Ubaguzi wa rangi ughaibuni, tupeane maujuzi kuukabili

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,529
196
Nina uhakika wapo wenzetu wenye uzoefu na hii kitu (racism) hasa walioishi ughaibuni more than 10 years watusadie ma-new comer jinsi ya kuwakabili hawa wenzetu maana naona soon uzalendo utanishinda nimtwange ngumi mzungu na kufukuzwa huku wakati sijamaliza kilichonileta.

Naomba mtupe ujuzi huwa mnafanyaje mkizinguliwa na hawa watu kwa sababu ya uafrika wako mpaka kufikia kukaa more than 10 years ughaibuni? Unaweza tupa mifano ya ishu ulizokumbana nazo na jinsi ulitatua au potezea hilo tatizo, itatusaidia sana.

Natanguliza shukrani za dhati!
 
mtegee electronic device urekodi tukio hilo la unyanyasaji either visual au audio....then peleka kwenye ofisi za ubarozi wa nchi yako kama evidence wao watakuelekeza la kufanya...Note. hakikisha wewe sio illegal migrant
 
Vumilia njaa yako hadi utakapomaliza muda wako salama

Ubaguzi upo kila kona ya ulimwengu huu ila kuna kitu kinaitwa kutofautiana
 
acha kutuzingua wazungu wabaguzi? si ndo wanatupa misaada kila kukicha? ungeniambia waarabu ningekuelewa
 
Racism ipo duniani kote we mtu akikufanyia offense kama jamaa hapo juu mrekodi kwa njia yoyote, akiendelea kuongea unaeza toa hata simu mfukoni kizushi bila ye kujua ukatupia voice recorder, huyo anapewa adhabu na mahakama hilo hua ni kosa..
 
Ignore,move on. Ukishindwa sana mpigie kelele mwambie you are racist. Uone atakavyokimbia.
 
Wengi wanaokuja ughaibuni husumbulia mwanzoni na CULTURAL SHOCK, na hii huambatana na athari HASI ambazo ni dalili kuwa u are suffering from it.mifano ya athari hizo ni kama: kutojiamini, wasiwasi, homesick, feelings of being isolated and neglected, under performance kama wewe ni mfanyakazi, depression, lose of appetite, self alienation yaani unajitenga mwenyewe, kwa wale ambao hawana social skills hujikuta inakuwa vigumu kutengeneza marafiki wapya as a result of self alienation, hisia za kujiona unadharauliwa na kubaguliwa, developing inner hatred kwa jamii inayokuzunguka, upweke na kadhalika.
Hizi ni baadh ya symptoms ambazo zinaweza kukujulisha kuwa umepata cultural shock.
Nini ufanye:
1.Potezea, mara nyingi utakutana na matukio ya kukuudhi au kukushangaza, mf. Unapokaa kwenye siti ya basi au treni hakuna anaekuja kukaa na wewe, kushangaliwa rangi na nywele zako n.k dont panic, EXPECT IT ila jaribu kupotezea
2. Jifunze utamaduni wa hapo ulipo ughaibuni, hii itakusaidia kuwajua na kuanza kuchangamana nao na utaelewa miiko na desturi zao. Hivyo baadhi ya mambo utagundua kumbe si kwamba wanakufanyia wewe kama foreigner ila labda ni mila, tamaduni au tabia zao
3.keep yourself busy. Mind you that ideal mind is a friend of devil.
4. Try to make new friends, be sociable.
5.be flexible, usiwe muhafidhina (conservative).
6. Fanya mazoezi, haya yanasaidia kukujenga kiakili na kihisia.
7. Be kind to all people. Hii itakusaidia kuprove them wrong kama wanakuonesha ubaguzi. Mfano kwenye Subway au Bus, akija mzee amekosa siti , mpishe akae. Hii itakujengea heshima na it works for real.
8. Dont be too argumentative. Mind you uko ugenini na wewe mtu mmoja huwezi kuwabadilisha,.mambo mengine chukulia poa,na mara nyingine keep your mouth shut.
ALL IN ALL JIFUNZE KUADAPT MAZINGIRA AND BE OPEN MINDED!
 
Soma falsa za Marcus Garvey na Malcom X. Ubaguzi haupingwi kwa mtu mmoja mmoja bali ni tabaka la watu wa jamii mmoja kuonyesha kwamba wanaweza kujiongeza au kujitawala kwa manufaa ya jamii nzima.

Afrika ikipiga hatua kama bara si mtu mmoja mmoja basi heshima kwa mweusi itakuwepo. Mfano Afrika kuna wachezaji nje ya bara wanacheza soka katika viwango vya juu lakini hiyo haitamfanya mzungu asimbague mweusi. Lakini mpira wanaocheza akina Eto'o wangeupigia ligi za Afrika na hao wazungu wakaja afrika kucheza ligi zetu basi kiwango cha ubaguzi tungekipunguza.

Ebu niambie mkuu ikiwa mwanasheria mkuu wa serikali anaambiwa na kampuni ya wazungu awape ushauri wa kisheria katika mkataba watakaoingia na serikali ambayo yeye anaisimamia na wananchi hawaoni tatizo, hapa mtu mweusi ataendelea kubaguliwa.

Ikiwa mtu ni kiongozi anakula rushwa na hela anaenda kuweka bank za nje na wananchi wanaona sawa tu, mzungu hapa anaona hamnazo.

Zana ya kupambana na ubaguzi ni pana na ipo zaidi jamii baguliwa kuonyesha uwezo wa kujitawala kufikia malengo ya jamii nzima.

Mfano: wakati wa ubaguzi wa mfumo nchini marekani (jim craw laws) na kwingine kama afrika kusini ( apartheid) mtu yeyote asiye mzungu alikuwa anabaguliwa isipokuwa mjapani alikuwa na hadhi fulani kwa sababu walishaendelea. Wachina wakajitutumia kiuchumi na wakorea hadhi yao ikapanda, wakaja india kwasasa hadhi yao imepanda. Mtu mweusi ndo amebaki chini na mara nyingi ukiongolea ubaguzi unaongelea mtu mweusi kubaguliwa. Kwasababu weusi walidai uhuru wajitawale wameshindwa, watawala wa kiafrika wanatumiwa na mataifa ya wazungu na makampuni ya wazungu hivyo kuiweka heshima, uhadilifu nk vya mweusi pabaya.

Marcus Garvey anasema afrika ikionyesha uwezo na kujikomboa kiuchumi mengine yote yatafuata, wanaobagua waafrika wataacha wenyewe.

Wazungu hawambagui mtu mweusi kwa sababu ya rangi bali jamii ya watu weusi hawaonyeshi udadisi, uwezo na nia ya kujikomboa, hivyo mzungu anaona wote hamna kitu.
 
Bora ukabaguliwe ughaibuni kuliko ubaguzi huu unaofanyiwa ndani ya nchi yako na haohao wazungu,
Nenda migodini,mahotelini,viwandani uone mambo yanavyofanyika utalia kaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom