Ubadhirifu wa dawa zenye thamani ya Tshs 26.7 billioni wabainika kwenye Hospitali za Rufaa za mikoa 28 Tanzania bara

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,596
3,639
Timu ya ukaguzi maalumu kutoka Wizara ya Afya imegundundua ubadhirifu huo wa dawa na vifaa tiba kutoka hospitali hizo za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Kula 2019 hadi Desemba 2020. Hayo yametangazwa leo na Waziri wa Afya Dr Dorothy Gwajima wakati akitoa taarifa ya uchuguzi huo uliotokana na malalamiko ya wananchi ya kukosa dawa mara kwa mara kila wakienda kutibiwa kwenye hospitali hizo. Taarifa kamili soma kiambatanisho hapo chini

IMG-20210301-WA0051.jpeg
IMG-20210301-WA0052.jpeg
IMG-20210301-WA0053.jpeg
 
Mfumo wa afya wa nchi hii lazima ubadilike kinyume na apo mtakuwa mnawaonea watumishi kila siku kuwa wanawaibia dawa.
Hospital na na vituo vya afya vilivyochin ya serikali huduma za misamahaa ziko juu kuliko wanaolipia so kujiendesha n kaz
Kama nchii tuamue if tunatoa huduma za afya kama sehemu ya kusaidia wanachi au tuiendeshe sekta ya afya kama private sekta kina aga khan.
Nb wananchi wasifurahie iyo kashfa anayoieneza Mama coz kinachofuata n maumivu kwao maaana sasa huduma zinaenda kuwa ghali kwao kwa lengo la hospital kupata faida na kujiendesha kama taasisi binafsi
 
Hii naunga mkono kuna wizi mkubwa sana wa dawa yaani balaa.
Mama Gwajima hafai sababu anakurupuka Bambi comedian type. Aende pale mtu sirias aondoe hili janga kwa Taifa.
 
Kwani hawajui upigaji upo?
Sio tu kutaja ngapi zimepigwa bali ni lazima waonyeshe njia ya kuzuia upigaji
La sivyo kila mwaka wataleta takwimu za hasara tu
 
Huyu mama wangemuhamishia Takukuru ili aedelee kuwanasa wabadhirifu huku nadhani......., well sijui kwanini naona kama anapwaya
 
Hii naunga mkono kuna wizi mkubwa sana wa dawa yaani balaa.
Mama Gwajima hafai sababu anakurupuka Bambi comedian type. Aende pale mtu sirias aondoe hili janga kwa Taifa.
 
Wakati anaunda tume na kamati lukuki ajue huku mahospitali HAKUNA DAWA hata Muhimbili yenyewe
Amfikirie mtu aliyelipa tshs 1500000 kwa mwaka halafu akifika hospitali anaishia kuandikiwa dawa akanunue kwa fedha zake
Pia atoe suluhisho la kwa nini maduka ya dawa ya watu binafsi hawakubali kupokea order za NHIF (tetesi:; huwa bila mlungula hawalipwi).
 
Mlungula kivipi mkuu? Fafanua tujifunze wengi hapa
 
Wizara ya Afya imebaini upotevu wa Sh26.7 bilioni za dawa uliosababishwa na uzembe, kutojali katika usimamizi wa mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya, viashiria vya hujuma, wizi na udokozi wa bidhaa za dawa.

Hayo yamesemwa leo Machi Mosi, 2020 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Doroth Gwajima wakati akitoa tamko kwa vyombo vya habari kuhusu matokeo ya ufuatiliaji huo.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa huduma ya dawa na vipimo katika vituo vya kutolea huduma katika ngazi zote kinyume na matarajio, jumla ya thamani ya fedha ambayo imethaminishwa kwa upungufu huu inakadiriwa kuwa siyo chini ya Sh26.7 kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Desemba 2020,” amesema Dk Gwajima.

Amesema kufuatia malalamiko hayo, wizara iliunda kamati ya wataalamu kutoka Wizara na taasisi za sekta mbalimbali ili kufanya ufuatiliaji katika hospitali 28 za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18.

“Lengo ilikuwa kubaini changamoto zinazochangia upatikanaji duni wa dawa na vipimo licha ya kuongezeka kwa mtaji wa dawa,

Jumla ya bidhaa za dawa na vipimo 20 hadi 30 tu kati ya nyingi zilizo kwenye orodha ya bidhaa za afya kwa kituo husika ndiyo zilifanyiwa ufuatiliaji kuanzia ununuzi, mapokezi na matumizi,” amesema Dk Gwajima.

Mwananchi
 
Timu ya ukaguzi maalumu kutoka Wizara ya Afya imegundundua ubadhirifu huo wa dawa na vifaa tiba kutoka hospitali hizo za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Kula 2019 hadi Desemba 2020. Hayo yametangazwa leo na Waziri wa Afya Dr Dorothy Gwajima wakati akitoa taarifa ya uchuguzi huo uliotokana na malalamiko ya wananchi ya kukosa dawa mara kwa mara kila wakienda kutibiwa kwenye hospitali hizo. Taarifa kamili soma kiambatanisho hapo chini

View attachment 1714846View attachment 1714847View attachment 1714848
Watumishi wa umma sekta ya wamekuwa Kama ndo kafara la kwa hii wizara
 
Suala la Afya Tanzania ni changamoto kubwa sana, pamoja na kwamba muda mwingine tunailaumu Serikali kwa mambo kadhaa kwenye afya ila watumishi nao wamekuwa sehemu ya hizi changamoto, wapo radhi watanzania wenzao wakose huduma na hata wafe kwa ubinafsi wao wa kuiba vifaa tiba, madawa nk.

Bila shaka wahusika watachukuliwa hatua kali wawe mfano, sitarajii hatua kali za kuhamishwa vituo vya kazi.
 
Wizi wa dawa ni biashara kubwa sana kuna kipindi Marekani kupitia usaid ilikuwa inatoa msaada wa dawa za malaria Tanzania lakini dawa hizo zilikuwa zinakutwa zinauzwa Angola walipoamua kufatilia qakakuta kontena likifika airport linapotea
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom