Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 680
- 1,338
Hivi majuzi Rais Magufuli alifanya ziara ya gafla kwenye ujenzi wa machinjio ya kisasa vingunguti Jijini Dar es Salaam.
Kwa maelezo ya Mh Rais Magufuli ni kwamba kupitia mradi huo wa ujenzi wa machinjio kuna ufisadi mkubwa umefanyika.
Leo tena katika dhifa ya kuwaapisha Viongozi Ikulu amerudia swala hilo kwamba jengo la ghorofa moja linajengwa kwa zaidi 14 Billion.
Sanjali na hilo pia Mh Rais Magufuli amezunguzia harufu ya Ufisadi mwingine kwenye ujenzi wa fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Baada ya rejea hizo zote naona mashambulizi mengi kwa RC Makonda kana kwamba yeye ndiye mhusika Mkuu wakati Jiji hili linangozwa na Meya kupitia vikao na Madiwani.
Watu wa kulaumiwa ni Madiwani ambao ndio wanapanga bajeti na kuidhinisha hiyo miradi, na sisi Wananchi kimsingi ndio tunawachagua kupitia masanduku ya kura.
RC Paul Makonda anaweza kuwa na madhambi yake mengine lakini tuache'"vijiba' vya roho kwa vitu ambavyo vipo wazi kwamba tunajua au tunapotosha makusudi kwakuwa tu tunamchukia huyu Kijana
Alex Fredrick
Dar es salaam