Ubadhirifu wa fedha ktk Halmashauri ya Mwanga

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Wanajf:
Hususani wale Wa Mwanga kwenye mtandao huu,Naombeni ni zungumze machache juu ya Mwanga yetu, Tushauriane na Tushirikiane kuleta ukombozi Mwanga na Tz nzima Chini ya Chadema.

Bado naendelea kufanya tafakari ya yanayojitokeza wilaya ya mwanga.
Kwenye moja ya gazeti la mwananchi juma lililopita ilichapishwa taarifa ya mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali wakaonyesha kwamba uongozi wa halimashauri ya wilaya ya mwanga kwa mwaka ulioishia 30.06.2011 hakuna fungu la fedha lililopelekwa kwenye kijiji hata kimoja jambo ambalo limekemewa kwenye taarifa ile; lakini hilo linatokana na ama madiwani wetu na wenyeviti wa vitongoji kutojua jinsi* taratibu za serikali zinavyoelekeza kama kufanya mikutano mikuu ya mwaka kwa kila kijiji na wananchi kusomewa mapato na matumizi ya mwaka na watendaji wa vijiji hali kadhalika wananchi kuhoji pale ambapo wanafikiri kuna utata. Hata hivyo mbunge wetu akiwa kama msomi wa hali ya juu huwajibika kuwaelimisha madiwani na viongozi wa kata na hata wananchi namna serikali inavyofanya kazi ili waweze kdai haki zao pasipo viini macho. Huo ni udhaifu mkubwa uliojengeka wilani kwetu na sehemu nyingi za nchi yetu.
Habari nyingine ya kuthibitika ni kwamba lile lambo lililojengwa kati ya kijiji cha ujamaa Lwami na Ibwejewa ambalo halikutumika hata mara moja lilisomba Tshs 38.7 millioni ambazo kwa zimeenda mifukoni kwa watu kadhaa katika uongozi wa Mwanga. Fedha hizi zingeweza kutumika kuchimba visima virefu viwili kando ya bomba la kusambaza maji lililokuwa limewekwa tangu utawala wa Nyerere na kufanya marekebisho madogomadogo pale ambapo pangekutwa panavujisha maji na hatimaye kuwanusuru wafugaji wa vijiji vitatu na mifugo yao.
Suala la barabara zetu za asili ni jambo lingine la kusikitisha; kwa mfano ukipita kwenye barabara ya kwenda vuchama ndambwe utaikuta haina tofauti kabisa na wakati ule wa ukoloni hayati mzee Zuberi Shedehwa Mfinanga akiwa Mlao alivyokuwa amewahamasisha wana Shighatini,Mfinga, Ndambwe, Vuchama Ndambwe na Thongoa kujichimbia barabara ile kwa maendeleo yao; miaka takribani hamsini na miwili sasa tangu tupate uhuru barabara ile iko vile vile lakini utakuta inatengewa mafungu ya kuifanyia ukarabati na halimashauri yetu ya mwanga na linalofanyika halionekani. Ni lazima wananchi wahoji yote haya ili kuweza kuokoa fedha za maendeleo kutoingia mifukoni mwa watu wachache waliopo kwenye uongozi.
Uozo huo ukienda huko ugweno; Uasngi, Kilomeni na kadhalika utakuta mambo ni hayo hayo.
Wananchi wanapaswa kuwa makini sasa kuhoji mapungufu yote hayoa.

Wananchi wote wa Mwanga popote pale tulipo Duniani, Tusimame sasa wenyewe badala ya kusubiri misaada yaani kawaida ya Mwanga imekuwa sasa ni kuhongwa Uwaziri kwa kila Mbunge anayetokea Mwanga, Ujinga huu wa kutufunga macho hatutaki, Nitasimama imara katika hili na kuhakikisha watu wa Mwanga hatupigwi changa la macho tena.

