Yohana Shija Masalu
Member
- Nov 8, 2013
- 33
- 28
Historia ni mwalimu mwema. Historia inamulika kuonesha mwanadamu alikotoka, alipo kwa sasa, na inampa mwanga wa kujua anakokwenda. Ni historia inatuonesha kwamba chimbuko la mwanadamu ni jamii mmoja kwa maneno mengine ni shina mmoja. Hili likasindikizwa na Imani mbalimbali za kidini ambazo zote hukiri ya kwamba chimbuko la Mwanadamu ni Moja. Ndipo wengine huita Muumba. Kumbe kwa maneno mengine twaweza sema binadamu wametoka kwenye familiya mmoja, ya baba mmoja na mama mmoja. Hili ndilo chimbuko lao. Familiya hii ya baba mmoja na mama mmoja ilizaa watoto mbalimbali wengine wanene, wengine wembamba, wanjano, weusi, wekundu, weupe, wanene, n.k wote hawa kama zao la familiya hii. Inapotokea mmoja ya watoto kumwona mtoto mwenzie kana kwamba si ndugu yake ujue namna yaake ya kufikiri si sawa. Ni mgonjwa na fikira yake ni finyu katika kuchambua na kunyumbua mambo. na hivyo anastahili adhabu ya kumsaidia kumrudisha katika mstari wa kufikiri vizuri na sahihi.
Ni ukweli usiopingika kuwa binadamu ni binadamu tu. Rangi, kabila, dini, itikadi, ukwasi, umaskini, ujinga n.k ni manjonjo tu. Mtoto akizaliwa mahali fulani kwa mfano akazaliwa Moshi nchini Tanzania na akahamishiwa maeneo ya uheheni huko Iringa Tanzania angali na umri wa mwezi mmoja, akakulia na kuzeekea huko huko Iringa bila shaka kama hatajuzwa na mtu mzima hatajijua kama alizaliwa Moshi. Kwa mantiki hiyo atakua katika mazingira ya kihehe akifuata mila na desturi za kihehe. Kama ni ulanzi na ugimbi ataujua vizuri sana kuliko mbege. Ni mtu mzima anayeweza kumwingizia mambo ya ukabila kwa kumsimulia kuwa yeye siye mhehe. Chuki inaanza namna mtu huyu alivyojuzwa historia yake. Alivyopandikiziwa manjonjo mbalimbali. Ndiyo kusema ubaguzi wa kikabila, rangi, itikadi, dini n.k ni matokeo ya fikra mbovu na potofu ya mwanadamu.
Inashangaza sana kuona mtu anamnyanyasa mwanadamu mwenzie eti kisa ni wakabila tofauti. Mwajili anaajiri watu kwa ukabila. Dini inafanywa ya kikabila. Siasa nayo kadhalika. Uchumi ndo usiseme. Kwa mtindo huu tutafika wapi? Kwani kifo hutubagua? kwanini Kumnyanyasa ndugu yako, mwanadamu mwenzio, wafamiliya mmoja, ya Mwumba mmoja? Mtu asipewe kazi leo, akiwa wa mahali Fulani naa kabila la JOWA kuanzia mpishi, walinzi, madreva, wahasibu, madaktari n.k wanakuwa wa JOWA. Je hii ni haki? Kwanini mtu asiajiriwe kwa sababu anakidhi vigezo na si jinsia, kabila, rangi, uzuri wa sura n.k? Mambo ya uzuri au ubaya wa sura yanatuhusu nini siye? Kabila linatuhusu nini siye? Rangi yake inatuhusu nini siye?
Wakoloni walitunyanyasa kwaa sababu ya ukoloni wao. Leo hii tena tunanyanyasiana kwa sababu ya ujinga wetu. Kifo kitakuwa mchungaji wetu. Chenyewe hakibagui. Haya yote Historia aliye mwalimu mwema anatufundisha. Ijue historia ujifunze kufikiri kiakinifu na kiusahihi.