facts, zinakuwa hazina uzito, lakini tukiwapa nafasi halafu wakaharibu tukiwapiga mawe viongozi wanakuwa hawana jinsi ila kusikiliza, maana wakulu huwa wanapenyeza inquiry zao in private na kuulizia kuhusu some ishus hapa kuwa zimekaaje, kwa mfano mawe yetu hapa kuhusu Butiama, yaliwakosesha sana usingizi wakulu na maswali yalikuwa mengi sana,

Na yale mawe ya ziara ya mkulu UK, yalizua maswali mengi sana in private, na haya ndio majibu yake, sasa mkulu haji huko maana tunajua kuwa makampuni mengi kuanzia bongo mpaka majuu yamealikwa huko kwenye huo mkutano, na yote hiyo ilikuwa ni kwa mgongo wa ubalozi, mama balozi, na rais kuwepo, poor mama balozi kuna wanaomtumia hapo UK kutaka kujitajirisha na kujiiingiza kwenye siasa za CCM, all we can do hapa JF ni kupiga mawe tu, kama nilivyowahi kuahidi huko nyuma hatuna peremende hapa!

I mean kuna yanayowezekana na yasiyowezekana, lakini the worst thing ni kukaaa kimya kama magoi goi maana hatuwezi kujua yapi yanawezekana na yasiyo! Huu mualiko haukuwa umekaa sawa just simple as that,

Mtanzania, wape pole wakuu huko, waambie ni nothing but kumkoma nyani tu mpaka kieleweke, na nothing personal!
 
Unajua vitu vingine ni vya kushangaza.Juzi tu hapa India,Vp alipokuja baadhi ya maofisa walikataa risala ya wanafunzi isisomwe kwa madai eti VP hajaja kuhutubia.Ilikua taabu kweli but impact ya ile risala bado ilikua kubwa na juzi mambo yamekaa shwari.

People's power forever! Hiyo ndio silaha kubwa ya madikteta,mapambano tu!
 
Mkuu FM, I salute!!! Kwa kweli JF ni mwisho wa matatizo!! Haya jamani sasa nasi wenye vimeo tunapata moyo kuwa tikiviweka kwa kweli vitafika panapo penye!!!!

Wakulu wembe ni ule ule!!
 
haya ni moja maswali magumu ambayo vijana walitaka kuyauliza
1.EPA:
Baada ya kuthibitika wizi mkubwa katika akaunti ya madeni nje, aliyekuwa gavana wa benki kuu bw DAudi Balali alifutiwa ajira yake, lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa serikali iliyokuwa ikigharimia matibabu yake nje ya nchi ndiyo inayowambia wananchi kuwa haijui yuko wapi na wala hospital
aliyokuwa anatibiwa, lakini kama haijui yuko wapi je?
tumeshindwa kuvitumia vyombo vya usalama vya kimataifa
ikiwepo Interpol kwa msaada zaidi?

 
Jamani Msinichekeshe
Hii Ni Hatari Sana....muungwana Akifungua Jambo Achelewi Kusema Anrudi China Kuulizia Hiyo Risala...
Muungwana Toka Us Rudi China Upewe Data.....
 
Mkuu Wangu Hu,

Imefika hiyo ninayo tayari, sasa waambie huko ubalozi wake chonjo, maana majibu yatakuja tu, tena sio mbali sana.
 
Ingekuwa ni vigumu kwa balozi yeyote kukubali hii risala isomwe mbele ya Raisi, lets be realistic. Nani anayependa kuona kitumbua chake kinatiwa changa na vitoto vya shule?
 
Katika pitapita zangu nikitafuta Miantiao pale Duolojie nikakutana na vijana wa kichina wakiwa na hiyo Risala wakiiuza kwa dau zito la jiao 10 so nikalipa na kuimwaga hapa muone wana JF. Chapchap kwani sijamalizia Miantiao yangu...

Mkuu Wangu Hu,

Imefika hiyo ninayo tayari, sasa waambie huko ubalozi wake chonjo, maana majibu yatakuja tu, tena sio mbali sana.


risala imetulia
 
ilikuwa ni risala ya wanafunzi au ya wanasiasa sijui wa kambi gani huko china.


wanafunzi wameingiza siasa tena siasa ya msutano kiasi ikataliwe, ukweli haijatulia
 
Mimi naona wote walikuwa wanapoteza muda tu - hao wa Ubalozini na hao wanafunzi - walitegemea kupata majibu gani kwa Muungwana sana sana angewatolea tabasamu na kuendeleza usanii wake serikali ya CCM haina meno yakukabiliana na maovu.

