kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Yafaa serikali kuwatambua wahusika na kuwaburuza kwenye vyombo vya sheria baada ya serikali yenyewe kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi. Vinginevyo itakua ujinga hii hadithi ya huduma ya afya kwa umma. Si siri dawa na vifaa vingi vya afya vinaibiwa na kuuziwa maduka binafsi.Timu ya ukaguzi maalumu kutoka Wizara ya Afya imegundundua ubadhirifu huo wa dawa na vifaa tiba kutoka hospitali hizo za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Kula 2019 hadi Desemba 2020....
Maduka binafsi mengi yanategemea kama supplier serikali kwa dawa na vifaa vinavyoibiwa serikalini. Mtu anapata kazi ya kudumu halafu anakua kama mwekezaji serikali bila kuwekeza kitu kwa kujipatia faida kubwa kwa kuuza dawa na vifaa vya afya mali ya serikali.
Huu ni wazimu lazima ukomeshwe.