Ubadhilifu mkubwa wa viwanja unaofanywa na Chadema Jiji la Mwanza

Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.

Chadema wapo makini sana ndiyo maana wameamua kumfukuza uanachama huyu Matata Henry kumbe huyu jamaa ni fisadi wa kutupwa!
 
Utatunga chochote ili mradi uongelee cdm

Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.
 
Kumbe CDM wamegeuka maafisa ardhi?
Basi hatuna waziri mkuu kama kafumbia macho utapeli basi ajiuzulu.

Kwa hiyo cdm sasa wameizidi nguvu seikali ya chama cha mapinduzi?

Viwanja unavyo viongelea ni vya mwanza sehemu gani?
 
Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.
 
Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka
Thursday, 26 July 2012 20:36


Patricia Kimelemeta
MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi.

Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika.

Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu.

Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete.

Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi.

Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF)

Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mng'ong'o na Mwanakhamis Kassim Said.

Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu.

Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwang'onda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga.

Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM).

Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe.

Wananchi waja juu
Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni.

Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao.

"Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine," alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa).

Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha.

"Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida," aliongeza.

Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge.

Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake.

"Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi," alisema.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo.



 
Ritz unajaribu kupotosha umma wa Watanzania.Fuatilia kwa makini ujue kamati zakugawa viwanja kama kuna diwani hata mmoja.

Hati haipitii hata kwa meya kuidhinisha ,inatolewa na idara ya ardhi na ikishatolewa haiwezi batilishwa au kufutwa hata kama ilitolewa kwa makosa na hata madiwani mkihoji hamna mamlaka ya kufuta hati ila mnachoweza kufanya ni kumwadhibu afisa mipango miji na hati inabaki kama ilivyo mpaka Raisi ndie mwenye mamlaka ya kufuta hati.

Sheria hii ndio inayowapa mamlaka wakurugenzi ambao ndio wako kwenye kamati ya kugawa ardhi kuamua nani apate kiwanja nani asipate na kwa vigezo hata vya rushwa.

Kwa utaratibu huo ndio unaona migogoro ya ardhi haiishi na inaendelea hata kwa sehemu ambazo zinaongozwa na CCM.

Acheni kuwasakama madiwani bila sababu ya msingi.Hata hivyo nilimshangaa sana Waziri Mkuu kutamka waulizwe madiwani wa CDM HUKU AKIELEWA KUWA SIO KAZI YAO KUGAWA VIWANJA.
 
Ndo maana matata akapigwa chini na cdm.lakin matatizo ya viwanja bado ni tatizo la utendaji wa kabwe.ndo maana wananchi walimwambia pinda aondoke nae.yule ndo fisadi mwenye viwanja kila kona ya jiji
 
Mkuu hippocratessocrates,

Ubadhilifu unaofanywa na madiwani wa Chadema ni kuhodhi viwanja vinavyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza, viwanja vingi wamejigawia wao, diwani mmoja ana viwanja zaidi ya 20 ukiitaji kiwanja unanunua kwa diwani.

Mkuu kuna viwanja vimepimwa maeneo ya Kiseke, Nyegezi, Bugarika, ukienda Halmashauri ya Jiji la Mwanza wanakuambia vimeisha lakini ukionana na madiwani wa Chadema wanavyo wanawauzia wananchi.

Mkuu Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambayo ipo chini ya Chadema imechafuka kwa rushwa.

Mkuu Ritz, thanks for the update lakini nilivyokuwa najua

1. Kiseke: Eneo la viwanja liligawiwa zamani na eneo kubwa lilipewa kanisa(kujenga chuo fulani) na pili viligawiwa na ndipo kwenye nyumba takribani 700 za NSSF) maeneo mengine yako wazi hadi kule majengo mapya)

2. Bugarika: Hili ni eneleo la "mjini mjini" na nijuavyo mini vuwanja viligawiwa kati ya 2009/10..yaani kabla ya uongozi wa hao CHADEMA.


