Ubaguzi wa walimu wasio wazawa wazidi kushamiri idara ya elimu sekondari Bukoba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubaguzi wa walimu wasio wazawa wazidi kushamiri idara ya elimu sekondari Bukoba.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by opportunist2012, Mar 21, 2012.

 1. o

  opportunist2012 Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tukiwa tunaelekea siku ya kupinga vitendo vya ubaguzi duniani,hali bado ni mbaya katika idara ya elimu ya sekondari manispaa ya Bukoba.Afisa elimu sekondari wa manispaa,afisa taaluma pamoja na baadhi ya wakuu wa shule waendeleza ubaguzi,upendeleo na ukabila katika kuwahudumia walimu walioajiriwa katika manispaa ya Bukoba.Ubaguzi huu uko wazi wazi kwani Afisa elimu anadiriki kuwateua walimu anaotoka nao kijiji kimoja,kabila moja au anaosoma nao pamoja Open University kila katika fursa yenye malipo:iwe semina,kusimamia mitihani ya kitaifa na hata kusahihisha mitihani hiyo.Huku walimu wasiokuwa na uhusiano wa kikabila,kimaeneo na hata kidini wakiachwa bila kuteuliwa kufanya shughuli mbalimbali zinazoongeza kipato.Hali hii imewafanya walimu wanaobaguliwa kukata tamaa kabisa ya kufanya kazi.Wengi wao wanafikiria kuhama au kuacha kazi hii ya ualimu.Walimu wanaoteuliwa kwa sababu ya ukabila,undugu kutoka kijiji kimoja hamna hata siku moja waliokosa kuteuliwa kufanya shughuli hizo maalum yaani kusimamia mitihani,semina na kwenda kusahihisha mitihani.Sidhani hii ndo ile Tanzania aliyoitaka hayati Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere.Sielewi kwanini viongozi wanafumbia macho hali hii ovu ya ubaguzi unaokwenda kinyume na katiba ya nchi yetu.
   
 2. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tupe majina ya Maafisa Elimu hao hapa tuyafanyie kazi na tukupe CV zao pia humu humu. Usimfiche mtu muovu, hatuhitaji watu kama hao Tanzania ya Slaa from 2015!
   
 3. s

  sugi JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  mnawaonea wahaya,ndo walivo,hiyo ndo nature yao,kuibadili n ngumu,fanya utaratibu uhamie ktk sehemu yenye watu wa kawaida
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,735
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Nasikia sababu za ukabila ndio maana hata Kagera Sugar haiendelei. Wanaisusa timu kwa kuwa haiwapi wazawa (Wahaya ) kipaumbele. UKABILA UTAISHA LINI TZ!!!
   
 5. s

  sugi JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Sio TZ,sema kagera kwa wahaya
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  its their nature, nature must obey necessity. Mi nilipangwa Karagwe kwa Wanyambo. Mkuu wa PHYSICS dept akawa mwl wa Civics nikaacha kazi.
   
Loading...