Hili walitakiwa walijue kuwa kesi ya nyani haelpekewi sokwe kuihukumu na Mkuu Field Marshal nakutakia kila la kheri katika upelekaji wa barua utakuwa umefanikiwa kuwapiga bao hao watu wa Ubalozini China kuwa barua imefika, lakini hakuna hatua yeyote itayochukuliwa, mimi sina imani tena na serikali hii kutoa haki kwa raia hahe hohe.
 
Mkuu Hu,

Heshima mbele, ninahisi kinachotakiwa ni rais kuiona hiyo risala, waombe hao wanafunzi wakupe in e-mail, I promise you na hao wanafunzi kuwa nitamfikishia mikononi mwake, nirushie kwenye pm, wallahi imefika hiyo, kuna ambayo hatuyawezi lakini yapo tunayoyaweza hapa JF, nirushie hiyo kitu mkuu imefika.

Nitumie mkuu, nitampa mwenyewe mikononi na nitamwambia yaliyotokea mpaka ikaishia kutkosomwa huko China, irushe mkuu tukate mzizi wa fitina, hayo yalishatokea Mozambique, na yule balozi alikipata cha moto.

Nakuaminia mkuu! Haya ndio mambo. Wenye hiyo risala jamani mpeni huyu mkuu. Hii inazidi kuonesha kuwa JF ni jukwaa linalotumika kujenga nchi
 
Nimeiona na kuisoma hiyo risala. Kimsingi ina mambo mengi ya maana kama unazungumzia ukweli wa jumla na ujumla wa mzungumzaji (yaani isingekuwa imetoka specifically kwa wanafunzi wenye mahitaji yao maalum kama wanafunzi). Lakini kama ni matumizi bora ya fursa (namaanisha rational utilization of opportunities, neno "rational" badala ya "bora" sina kiswahili chake), wanafunzi hapa walihitaji ushauri zaidi. Nasema hivyo kwa maana kuwa fursa ya kukutana na rais ingefaa wao kuyatatua yale immediate issues zinazowakwaza kimasomo, kama hayo ya upungufu wa hela, matatizo ya matibabu, mahitaji ya kompyuta nk, sasa hayo mengine ya EPA na Richmond wangeweza kumwandikia na kumtumia kwa njia ya posta. Unapomdai mkubwa haki fulani, unaweza kuchomeka siasa kidogo kumuonesha una taarifa na uko pamoja nae katika jitihada za kujenga nchi, lakini usizidishe sana hadi ukaonekana kuwa hoja yako ni kumpinga huyo unayemtaka akupatie unachodai. Naona hawa wadogo zangu (na wengine wanangu) wamezidisha pilipili sasa chakula kikawa hakiliki! Ukichukua hii risala, ukafuta kichwa cha habari na kuwakabidhi watu 10, ukawaambia kila mmoja atoe maudhui au hoja kuu ya risala hiyo unadhani wangesema ni nini? Mahitaji yao halisi hawa vijana wameyafanya yakafunikwa na hoja za ufisadi ambazo kuna watu wengine wenye nafasi zaidi ya kupambana nazo kuliko hao wanafunzi, tupo sisi, wabunge wazuri tu kina Mwakyembe, Slaa, Zitto, Kilango na wengine, nk nk, ndio mgawanyo wa kazi, sasa wadogo zetu hawa wanataka wamalize kila kitu kwenye risala moja?

Ninapingana na uamuzi wa ubalozi kuwazuia kusoma risala hiyo. Badala yake wangewashauri tu jinsi ya kuiweka vizuri (unless wamepewa ushauri huo wakakataa), au wangewaonesha maneno wanayoona hayapendezi. Sasa ikitokea kuwa hayo maeneo ubalozi unayokataa ndio maslahi halisi ya wanafunzi, basi hapo ndio wasaa wa kupiga kelele, na kumuwahishia Field Marshal ES amfikishie muungwana. Risala hii kama ilivyo kwa sasa inafanana na hotuba anayosoma mtu dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa, mfano unapomhoji rais kuhusu ajira milioni 1 alizoahidi, sasa sijui ndio unamsuta au ni nini? Na hapo hapo unamwomba akuongezee fedha za kujikimu nk, sasa wewe kipaumbele chako kipi, uongezewe hela za kujikimu au rais atimize ahadi yake ya ajira milioni 1? Vipaumbele, na matumizi rational ya fursa mbalimbali (kama hii waliyopata ya kukutana na mkulu) ndio vinavyowaangusha hawa vijana.
 
Mku mtu wa Pwani labda tueleze mwanafunzi ni nani?? Na kwanini anaitwa MWAnaFUnzi? hapo utabaini kuwa mwanafunzi ni kila kitu,pia jua Ilimu haina mwisho na sisi sote duniani ni wanafunzi ila tu tunatofautiana tunasoma angle gani katika hilo jungu kuu la uanafunzi..Naomba Toa Hoja

mzee kithuku amejibu vyema rejea soma utapata majibu ya masuali yako
 
Back
Top Bottom