Ubaguzi au Maslahi Kisiasa?

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Katika Mikoa tofauti na hekaheka za kisiasa za CHADEMA kumetokea vifo viwili ambavyo vyote vimehusishwa na Polisi kwa njia moja au nyingine.

Vifo hivyo ni vya watu wenye fani zinazotegemeana, mmoja ni Mwandishi wa habari za magazetini na mmoja ni muuza magazeti. Wote hao ni wadau wakuu wa magazeti na wote hao ni wapenzi wa Chadema.

Cha kushangaza ni pale tunapoona mmoja kapata kila aina ya huruma kuanzia viongozi wa chadema mpaka wanaharakati wa hakiza binaada na "exposure" iliyotukuka kwenye TV, magazeti, maandamano, wana harakati, michango ya maziko, michango kwa aliowaacha, ahadi za kutazamwa familia yake na hata kusomeshwa wanawe na mwingine akisahauliwa kabisa.

Tumeona maziko ya mmoja ya kiongozwa na Viongozi wa Kitaifa wa chadema na kurushwa kwenye magazeti na kwenye mitandao, mwengine yule sijui hata kama alijulikana kazikwa wapi.

Watu hao ni:

Ally Singano - Muuza Magazeti
Daudi Mwangosi- Mwandishi wa magazeti.

Jee, ni Ubaguzi au Maslahi ya Kisiasa?
 
Both ... mkuu Zomba mim nashangaa sana viongozi wa CDM wa kitaifa wanavyoligeuza suala la kifo cha Mwangosi kuwa ni suala la kisiasa na kuacha suala la muuza magazeti kuwa ni suala la kiutendaji. Huu ni mchezo mbovu wa wanasiasa na wanaoumia ni walalahoi.

By the way, Dr. Slaa alipata wapi cell number ya IGP mpaka akamwandikia text? .... Ask yourself.
 
Akili kichwani...

Umesahau similarity moja kwamba katika mazishi yote CHADEMA walikataliwa kushiriki. Kwa Singano wakapotezea kwa Mwangosi wakang'ang'ania mpaka wakashiriki.
daudi-mwangosi-slaa333.jpg

Akili kichwani...

Umesahau similarity moja kwamba katika mazishi yote CHADEMA walikataliwa kushiriki. Kwa Singano wakapotezea kwa Mwangosi wakang'ang'ania mpaka wakashiriki.
Kwanini waling'ang'ania? Kwa sababu Mwangosi is more of a public figure na ni rahisi kumtumia kipropaganda.

Usitake kuleta stories za makande kaka huo ndiyo ukweli. It's a shame kumtumia marehemu kisiasa.
 
acha udini wewe kiumbe ... huu ni udhaifu mkubwa sana unaotokana na malezi .. mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

hata watoto wako na wajukuu wako watakuwa wadini ...

what a silly thread
 
zomba, jambo hili kwa hakika limewahuzunisha sana maelfu ya watanzania. Lakini pia limezidi kuwaweka wazi CDM, mwenye macho haambiwi tazama! Ilikuwa ni muhimu sana kucapitalize katika huu msiba wa mwandishi ili kujinufaisha kisiasa.
 
acha udini wewe kumbe ... huu ni udhaifu mkubwa sana unaotokana na malezi .. moto umleavyo ndivyo akuavyo

hata watoto wako na wajukuu watakuwa wadini ...

what a silly thread
Sasa hapo dini imeingiaje?
 
acha udini wewe kiumbe ... huu ni udhaifu mkubwa sana unaotokana na malezi .. mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

hata watoto wako na wajukuu wako watakuwa wadini ...

what a silly thread

Wewe umeingia kwenye religious line unnecessarily...
 
Ndio maana Maggid Mjengwa a.k.a Mwenyekiti alipoenda Nyololo akasema nendeni mkajionee hali halisi...
 
Kwanini waling'ang'ania? Kwa sababu Mwangosi is more of a public figure na ni rahisi kumtumia kipropaganda.

Usitake kuleta stories za makande kaka huo ndiyo ukweli. It's a shame kumtumia marehemu kisiasa.

Ni kweli. Ndio maana baada ya Slaa kutumiwa ujumbe kuwa this time polisi watakuwa wakali na kuwakamata viongozi yeye "akachelewa" kufika kwenye shughuli ya ufunguzi wa matawi.
Lakini cha kushangaza, pamoja na kwamba yeye ndio mgeni rasmi lakini shughuli iliendelea bila yeye kuwepo!

Yeye kaingia mitini ili asikamatwe halafu kawaambia wanachama wasisikilize polisi "mpaka kieleweke" ili itokee vurugu wacapitalize kisiasa. Ndio maana kamati ya mazishi ilipowaambia hawaruhusiwi kushiriki kama chama Slaa alitokwa na mishipa ya shingo, aliona jitihada zote za kutafuta umaarufu wa kisiasa zinataka kupotea dakika ya mwisho.
 
Huwa wanawasiliana mara kwa mara na RPCs, OCDs na mpaka IGPs, Slaa hawezi kwenda mahali kwenye mkutano wa hadhara bila kuwasiliana na Polisi na nahisi huwa wanawasiliana sana na IGP, la sivyo asingekuwa na cell phone number yake.
 
Kwa hiyo Slaa kawaingiza vijana chaka yeye kalala mbele. Kile kibabu kinaonekana kimechoka kumbe kitoto cha mjini!!!
 
Huwa wanawasiliana mara kwa mara na RPCs, OCDs na mpaka IGPs, Slaa hawezi kwenda mahali kwenye mkutano wa hadhara bila kuwasiliana na Polisi na nahisi huwa wanawasiliana sana na IGP, la sivyo asingekuwa na cell phone number yake.

Nakubaliana na unachosema, ndio maana RPC alipofika kwenye tukio alisema "hapa hakuna kiongozi wa kitaifa, wale watoto siyo viongozi wa kitaifa". Ukijiuliza RPC alijuaje nani yupo na nani hayupo wakati milango ya ofisi za CDM ilikuwa imefungwa?!
 
Ila day by day watanzania wanaona their true colour. Ndio maana napenda M4C iendelee ili wale waliokuwa wanasikia kwenye radio na kuona kwenye TV tu vituko vya hawa jamaa wajionee live.
 
Nakubaliana na unachosema, ndio maana RPC alipofika kwenye tukio alisema "hapa hakuna kiongozi wa kitaifa, wale watoto siyo viongozi wa kitaifa". Ukijiuliza RPC alijuaje nani yupo na nani hayupo wakati milango ya ofisi za CDM ilikuwa imefungwa?!
Mtandao umeshehena ila wananchi tunawastukia!!
Subiri chaguzi za vyama ngazi ya taifa.
 
Back
Top Bottom