Tabia ya kuambiwa ni chaguo la fulani ni kiini macho, Tu chague wenyewe matatizo tunapata sisi wanyonge hawo wajuu hawajui wala hawataki kusikia.

Tambarare yote kwasasa hali ni mbaya sana ya maji,Afya na Elimu, wakati wilaya ya mwanga ni moja ya wilaya za kwanza kupata maendeleo kipindi cha ukoloni.

Watu wote Wema muishio nje ya Mwanga ila mnauchungu na Mwanga Ungeni mkono harakati hizi za M4C kukomboa Taifa letu.

Henry Kilewo
Katibu mkoa
Kinondoni na Dsm
Never say Never
2015 CDM we Can
29/09/2012
 
mkuu jitahidi ujue kero za kila kijiji,tatua matatizo kadiri uwezavyo sasa, kura utapata 2015,usisubiri dk za mwisho
 
Lugha iliyo tumika nina mashaka nayo sijui ni Kipare au Kiswahili nimesoma sijaelewa
 
Umesomeka mkuu, na wale viongozi wengine tokeni hadharani. Kampeni mitandaoni, fungueni na blogs kabisa na mzitangaze kwa wale wanaoweza access. Maeneo yaanzishwe mabaraza ya vijana, wekeni hata tv na inverter kama hakuna umeme vijana wakutane jioni. Kitanda hadi kitanda, nyumba hadi nyumba!! Mpaka kieleweke.
 
Umesomeka mkuu, na wale viongozi wengine tokeni hadharani. Kampeni mitandaoni, fungueni na blogs kabisa na mzitangaze kwa wale wanaoweza access. Maeneo yaanzishwe mabaraza ya vijana, wekeni hata tv na inverter kama hakuna umeme vijana wakutane jioni. Kitanda hadi kitanda, nyumba hadi nyumba!! Mpaka kieleweke.

www.kilewo2015.blogspot.com
 
mkuu jitahidi ujue kero za kila kijiji,tatua matatizo kadiri uwezavyo sasa, kura utapata 2015,usisubiri dk za mwisho

Mkuu Tunajenga chama Mwanga na kuwaeleza wajibu wao wa kuwajibisha viongozi kwa kutokutatua kero zao, Na kuwaeleza jinsi kero hizo zinavyoweza kutatulika kama wenye dhamani wakiacha kuchumia matumbo yao!
 
Enheeeeee, nkitafuta na mie? Chioni mahusiano hayo.

Mbunge anawajibu wa kurudi kwa wananchi kutimiza ahadi alizo ahidi kwenye kampeni, kama mbunge harudi jimboni nani wa kutatua kero? Mbunge huyo alihusika kwenye sakata la 38.9M. Kwasasa ni hayo ila yanakuja mengi mutayaona humu humu jf baada ya wakazi wa mwanga kuyasikia.
 
Kilewo,
nilifikiri uozo ni huku kwetu same tu, kumbe umesambaa mpaka mwanga. kusema ukweli kuna ulazima wa kuzikomboa wilaya za same na mwanga toka makucha ya ukoloni wa ccm. tunakutumia salamu toka same na kukuhakikishia kwamba tuko pamoja katika harakati kurudisha heshima ya wilaya za mwanga na same, ambazo miaka ya mwanzo ya uhuru zilijulikana kama pare district.
 
Mueleze Mfinanga na Mchome hao wakikubali tutashirikiana, wakikataa endelea kuandika makala.
 
Mbunge na pesa za halmashauri wapi na wapi.

Au mtoa mada amekosea. Kwani mtendaji mkuu wa halmashauri ni Mkurugenzi (DED) na sio Mbunge.

Pitia vizuri kujua mamlaka ya nchi yako hususan kazi za Mbunge na DED.

Pole sana
 
...Sasa hapo ni Mwanga yamkataa Mbunge au Kileo amtuhumu Mbunge wa Mwanga?...
 
Back
Top Bottom