Elections 2010 Ubabe wa Makamba... ashinikiza mwanae awe mbunge....

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
313
7
Hivi unajua kwamba mzee makamba aliwahi kufukuzwa shule baada ya kumpa mimba mwanafunzi wake yeye akiwa mwalimu????

Jee unajuaaliyemshauri nyerere makamba apewe nafasi kwenye chama ni marehemu mzee kawawa baada ya kumuona akiwa anacheza sana ngoma kwenye sherehe.....

Jee unajua kwamba mzee makamba alishawahi kugombea ubunge jimbo la bumbuli mara mbili akashindwa.

Mwaka huu sasa amempeleka mwanae january makamba akagombee jimbo lile aliloshindwa yeye na kushndana na mzee shelukindo ambaye alimshinda.
Safari hii anaenda akiwa yeye ndiye katibu wa chama cha ccm ambacho ndicho mwanae anachotumia kugombea, na pia mwanae huyo akiwa akifanya azi na raisi, mwenyekiti wa chama.

Wengi tunamjua january makamba japo hata kama sio sana.
Kinachotokea sasa ni kwamba mzee makamba anatumia nafasi yake kushinikiza kijana wake ndio aje awe mbunge w bumbuli kwa hali yoyote...mazingira yote yanaonyesha na dalii zote zinaonyesha hivyo nitatoa baadhi ya mifano:

1. Kuna vipepelushi jimboni bumbuli vinavyosema mbunge wa 2010 bumbuli ni januarymakmba na kama kun wanachama hawana makadi ya chama basi wawasiliane na viongozi wa chama.....

2. Mzee makamba akiwa ktka ufunguzi wa shule katika kata ya tamota, alimuita january aje akae karibu na mzee sherukindo na kumuambia mzee sherukindo amroge kama anaweza, pamoja na kutoa maneno ya kejeri..

3. Mzee makamba ameonana na makatibu wa kata wote wa jimbo labumbuli na kuwataka wafanye kazi moja tu ya kumtangaza january, mkutano wa kwanza ulifanyika, mahezanguru...

4. Baadhi ya makatibu kata waliogundulika kutomuunga mkono january makamba au kushindwa kutoa ushirikiano katika kampeni mpaka sasa wamesimamishwa kazi kwa amri ya makamba japo viongozi wa wilaya waliwapa tu onyo, makatibu 2 wamesimamishwa na wengi wamepewa onyo.

5. Baadhi ya watendaji wa kata pia wamebadilishwa na kutolea jimboni bumbuli baada ya kubainika hawaungi mkono kampenza january katika maeneo yao, watendaji wa mgwashi na bumbuli wamehamishwa...walihisiwa kusaidia mbunge aliyepo madarakni.

6. January makamba amefanya kampeni za wazi katika kata zote kwa mikutano ya hadhara ikiwa ni pamoja ni kutoa pesa hadharani kwa wananchi lakini hakuna aliyechukua hatua na badal yake ccm mkoa imeamua kusamehe yaliyopita wakati huohuo wakilalamikia mzee sheluindo kufanya kampeni japo ni kazi yake bado kukutan na wnanchi wake, lakini la january ahalikusemwa na kusemwa la mheshimiwa....

7. January amefnya mikutano n wazee na akina mama katika kata za vuga,mgwashi na bumbuli kwa kuandaa vyakula na kutoa pesa kwa wahudhuliaji wote, lakini hilihalijasemwa na mtu pamoja na kulalamikiwa na wananchi...

8. Januar anapigiwa kampeni na viongozi wa chama kinyume na kanuniza chama, hata ktika misafara yke huongozana na viongozi hao.

Yapo mengi yanayolalamikiwa na wananchi na hata viongozi wa chama lakin hakuna hatua zinazochukuliwa....kisa ni mtoto wa katibu mkuu na mtu wa karibu wa mwenyekiti wa chama (raisi)...

Zipo tetesi kwamba january anatumika kumuondoa tu mzee shelukindo na hata yeye dio sera anayonadi na sio kutaka kusaidia wananchi, katika sherehe ya kufungua shule yake mzee makamba aliashukuru marafik wake waliomchangia kina rostam azizi, yusuph manji.....na mzee lowasa.

"kakia ka mbuzi kahaghia kahelala"....mkia a mbuz hufagia pale unapolala...ndio usemi maarufu wa mzee makamba na labda ndio maana toka amewahi kuwa kiongozi amekuwa akisaidia eneo moja tu analotoka,na sio jimbo lote au wilaya yote au mkoa wote.....

Mambo bao...
 
Niliwaambia siku zamani kwamba hata chizi wa wodi ya vichaa akisimamishwa kwa tiketi ya ccm atashinda. kwa sababu ccm ni majambazi wa kura ktk uchaguzi na sisi ni wanyonge tuliofungwa na nira ya umoja wa kitaifa wa mashaka
 
Tofauti ya Shelukindo (MB) na Januari (MB mtarajiwa) nini? Wote CCM na wote wanatafuta chakula?

Of all the places - Mkoa wa Tanga hautakiwa kuwa maskini kama ulivyo!!! Ni fikra duni na ubinafsi unawamaliza

Kuanzia bandari - mpaka mashamba ya mkonge - vyote kwishnei - Sababu ni Shelukindo au Januari ataleta nini kipya?

