Ubadilishaji wa viongozi/watendaji hauwezi kuitakasa CCM machoni mwa watanzania

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katika jitihada za kuiipa CCM uhai mpya kuna tetesi kwamba chama hicho kiko mbioni kufanya mabadiriko makubwa katika safu yake ya watendaji wakuu na baadhi ya viongozi waandamizi.Hata hivyo, kulingana na maoni ya wadadisi wa mambo, chama hicho kikongwe kikitaka kunusurika, mbali na mabadiriko hayo kinayokusudia kufanya, hakina budi kuanza kuchunguza uwezekano wa kurejelea sera zake za zamani za ujamaa na kujitegemea. Maoni hayo yanatokana na ukweli kwamba, baada ya chama hicho kukumbatia ubepari kimejikuta kinatengana na wananchi wa kawaida walio wengi na badala yake kuungana na walio nacho wachache wanaotumia chama hicho kufilisi uchumi wetu. Aidha chama hicho kimegeuzwa kuwa pango la waharifu wa kila ainal wezi, wanyang'anyi. majambazi, wauza unga n.k. Hali hiyo imekifanya chama hicho kupoteza hadhi yake machoni mwa watu wengi.Ni kutokana na sababu hizo zinazowafanya watu wengi kuamini kwamba, bila ya kurejelea siasa zake za huko nyuma uhai wa chama hicho huko mashakani.
 
Eti kufanya mabadiriko makubwa katika safu yake ya watendaji wakuu na baadhi ya viongozi waandamizi? Thubutuu! Ni vigumu, given the status quo
 
Back
Top Bottom