Jumba la Mkuu wa Chuo Dkt Richard Masika analojenga Njiro Arusha
Viwanja vitatu vya Richard Masika vilivyopo USA- Arusha
Sasa habari ya ubadhirifu na ufisadi wa Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt Richard Masika si kitu cha kuficha wala siri tena. Picha alizopiga na kutuma kwa rafiki zake kwa maneno ya kumdhihaki Mhe Rais ya 'HAPA KAZI TU' akimaanisha majumba na viwanja hivyo alivipata kwa kile alichoita hapa ni kazi tu ni kama zilivyowekwa hapo juu. Majumba hayo ya gharama kubwa yamejengwa kwa kutumia sehemu ya matofali 20,000 yaliyochukuliwa na Mkuu wa chuo hicho Dkt Richard Masika kutoka katika ujenzi wa jengo la madarasa la chuo kwa kutumia madaraka yake.
Matofali hayo yangetosha kujengea madarasa 20 watoto wetu wakayatumia kusomea katika sehemu mbalimbali ambapo wanafunzi wanasoma kwa msongamano kwa kukosa madarasa ya kutosha. Kweli hapo ni kazi ya ubadhirifu na ufisadi tu