3. Nyegezi: Sina uhakika upande upi ule wa St. Augustine, Luchelele, au upi...lakini ni huko huko ican tell you mkuu Ritz, kuna mkubwa mmoja anaeneo lake KUBWA tu ambao upatikanaji wake ni utata.


let me do some digging,mkuu.
 
Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.
ritz unajua mambo mengine unayoleta hapa yanakushushia heshima ya utu uliyobakiwa nayo kwani akili najua huna,hili ni jukwaa la magreat thinker tafakari kabla ya kuandika
 
Huyo mkubwa si ni wilison kabwe mbona unamumunya maneno?tena anajenga hotel ,hata kiwanja cha kikwete kipo luchelele!
 
@ritz thread kama hii huwa unapata shilingi ngapi ili na mimi nijiunge upande wenu naona huwa unajitahidi kila wiki lazima ushuke na single ya CDM.
 
UFISADI mkubwa wa madiwani wa CHADEMA wakishirikiana na watendaji wa halmashauri husika. Pongezi kwa RC wa Kilimanjaro kwa kushitukia ubadhirifu Moshi Mjini
 
La msingi ni kupata data za kweli. Ila kama ni kweli hii peoples power inarudia yale yale basi hakuna ukombozi. Majina na namba za viwanjwa yawekwe hadharani na wapewe muda wa kulipia. Ufisadi mwiko CDM.
 
Wanabodi,

Wakazi wa Jiji la Mwanza wanalalamika ugawaji wa ardhi unaofanywa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza watendaji wa Halamashauri wakishirikiana na madiwani wa Chadema ambao ndio wengi kwenye baraza la madiwani.

Wananchi wa Mwanza wanalalamikia ubadhilifu wanaofanywa na madiwani wa Chadema kujigawia viwanja maeneo ya Kiseke, Nyegezi, Bugarika, na sehemu tofauti tofauti katika Jiji la Mwanza.

Wananchi wa Mwanza walipeleka malalamiko yao kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofanya ziara katika Jiji la Mwanza, Waziri Mkuu aliwambia wakazi wa Mwanza malalamiko yao wanatakiwa wayapeleke kwa chama cha Chadema, ambacho kina dhamana ya kuendesha Halmashauri hiyo, ambao Chadema wana nafasi ya Meya hadi madiwani

Wananchi wa Mwanza wanalalamika unafanyiwa utapeli na Halamashauri ya Jiji la Mwanza viwanja hawapewi pamoja na kuwa wameishavilipia pesa lakini viwanja hivyo vipo mikononi mwa madiwani wa Chadema.

Mh watakuwa na mikono mikubwa kweli hawa yaani ........ushabiki mwingine bwana.
 
Huyu Ritz anafikiria kwa kutumia masaburi. msameheni bure!! Kama hajui hata wanaogawa na kupima viwanja anafikiri ni madiwani! Basi mnabishana na chizi!!

Au ni Adam Chagulani anawachafua wenzake kwa kuwa katimuliwa nini?
 
Mkuu wangu hippocratessocrates,

Kama unataka kiwanja Luchelele tafuta milioni 4 utauziwa madiwani wa Chadema wanavyo lakini ukienda Jiji wanakuambia vimeisha.
 
Last edited by a moderator:
Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.
Kwenye nyekundu nimehamasika kujua maana ninakaeneo mbali na mjini nadhani hii technology itanifaa kukaleta mjini

Madiwani wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti wa kamati ya mipango ya Jiji la Mwanza Matata Henry, wanagawana viwanja, kutoka sehemu tofauti tofauti.
Asante kwa kuyakuza ili yaeleweke vizuri!.

ritz unajua mambo mengine unayoleta hapa yanakushushia heshima ya utu uliyobakiwa nayo kwani akili najua huna,hili ni jukwaa la magreat thinker tafakari kabla ya kuandika
Mkuu Marire labda hujamuelewa vizuri Ritz!.
Kama sijaelewa vibaya, ni kuwa wamekusanya viwanja kutoka sehemu tofauti tofauti alafu wakaanza kuvigawana!.
Sasa huu utaalamu watufundishe na sisi tuweze kukusanya vilivyoko vijijini tulete mjini tugawane!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom