Ubaguzi wa kikanda waanza kuitesa CCM

Status
Not open for further replies.
Dec 11, 2010
3,321
6,328
Akihutubia wananchi wa Kongwa wanaogoma kuondolewa kwenye maeneo yao kwa nguvu ili kupisha wawekezaji Job Ndugai ameonyesha dhahiri kuwa kuna kauli za ukanda za kuwabagua wana Kongwa zilizotolewa na aliye kuwa mkuu wa wilaya ambaye ni mmasai.

"... huyo bwana ametoa kauli huku akisahau kuwa naye ni mmasai"

Chanzo: ITV habari.

My take.

Haya ni maumivu ya ubaguzi wa dhahiri kama jinsi chama chake kilivyo kuwa kinaeneza propaganda za ukanda na udini ambazo zinaendelea kulitesa taifa.

CCM ikiwazwa sana na mtu mwenye akili nzuri ataishia kuwaona viongozi na mashabiki wake kuwa niwa jinga wa kupuuzwa.

kwa nini

Tangu Tanzania ipate uhuru karibu mawaziri wakuu 4 wametokea Kaskazini lakini hili halija wahi kuwa tatizo kwetu watanzania.

1. Edward Moringe

2. Cleopa Msuya

3. Fredrick Sumaye

4. Lowassa (aliyejiuzuru kwa kashfa ya rushwa).

Hao wote ni kutoka kaskazini lakini kwa kuwa shida yetu haikuwa kujadili watu wala maeneo wanayotoka bali uwezo, hakuja wahi kuwa na kelele za ukanda kwa upande wa wananchi.

Wakati huohuo, ukiacha takwimu za nyuma kabisa, baraza la mawaziri la kwanza la utawala wa raisi wa sasa (jk) ambapo kauli za ukanda zimeshamiri kwa kasi lilikuwa na manaibu na mawaziri kutoka Kaskazini 21. Wengi kutoka kanda yoyote. lakini bado wakisimama kwenye mimbari za kisiasa utasikia chadema ni chama cha ukanda!

chadema wanachosema kuwa nicha ukanda uongozi wake wa juu kabla ya MM na mzee Said Arfi kujiuzuru ulikuwaje?

1. Mh Mbowe (Mwemyekiti) - Kanda ya Kaskazini, Hai K'Njaro

2. Said Arfi (Aliyekuwa makamu mwenyekiti bara) - Kanda ya Magharibi, Mpanda.

3. Dr Slaa (Katibu) - Kaskazini, Karatu

4. Zitto Kabwe (Naibu katibu) - Kanda ya Magharibi, Kigoma.

Makamu mwenyekiti na Naibu katibu Zanzibar mmoja kanda ya Unguja na mwingine kanda ya Pemba.

Huo ukanda wanao ughani CCM na mashabiki wao wenye ukame wa maono kila siku kuhusu ukanda wa chadema ni upi?

Mbona huwa hawasemi kuwa chadema ni chama cha kanda ya magharibi wakati nafasi za uongozi zina uwiano sawa?!

Angalizo.

Ukisikia watu wa ccm wanaghani ukaskazini jua kuwa hawamaanishi Tanga, Arusha, wala Manyara bali wanaendeleza chuki za kijinga na kipuuzi dhidi ya Wachaga.

CCM wametuletea ugonjwa mbaya wa ubaguzi ambao Mwl Nyerere aliukemea kwa sauti yenye mwagwi mkali.
 
Mkuu, nilidhani ungekuwa sahihi kama ungeandika kuwa, sera za ukanda kama zinavyoshadadiwa na chadema zina madhara makubwa kama ilivyoanza kujitokeza huko kongwa
 
Siku zote ccm hubagua wamasai,ndio maana govt ya ccm huwatengea maeneo ya kufuga na kuishi peke yao!hawana huduma muhimu za kibinadamu
 
Chadema badala ya kuhamasisha umoja na mshikamano wa kitaifa, nyie mmekalia ubaguzi na utengano
 
Siku zote ccm hubagua wamasai,ndio maana govt ya ccm huwatengea maeneo ya kufuga na kuishi peke yao!hawana huduma muhimu za kibinadamu
Mkuu, mbona huku kwetu Mvomero wamasai wamejaa kweli na tunawavumilia katika mengi ikiwa ni pamoja na tabia zao za ubabe, kulisha mifugo shambani na hata kufanya mauaji. Nadhani wamasai ndo wanapendelewa zaidi na serikali
 
Kuna haja ya mods kuandaa kirufe cha Dislike. Mada kama hizi tungekuwa tunajivinjari kwa kugonga tu Dislike
 
Jamani, mimi nina swali moja katika hii mada. Tanzania tunajulikana kuwa na ardhi kubwa ingawa matatizo kati ya wakulima na wafugaji serikali imeshindwa kuypatia ufumbuzi. Na kama tuna ardhi kubwa hivi ni kwa nini kila wanjapokuja wawekezaji tunalazimika kuhamisha raia wetu ili mwekezaji apate ardhi? Kwa nini mwekezajia asitafutiwe ardhi huko pembeni asiwabughudhi raia wetu kwenye ardhi yao?
 
Mkuu, tatizo lipo kwa hao wawekezaji wenyewe. Badala ya kuchagua kuweka miradi yao kwenye maeneo wazi, wao wanataka yale ambayo yanakaliwa na wananchi
 
Jamani, mimi nina swali moja katika hii mada. Tanzania tunajulikana kuwa na ardhi kubwa ingawa matatizo kati ya wakulima na wafugaji serikali imeshindwa kuypatia ufumbuzi. Na kama tuna ardhi kubwa hivi ni kwa nini kila wanjapokuja wawekezaji tunalazimika kuhamisha raia wetu ili mwekezaji apate ardhi? Kwa nini mwekezajia asitafutiwe ardhi huko pembeni asiwabughudhi raia wetu kwenye ardhi yao?

Swali la msingi ndilo hili, safi sana mkuu.
 
Mkuu, mikoa haijatengwa kibaguzi, ndo maana utaona mkuu wa mkoa au wilaya mmasai anaongoza Singida. Hii ni rofauti na sera za chadema
kama usimayo ni kweli myika asingegombea dar, hiyo ni hakili yako finyu,ila nakuuliza ukanda na umikoa ni kipi kimekaa kikabila zaidi?
 
kama usimayo ni kweli myika asingegombea dar, hiyo ni hakili yako finyu,ila nakuuliza ukanda na umikoa ni kipi kimekaa kikabila zaidi?
Mkuu, ndo maana alienda kugombea Ubungo ambako kumejaa wachagga wenzake. Mbona hajawnda kugombea Temeke au Kigamboni?
 
story haijakaa sawa, japo sio vyema kuzungumzia utendaji kazi wa mtu kwa kulinganisha na kabila yake!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom