Ubadhilifu malisili -halmashauri ya bagamoyo mtushi mmoja atolewa kafara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubadhilifu malisili -halmashauri ya bagamoyo mtushi mmoja atolewa kafara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurunzi, May 11, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mtumishi wa mmoja wa Halmashauri ya Bagamoyo Erick Mnon'gona ambaye alikuwa ni mkusanya ushuru wa wamzao ya miti jana amepandishwa kizimbani kwa makosa ya udhadhilifu wa fedha zaidi ya sh mil 60.

  Amekutwa na mashitaka yapatayo 300 na alitakiwa kulipa dhamana ya sh mil 30 au hati ya nyumba iliyofanyiwa tathimini hata hivyo mshitakiwa aliekana mashitaka na kupelekwa lupango kwani alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.

  Binafsi nimekuwa nikifuatilia sana sakata hili la ubadhilifu wa idara ya maliasili almashauri ya Bagamoyo, Huyu kijana watakuwa wamemtoa kafara kwani kwa mujibu wa habari nilizonazo sinasema TAKUKURU Waligundua zaidi ya milioni 100 zilitafunwa na wakuu wa idara lakini walitembeza mlungula kwa maafisa hao wa TAKUKURU na ndupo walipoamua kutoa kafara kijana huyo ili kuwalinda wabwana wakubwa.

  Mfano mkuu wa idara hiyo anayejulikana kwa jina la Msaki anavijana wake ambao wapo kwenye mapori ya bagamoyo wakishirki katika ufanikishaji wa uvunaji wa miti na mkaa kinyume na taratibu.

  Huyu jamaa kwa pale bagamoyo ni mmoja wa wanaojulikana wanautajiri mkubwa unaotokana na kutumia cheo chake kwa maslahi yake, anamiliki mashamba karibu vijiji vyote bagamoyo mfano pale kidomole anaheakari zaidi ya mia 600.
   
Loading...