Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,108
- 18,326
Tumekua tukisikia kwamba mkuu wa nchi ni mbaguzi hasa linapokuja swala la mitazamo ya kisiasa, kitu ambacho si kuzuri na hakifai kwa mkuu wa nchi.
Tofauti na viongozi wengine, hata marais waliopita, Mheshimiwa hapa amefeli na inaonyesha anafanya makusudi.
Jana akiwa Msoga, diwani wa hilo eneo aliitwa atoe kero. Mh akadhani ni diwani toka chama cha Chadema kwa sababu hakuvaa sare ya CCM, akaamuru anyang'anywe mic na maneno makali juu lakini baada ya kuuliza chama gani akaambiwa ni wa CCM, mara moja akaamuru arudishiwe mic na aendelee kuongea.
Leo tarehe 29 June 2020 akiwa Kilosa akaanza kumponda mbunge wa eneo na kusema wananchi wa eneo hilo wanachagua kwa jazba akiamini mbunge wa eneo hilo ni wa Chadema. Anaongeza kwa kusema yeye angekua mbunge wa eneo hilo angekua amemaliza changamoto zote ila kwa sababu wananchi wanachagua kwa jazba na wanachagua wabunge sio, ndio maana bado changamoto zipo.
Baadaye akauliza mbunge wa hapo anaitwa nani na wa chama gani? Wananchi wakamtaja na kumwambia anatoka chama chamapinduzi. Bila hata aibu akaanza kumsifia na kuahidi kuzimaliza changamoto hizo akisadiwa na waziri husika.
Wananchi wa Tanzania sio watoto wanajua na wanaelewa vizuri, wao wanapendana bola kujali vyama, dini wala kabila lakini bado kuna viongozi karne hii wanasimamia ubaguzi.
Naamini mh Rais ana nia njema na Tanzania, lakini bado ana nafasi ya kuondoa hurka hii ya ubaguzi hata kama chadema walimpa wakati mgumu 2015.
Rais ndio kiungo pekee cha kuwaunganisha Watanzania.
Sio sababu ya yeye kuendelea kubagua vyama vya upinzani hali kazi zake alizo zifanya zinaonekana.
Haya mambo madogodogo yanamuondolea kitu fulani kama kiongozi.
Tuungane kuupinga ubaguzi. Na asilazimishe vyama vya upinzania kupata ajenda.
Prof Jay