Ubadhirifu wa USD 400,000 za Sekta ya Afya: Philip Mpango alikuwa wapi mpaka aambiwe na Global Fund wenyewe?

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,817
2,000
Kwenye vyombo vya habari jana kuna taarifa inaonyesha Waziri wa Fedha Philip Mpango akitiliana sahihi kupokea msaada wa USD 600 Million kutoka Taasisi ya The Global Fund ambayo ndiye mfadhili mkubwa wa dawa za Malaria, Kifua Kikuu na Ukoma. Katika makabidhiano ilionekana kuna USD 400,000 zilizoletwa mwaka 2018 ambazo matumizi yake hayaeleweki. Waziri Philip Mpango alisema hivi;

"Kuhusu ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani 400,000 zinazodaiwa kufujwa na baadhi ya Watendaji wa Serikali wanaotekeleza mradi huo hapa nchini, Dkt. Mpango ameuahidi Mfuko huo kwamba Serikali itachunguza na kuwachukulia hatua kali watu wote waliohusika na vitendo hivyo"

My Take:
1.0 Serikali ya Awamu ya 5 ndiyo inajinasibu kuwa inapambana ma ufisadi, imekuwaje vyombo vyetu kuanzia TAKUKURU, CAG, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha wasigundue ubadhirifu huu hadi aje Ofisa wa Global Fund kutoka Ulaya ndiyo mushituke?

2.0 Au tuungane na wanaposema hii ni awamu ya wapigaji wa kutisha kuliko awamu zote?

3.0 Au mnataka kila kitu asimamie Magufuli? Hata hili ambalo liko wazi Philip Mpango anasema anakwenda kuchunguza?
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,262
2,000
Kwa mazingira ya kukataa kukosolewa na kuzuia shghuli za kisiasa na Uhuru wa kutoa maoni na vitisho vinavyotolewa serikali ya awamu ya tano. Itajikuta ndio serikali ambayo ina janga kubwa la rushwa na ufujaji/ ufisadi kuliko awamu zote ambazo aidha zinaigusa Ikulu yenyewe au taasisi zake au watumishi wake.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Hili swali sio valid!

Mimi nikikupa milioni 100 ununulie gari la wagonjwa, wewe ukazitumia kununulia Range Sport na kumpa kimada wako, nani atajua mimi nilikupa pesa na ni za nini?

Ni mpaka mimi niliyekupa pesa, nitakapokuja tena kwako na kukuambia naomba nionyeshe gari ya wagonjwa uliyonunua, hujaonyeshwa ndipo unaripoti. Dr. Mpango ni mpokeaji tu, unapofanyika ubadhilifu, bila ya yeye kuambiwa, atajuaje?

P
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,817
2,000
Bajeti ya sekta ya Afya inafadhiliwa na na mataifa ya Ulaya na America kwa takriban 80%. Yaani kwa kila Shillingi inayotumika kutibu binadamu Tanzania, Senti 80 imaletwa na wafadhili kwenye dawa za ukimwi, malaria, Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Chanjo za watoto na magonjwa yaliyo sahauliwa.

Unashangaa nchi tegemezi kama hii, wafadhili hao hao wakiuliza kuhusu utawala bora tunawaita mabeberu.
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,817
2,000
Pascal Mayalla,
Mpango kazi wa Fedha za Mfuko huandaliwa mapema na kushirikiana na maafisa wa Afya na Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia TACAIDS. Yote yanayopaswa kufanyika yanakuwa yameainishwa na yako wazi kabla ya Fedha hazijaingia nchini.

CAG ana wajibika kuzikagua kwenye kazi zake za kila mwaka na kutoa ripoti. Nao Global Fund wanafanya kaguzi zao kila mwaka na kutoa ripoti.

Kwa hiyo hakuna excuse kwa Philip Mpango kutojua ubadhirifu huu kabla ya Global Fund.
 

