Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,354
- 17,902
Kwenye vyombo vya habari jana kuna taarifa inaonyesha Waziri wa Fedha Philip Mpango akitiliana sahihi kupokea msaada wa USD 600 Million kutoka Taasisi ya The Global Fund ambayo ndiye mfadhili mkubwa wa dawa za Malaria, Kifua Kikuu na Ukoma. Katika makabidhiano ilionekana kuna USD 400,000 zilizoletwa mwaka 2018 ambazo matumizi yake hayaeleweki. Waziri Philip Mpango alisema hivi;
"Kuhusu ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani 400,000 zinazodaiwa kufujwa na baadhi ya Watendaji wa Serikali wanaotekeleza mradi huo hapa nchini, Dkt. Mpango ameuahidi Mfuko huo kwamba Serikali itachunguza na kuwachukulia hatua kali watu wote waliohusika na vitendo hivyo"
My Take:
1.0 Serikali ya Awamu ya 5 ndiyo inajinasibu kuwa inapambana ma ufisadi, imekuwaje vyombo vyetu kuanzia TAKUKURU, CAG, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha wasigundue ubadhirifu huu hadi aje Ofisa wa Global Fund kutoka Ulaya ndiyo mushituke?
2.0 Au tuungane na wanaposema hii ni awamu ya wapigaji wa kutisha kuliko awamu zote?
3.0 Au mnataka kila kitu asimamie Magufuli? Hata hili ambalo liko wazi Philip Mpango anasema anakwenda kuchunguza?