Sababu tunazifahamu - bila kubadilisha mfumo yote ni kama kumpigia mbuzi gitaa!!
 
Wananchi wa Bumbuli wana akili za kujua nani anatakiwa kuwa mbunge wao.

Haya ya kukimbilia na tuhuma kibao hapa JF ni ya watu ambao wameshindwa kwenye siasa za hoja na sasa wanakimbilia kwenye siasa za kuchafuana.

Ubunge agombe January, nyie mnatumie muda wote kumuongelea babake, why? January ana miaka zaidi ya 18, ana maamuzi yake na mshambulieni yeye kwa matendo yake na wala sio matendo ya baba yake. Hivi nyie mkiwa judged kwa matendo ya baba zenu, mtakuwa wapi?

Mkipigwa bao mwezi wa 10 mnaanza kusema CCM wameiba, kumbe mlipotakiwa kuwaelemisha wananchi, nyie mnakimbilia kumwaga matusi JF. Hapa JF hatuchagui wabunge.
 
Kama mtoto wa Makamba ni mtanzania ana hahi ya kugombae ubunge,kama ni mwana CCM ana haki ya kuwa mgombea wa CCM.Cheo na umaarufu wa baba yake havimnyimi haki hizo.
 
We Gender sensitive udaku unaujua?? wa2 wanajaribu kufichua maovu ili kuleta mabadiliko we unasema ni udaku!!

Kama haya yaliyosemwa ni ya kweli, ilistahila makamba ajiuzulu kabisa huo ukatibu wa chama, na astakiwe kwa kumpa mimba mwanfunzi,
na kufanya kampeni b4 time.
 
Hivi unajua kwamba mzee makamba aliwahi kufukuzwa shule baada ya kumpa mimba mwanafunzi wake yeye akiwa mwalimu????
Jee unajuaaliyemshauri nyerere makamba apewe nafasi kwenye chama ni marehemu mzee kawawa baada ya kumuona akiwa anacheza sana ngoma kwenye sherehe.....
daaah huyu ndio Makamba ambae ni Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi. kwa hiyo yule mwanafunzi ndio alie mzaa January ?
 
Chama cha Mapinduzi...kwa "ubaba na umwana" mbona mtakoma sana saivi...usultani mambo leo, uimla au sijuwi tuuite nini..ndo upo huo na utakuwepo tu...moja tu ndo lamsingi...agombee Shelukindo au J.Makamba...wote hao wanatumikia chama kibovu kilichoshindwa ku meet matarajio ya watanzania masikini tokea uhuru mpka leo...pengo la walionacho na wasiokuwa nacho limekuwa kubwa na sababu ya hayo ni wao CCM...hata akigombea malaika kutoka mbinguni, achilia J Makamba ua Shellukindo,kwa tiketi ya CCM, bado CCM ni ilele na sera za kuwazidishia ujinga, maradhi na umasikini wananchi ndo zile zile hawana jipya.
 
Huyu sie yule mtoto wake aliyefukuzwa kazi ya Uhakimu kule mahakama ya mkoa sababu ya ulevi? If so anawezeje kuwa mfano mwema kwa jamii atakayoiongoza?
 
Huyu sie yule mtoto wake aliyefukuzwa kazi ya Uhakimu kule mahakama ya mkoa sababu ya ulevi? If so anawezeje kuwa mfano mwema kwa jamii atakayoiongoza?
Sio yule wa Moshi huyu mwingine
 
binafsi sioni ajabu manake imekuwa kama fashion kila kigogo anajitahidi kumwingiza mwanae either kwenye ubunge au NEC na pia kwenye nafasi za juu kwenye UVCCM. Habari ndio hiyo wajameni
 
CHADEMA wako wap katika haya mabifu yanayoweza kuwafaidisha? mnatakiwa kuwa strategic hata kuongea na mzee Shelukindo kuangalia uwezekano wa kumnasa atakapokataliwa kusimamishwa na kama mgombea kwa tiketi yaCCM
 
marhabaa baba enock yaani umenikuna vilivo mie kweli hapo hakuna jipya ni umasikini we acha hivi tanga kunani palee....
Conquest -nikipata chance na mie fisadi
 
Huyu sie yule mtoto wake aliyefukuzwa kazi ya Uhakimu kule mahakama ya mkoa sababu ya ulevi? If so anawezeje kuwa mfano mwema kwa jamii atakayoiongoza?

Mkuu,

Mtoto/watoto wa wakubwa hawafukuzwi kazi Tanzania ya leo, Kijana wa makamba ni kweli ni mlevi wa kutupwa na mzembe wakubwa walichokifanya walimhamisha kutoka Moshi Mjini wakampeleka wilaya ya Rombo,,anakula Taska baridi huko,, TZ kila kitu kinawezekana kwa wakubwa
 
Tofauti ya Shelukindo (MB) na Januari (MB mtarajiwa) nini? Wote CCM na wote wanatafuta chakula? Of all the places - Mkoa wa Tanga hautakiwa kuwa maskini kama ulivyo!!! Ni fikra duni na ubinafsi unawamaliza Kuanzia bandari - mpaka mashamba ya mkonge - vyote kwishnei - Sababu ni Shelukindo au Januari ataleta nini kipya? Sababu tunazifahamu - bila kubadilisha mfumo yote ni kama kumpigia mbuzi gitaa!!

Excellent....CCM itoke jamani!!!
 
Back
Top Bottom