Schmidt

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
5,085
2,000
Hili swali sio valid!.
Mimi nikikupa milioni 100 ununulie gari la wagonjwa, wewe ukazitumia kununulia Range Sport na kumpa kimada wako, nani atajua mimi nilikupa pesa na ni za nini?.
Ni mpaka mimi niliyekupa pesa, nitakapokuja tena kwako na kukuambia naomba nionyeshe gari ya wagonjwa uliyonunua, hujaonyeshwa ndipo unaripoti. Dr. Mpango ni mpokeaji tuu, unapofanyika ubadhirifu, bila ya yeye kuambiwa, atajuaje?.
P
Kwahiyo wajibu wake unaishia kwenye kuzipokea pesa tu? Baada ya hapo ni kila mtu kivyake?
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,510
2,000
Mnamshangaa Rais anapopata hela na kuingiza kwenye miradi kama barabara, na ununuzi wa meli, reli na ndege yote hayo ni kupunguza wizi Sasa mtakula reli?

Ingawa bado watu wanahujumu na kuiba lakini bora zinazopatikana zinaingizwa mahali
Hatutaendelea hata siku moja na tutabaki tegemezi tu mpaka kiyama


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,346
2,000
Magufuli anasema wizara umiza kichwa ni wizara ya mambo ya ndani,hapana mimi nasema wizara yenye matatizo sugu na pasua kichwa ni wizara zinazohusika na afya( wizara ya afya+ tamisemi).

Yaani fedha zinapigwa kwa sana tuu, ndiyo maana tutazidi kufa kama kuku hasa uku vijijini.Tatizo lingine kubwa ni ukosefu wa usimamizi thabiti (leadership and governance). Kwa mfano maelekezo mengi yanayotolewa na tamisemi huko mikoani na mawilayani kuhusu huduma za afya hayatekelezwi na wala hakuna wa kufatilia kwa ukaribu.

Wasimamizi wa afya wanapwaya sana hasa ngazi ya mkoa na wilaya.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Kwahiyo wajibu wake unaishia kwenye kuzipokea pesa tu? Baada ya hapo ni kila mtu kivyake?
No hata wewe kwenye matumizi ya nyumbani kwako, ukiishatoa pesa ya kununua kila 20 za mchele na kumpa wife, wife nae kampa dada, wewe huwa unarudi jikoni kukagua kama hizo kilo 20 zimenunuliwa?. Anayepaswa kukagua ni wife, asipokujulisha kuwa nimekagua jikoni, dada kapiga, wewe huwezi kujua.
The end user sio MOF.

Enzi za Mkapa, mhasibu mkuu wa wizara fulani kwa kushirikiana na mtu wa procurement walikuwa wanapiga pesa ya wafadhali, vifaa vinanunuliwa, pesa zinalipwa, kumbe hewa!.
Final end user asiporipoti, wewe mtoa fedha huwezi kujua, wewe utatoa pesa, utapewa risiti, bidhaa zimenunuliwa na zimetumika kumbe watu wamepiga.

P
 

uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
5,595
2,000
Pascal Mayalla,
[/QUOTE]

Paschal Kaka hapa umekosea!

Kuna assumption moja we must make kwamba viongozi wa serikali wanapaswa Kuwa na weledi......

Kwa hiyo unataka kusema mifumo ya serikali yote ni ya kipigaji na wanaotoa ndo wanawajibika kukagua?

Kama hiyo ndo argument yako, then na wewe utakuwa mtu wa hovyo na wa ajabu kabisa katika Tanzania!

Sisi tunatakiwa kuamini na Kuwa na assumption kwamba viongozi wana weledi, Sasa kama hawana, how do you hold them responsible?

Hii comment ni ya hovyo kabisa kuandika na mtu kama wewe! Yani Hauamini kabisa weledi na uwajibikaji wa serikali bila kufuatwa!
 

Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,583
2,000
Kwa hiyo watatoa au barua imeshapenya mbona wanatanguliza upigaji walioubaini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom